GE2025 Professor Lipumba: Oktoba 29 kura zitahesabiwa kama zilivyopigwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ametoa wito kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuhakikisha kuwa kura za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 zinahesabiwa na kutangazwa kama zilivyopigwa na wananchi.

Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo jana, Oktoba 5, 2025, alipohutubia wakazi wa Mbagala Rangi Tatu, Dar es Salaam, ambapo amesisitiza kuwa usawa na uwazi katika mchakato wa uchaguzi ni msingi muhimu wa kujenga demokrasia ya kweli nchini.

“Sisi tumeamua kushiriki katika uchaguzi huu, pamoja na changamoto zilizopo katika taratibu kwa kuamini kuwa ujenzi wa demokrasia ni mchakato unaochukua muda. Tunaamini kura zitahesabiwa na kutangazwa kama zilivyopigwa,” amesema Profesa Lipumba.

Aidha, ametoa wito kwa vyombo vya dola kuepuka kuingilia masuala ya kisiasa, akisema hatua hiyo itasaidia kulinda amani na kuimarisha imani ya wananchi katika taasisi za kikatiba.

“Vyombo vya dola visijihusishe na siasa, bali viache wanasiasa washindane kwa hoja. Hiyo ndiyo njia sahihi ya kujenga demokrasia ya kweli,” ameongeza.
 
View attachment 3484357

Hakuna muislamu mwenye akili labda awe muislamu jina siyo mbinua kijambio
 
Back
Top Bottom