Professor Jay: Madingi wapunguzwe BASATA, wataua muziki

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506

Mbunge wa Mikumi, Muheshimiwa Joseph Haule au Professor Jay amefunguka na kusema tatizo linalosababisha kufungiwa kwa wasanii na kazi zao mara kwa mara ni kuwepo kwa mrundikano wa watendaji waliopitwa na wakati "madingi" huko BASATA.

Showbiz Xtra: Hivi karibuni pia kulikuwa kuna majibizano kati ya Diamond na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, kama sakata hili ulilifuatilia una maoni gani?

Professor: Sitazungumzia sana kuhusu mvutano wao lakini nitatoa maoni yangu kuhusu kinachosababisha haya yote.

Mimi ninaona tatizo lipo Basata. Wapo watendaji ambao wamepitwa na wakati.
Ndiyo wanaosababisha kazi za wasanii kufungiwa mara kwa mara.
Sasa kuna haja kwenye baraza hilo wawekwe vijana ambao wanafahamu nini kinafanyika katika dunia ya leo, hili litasaidia na hakutakuwepo kwa malalamiko kama hayo ya Diamond.

kwani shonza naye ana miaka mingapi..shonza si 30 tu..aseme tu ni uwezo mdogo wa shonza ndio yalipekelekea yote hayo
 
Tatzo siyo Madingi ila tatzi ni Siasa/watawala na mambo yao ya hovyo...huko mambele mbona wapo Madingi na ndyo wanao-run entertainment industries zote kuanzia kwenye ngumi,music mpaka category ya porn!
 
Napenda hata president awe kwenye miaka ya 40's under 50 na mwenye exposure ya kutoka.maybe kutakuwa na mabadiliko fulani ya nchi. Wanapachikwa uongozi watu wale kwa wale wanatolewa sehemu moja na kuwekwa sehemu nyengine
 
Vijana wanapotea basata simamieni maadili ya wasanii
 
Hao wazee ndio walikuwa wanakata mauno ya kanda bongoman kipindi kile na katitu pia Mshanajr anaijua katitu.
Ila leo wanajifanya wanajua sana maadili wakati ukifuatilia familia zao utakuta wamelala na mahausigelo wao
Wakiwa wamevaa suruali zikiitwa bagi
 
Laweza kuwa ni tatizo pia lakini pia nahisi hawana weledi wala elimu ya kutosha ya sanaa
 
Back
Top Bottom