Programmer na developer wa Tz tunafeli wapi?

Ili kuingia kwenye soko lazima ugharamike na ukubali hasara, pia kuhusu soko si lazima kulenga watanzania tu, lenga Dunia, muhimu utengeneze kitu kinachohitajika kwa nyakati za sasa.
Kuhusu kuwa na wataalamu wengi, ni jambo zuri; kwa sababu usitegemee kitu kizuri ule peke yako.​
 
Developers wenzetu kwa ujumla hawaingii hasara kuanzisha hizi kampuni za gemu/app/software.

Angalia kama NALA kwa mfano, wao wametengeneza wazo lao la biashara wameenda kwa wenye hela (Venture Capitalists) wamewaeleza idea yao, NALA investors wa kwanza walikuwa Y-Combinator (YC) hii "fund" inainvest kwenye maelfu ya kampuni ni kama wanabahatisha kwa kiasi fulani, wanajua asilimia kubwa zitafeli ila kutakuwa na ambazo zitahit sana, so YC wanawapa NALA $150,000 -$500,000 waende wakajaribu hiyo biashara ya kwa makubaliano ya kuchukua 7% ya kampuni.

NALA anaenda anaanzisha hiyo kampuni anatumia hiyo pesa kuajiri watu, kuitangaza kampuni etc, inaonekana kuna mafanikio fulani pamoja ya kwamba hakuna faida mpaka sasa, wanarudi kwa investors yule yule au wengine anapata capital upya anagawa kipande kingine cha kampuni, tunarudia hivyo hivyo wanasonga mbele, mpaka sasa wameshapata capital $50 million hajarisk pesa zake wala kuingia hasara yoye ni hela ya investors ambayo wanatarajia itazaa matunda huko mbeleni.

Sasa fikiria UBER walipata capital ya $22 billion kabla ya kupata faida yoyote kama kampuni.

Kuhusu kutengeneza app ambazo haziwalengi wa TZ ni sawa ila unashindana na kila mtu hapo, wewe hauna capital mwenzako ana mamilioni ni kazi ngumu sana. Kuhusu watu wengi tatizo sio kula peke yako tatizo wewe utawalipa vipi hao watu wakati unaanza?

Tatizo ni hela, matatizo mengine yote yanatatulika kama hela ungekuwa unayo hata developers kama bongo hakuna siku hizi ni simple kuajiri watu remote kama hela unayo.
 
💯💯💯💯💯💯
 
Uko sahihi, bila mtaji ni changamoto. Kama wewe ni developer na hauna mtaji anza hivi:-​
  • Andika wazo lako ata kurasa tano​
  • Tengeneza business plan​
  • Tegeneza App/website​
Andika proposal ya kuomba fedha kwenye makampuni

Lazima uwaonyeshe wenye pesa kuwa unajua kitu fulani, na wanakiona ili washawishike kutoa pesa.

 
Nitumie link ya hiyo app
 
Mimi ni self-taught developer mwenye experience ya zaidi ya miaka 7. Mimi ntakujibu kwa kupitia changamoto ambazo nimekutana nazo.
  1. Nahisi kuna changamoto kwenye mitahala ya elimu kwa ujumla, Watu wengi sana ambao wanasoma programming kama professional ni vitu ambavyo wamevijulia chuo. Na programming ili usuke vitu vya kuogopesha unatakiwa kuijua mapema. Hii kitu ni kama lugha, ndio maana zinaitwa lugha pia, Mfano ni rahisi sana kutofautisha mtu aliyejua kiswahili akiwa na miaka 2 na yule aliyejifunza ukubwani.
  2. Uwezeshwaji aisee. Unaweza ukawa na wazo na ukatengeneza system yako safi. Lakini kuiweka hiyo system hewani inahitaji pesa, Na watu wengi sana wenye pesa bongo sio rahisi kuwekeza pesa kwenye vitu vya kidijitali. Sasa muda mwingine wazo lako linakufa kisa tu umeshindwa kulipia bill ya AWS.
  3. Mapato. App nyingi sana zinahitaji kutengeneza pesa ili ziishi, Jiulize wewe binafsi ni mara ngapi umelipia kitu kupitia app ya Mtanzania. Diamond alianzisha website ya wasafi kuuza mziki lakini ilikufa maana watanzania wanataka kupakua miziki bure kwa bekaboy. Lakini hapa kama watu wangekuwa wako radhi kulipia bidhaa na vitu kadharika mambo yangeenda safi.
  4. Sheria na Taratibu. Sheria za marekekani kuhusiana na kampuni za teknolojia ziko vizuri sana na zinaruhusu watu kuanza bila kutumia pesa nyingi. Mimi nilijaribu kusajili kampuni yangu ya teknolojia (kosa ambalo najuta hadi leo) Maana nilitumia pesa nyingi sana na bado app yangu haikuvutia watu wengi. Kwa nini nimeandika hichi? Sababu app yangu ilikuwa ya kuuza vitu vya kidijitali. Ukienda kwenye makampuni ya simu ili upate API baadhi wanataka uwe umesajiliwa kama kampuni, na kusajili kampuni kwa TZ ni pesa, mambo ya kodi sijui mara hili mara lile yani ni mlolongo mrefu kwa kweli.
  5. Programmers kuandaa vitu vitakavyofeli. Kiuhalisia startup nyingi sana zinafeli. Uthubutu wa watanzania uenda unaogopa hili.
  6. Watanzania wengi hawaamini kazi za watanzania wenzao. Kampuni iko radhi ilipe watu kutoka nje wasuke mfumo na sio wabongo au mtu yuko radhi atumie mfumo wa wazungu na sio wa wabongo.
  7. Support, Mara nyingi sana watanzania wanaamini nje ndio wanatengeneza app nzuri zaidi ya watanzania wenzao. Kwenye app development kuna kitu kinaitwa MVP. Ukiona MVP ya facebook ni tofauti sana na ilivyo sasa. Kwa nini naongelea support, sometimes unatakiwa tu kudownload app ya mtanzania mwenzako hata kama unaona ni mbovu na umpe feedback yako.
  8. Muda. Kutengeneza vitu kama games ni kitu ambacho kinataka muda mno. Kwa mtanzania wa kawaida anayewaza apate wapi hela ya kula hawezi kufanya hichi kitu. Hapa unahitaji watu ambao labda uwape idea waikubali wawe wanakulipa hela ya kula ujikite kwenye game tu, Hii sio rahisi.
  9. Elimu pia. Mimi binafsi nimeanza kutumia computer toka nikiwa shule ya msingi bahati mbaya sikusoma mambo ya computer chuo kikuu lakini watu wengi sana wenye degree za computer science niliokutana nao ni watu wasio na passion na computer, kama mimi jinsi nisivyo na passion na degree niliyosoma. Programming ukifanya kama hobby ni rahisi sana kutengeneza vitu vikubwa maana utafanya tu hata kama ulipwi hata sh mia, Lakini kama ni kitu hupendi sizani inakuwa changamoto.

