Professor J na Frank Majani wana beef zito

Majani alikua na njaa kali kwahiyo ameponea kwenye hiyo pesa
Majani hajakanusha alichosema Prof. Na Prof hajalalamika, ameweka rekodi sawa nani kapata nini.

Mbona kama Majani anawaka bila msingi?

Au kuna vita zaidi nyuma ya pazia?
 
Kama kikao kilikua ni cha kamati ya bunge haya majibu pia yalipaswa kuishia huko huko kwenye kamati ya bunge, kuyaleta public na ku mtaja mtu moja kwa moja sio sawa Jay kakosea.
Sasa aliyeyaleta nje si huyo dogo Milad Ayo?

Prof J hanaga Noma kabisa na Hana ukalapina au ududu baya!

Tukubali tu P Funk kazingua!
 
Hapa wengi mmemwandama Pfunk,,lakin angalieni uandishi wa Prof J , obvious hiyo hela imemuuma sana...rudieni kusoma hiyo tweet yake
Hiyo hela siamini kama imemuuma Prof J, sana sana angepewa kama 25Mil, wakati kwa mwaka J anaweza kuvuta zaidi ya milion 600....
 
Ok tufanye wewe ndo Prof alafu unaambiwa umevuta 100 sasa unataka kukanusha ungesemaje ili usilete mvutano.
Noma sanaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Hapo ukute kuna wanaokudai...Wife nyumbani utamwambia nini.. wanafamilia hawahaambulia hata miaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119] Yani bora useme ukweli tu
 
Inavyoonyesha Majani alikuwa anasubiri sana hii nafasi aongee alichoongea, maana kiukweli sioni upungufu wowote kwenye andiko la Prof.

Amenikumbusha utani mmoja wa zamani, kwamba Mke na Mume waligombana Mke akaamua kutoka nje na kukaa barazani, Mume akafungulia redio (RTD enzi hizo redio ni moja), ilikuwa muda wa taarifa ya habari...basi Angalieni Mpendu (mtangazaji) akaanza "New york" mama kule nje akalipuka "nyoko mwenyewe limbukeni mkubwa wewe....." huku akirudi ndani kumfuata mzee, yaani vagi likaanza upya.

Kilichoandikwa na alichotafsiri Majani ni maji na mafuta.
 
COSOTA walitaka ujiko kwa mgongo wa Profesa, ndio maana naye amelazimika kukataa hadharani, na ofcourse ina uzito zaidi kwa cosota kumtaja Prof (Mbunge) ukilinganisha na P Funk.

Hata kama Prof ndio kwamba kapatia upenyo wa kutoa la moyoni lakini bado ndio ukweli kwamba hajapokea hizo milioni 100 yeye kama wao cosota walivyorekodi kwenye kumbukumbu zao.
 
producer huwa analipwa chake
so obvious msanii ndio mmiliki maana huwa ananunua beats kwa producer
Sio kwa majani.

Kwenye interview za majani alisema business modal yake ilikuwa tofauti na MJ ambaye yeye huwa anatoza studio time sio kununua beats.

Kutoka kwenye hiyo video dakika ya 8 na kuendelea P FUNK anaelezea hilo.

Yeye alikuwa anafanya kwa mtindo wa label hivyo alikuwa hacharge msanii yeyote pesa na akatoa mfano wa diamond na WCB hivyo beats zote za bongo records ni mali ya bongo records chini ya p funk.

Na hilo ulilongea kuwa msanii akilipa beats ndio umenunua pia sio kweli, Unapoenda studio unalipia unalipia studio session na sio beat Kwa mujibu wa MJ pia mikataba ya COSOTA, beat inaendelea kubaki mali ya prodyuza.

Mfano Windows ni mali ya microsoft pamoja unanunua kwa dolla zaidi ya 200 bado Microsoft wanabaki na haki ya umiliki au nguzo za tanesco.
 
Mleta mada naona nawe kama umekuza mambo, umekosea kuandika vizuri kichwa cha thread...

Anayeonekana mkorofi hapo ni P Funk, maybe kashindwa elewa Kiswahili maana huwa ana kawaida ya kusema Kiswaz si lugha yake ya kwanza...
 
Kwa nini mnailaumu BANGI? Bangi inahusikaje hapa? Hapa alaumiwe P Funky na sio Bangi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…