Beat kuwa Mali ya msanii au producer nadhani ni kutokana na mkataba na jinsi makubaliano yalivyo. Kwa navoelewa mimi kipindi hicho producer majani alikua anamiliki beat zake ndio mana hata alikua hawauzii wasanii alikua anawarekd bure kabisa ila yeye alikua anamalizana nao kwenye mapato ya shows na mauzo ya Album
Ndio maana hata ukiangalia aina ya wasanii aliokua anawachagua ni wale wenye vipaji hasa ili akiwa enrol kwny Lebel waweze kuuzika fast.... Check Prof J, Juma Nature, Fid Q, Afande Sele, Mangwair, Feruz, J. Moo, Temba nk nk jamaa alikuwa anakuchukua hafu hulipi ata Mia wewe unarekodi tu bure kabisa hafu mtakatana huko mbele kwa mbele
Kuna kipindi nilimsikia akilalamika kuwa system yake hiyo ndo ilimuumiza mpk akashindwa kuendelea na wkt mwingine akitoa lawama kwa Cosota.
Nadhani hii system ya sasa iko tofauti na ilivyo kwa majani maana naona wasanii wananunua beats tena kwa pesa kubwa tu so wanakuwa na umiliki wa 100% kwny nyimbo yote mf halisi ni Mwana Fa & the Ay kwny ile kesi yao against tigo.