Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,506
Mbunge wa Mikumi, Muheshimiwa Joseph Haule au Professor Jay amefunguka na kusema tatizo linalosababisha kufungiwa kwa wasanii na kazi zao mara kwa mara ni kuwepo kwa mrundikano wa watendaji waliopitwa na wakati "madingi" huko BASATA.
Showbiz Xtra: Hivi karibuni pia kulikuwa kuna majibizano kati ya Diamond na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, kama sakata hili ulilifuatilia una maoni gani?
Professor: Sitazungumzia sana kuhusu mvutano wao lakini nitatoa maoni yangu kuhusu kinachosababisha haya yote.
Mimi ninaona tatizo lipo Basata. Wapo watendaji ambao wamepitwa na wakati.
Ndiyo wanaosababisha kazi za wasanii kufungiwa mara kwa mara.
Sasa kuna haja kwenye baraza hilo wawekwe vijana ambao wanafahamu nini kinafanyika katika dunia ya leo, hili litasaidia na hakutakuwepo kwa malalamiko kama hayo ya Diamond.