Mwisho nataka kusema kuna app nzuri tu za watanzania zinafanya vizuri tafuta app kama Nilipe, Dawa Mkononi, Nala (Maybe) na nyingine nyingi ni kwamba tu uenda wewe ulilenga app za social interaction kama jamiiforum kitu ambacho sio Tanzania tu hata nchi nyingine wamefeli kutengeneza big social networks kama instagram, facebook.
 
Onyrsha mfano huo mkuu... tayari umeona gap na nakupongeza kwa hilo sasa njoo na solution.
 
Vijana unaowazungumza angalia ¾ ya post hapa jf ndio uta determine future generations yao..

Kila kipo kipo pale kinamsubiri mtu yeyote kuwa tayari kukipata.
 
Huenda kizazi cha sasa ndio kizazi kikawa kizembe kuwahi kutoka toka kuumbwa ulimwengu. Vijana wa sasa hawana maarifa lakini wana elimu

Angalia histori za watu wa zamani wana maarifa makubwa lakini hawana elimu..

Ujio wa AI ndio utachangia ongezeko la uwezo wa watu kifikiri na kifanya mambo yao, kwakumsukumia majukumu AI ayafanyie kazi
 
Support gani? App inajisapoti yenyewe kwa kuwa ya kiwango cha juu na ubunifu. Hujui chema chauza na kibaya chajitembeza? Unataka watu wanunua app za vilaza zisizo na ubora?
 

Naona unachanganya AAA games, indie na mobile games kama flappy bird. Hakuna indie developer anaweza kutengeneza game kama RDR2 ambayo budget yake ni usd 500,000,000 hiyo ni Trillion ya kitanzania na ushehe. You can't compete with giants kama RockStar, not even the giants themselves. Mfano Trailer ya GTA 6 ilipata 100 million views youtube in a day, leo ina 200 million views.

Unlike AAA games, yoyote mwenye computer na akili anaweza kutengeneza PC au Mobile game bure. Wanaitwa indie developers. Hivyo budget sio sababu.

Mobile Game haziuzwi mkuu, ni bure, unless uuze mwenyewe, na ukifanya hivyo utakuwa mjinga sababu hakuna mtu ananunua mobile games. Na sio kweli kwamba kila successfully PC game au mobile game zipo chini ya giant companies with over a 100 workers. Mfano kwa mobile games, ukiingia playstore leo utakuta most games zimetengenezwa na indie developers, eidha ni solo developers mpaka 2 to 5 people na mostly utakuta zina downloads sio chini ya 100,000 to 1,000,000. Kwa mfano Among Us yenye over 500 million downloads playstore. Lile game limetengenezwa na watu 3 tu. Mwanzo lilikuwa between 10,000 downloads kama vigemu vingine vya ajabu ajabu, until Corona lock down ndipo lika blow up. Naweza kutengeneza Among Us clone in less than a week.

Alafu kusema "kwa bongo hiyo kitu haina hela." Ni nonsensical. Sababu once application ipo Playstore tayari ni available worldwide, that's a world wide market. Kinachobaki ku-determine mafanikio ya application yako ni niche, quality na marketing. Vitu pekee vitakavyokufanya ustand out lasivyo utakuwa buried chini ya mamilion ya other applications.

Kuna major factors nyingine zinazofanya kusiwe na big companies za Games au applications Tanzania. Lakini sio market, faida wala budget.

Just in case, I'm an application/game developer.
 
Kareem Design anakuja na game kali litaitwa BUS SIMULATOR TANZANIA
Muangslie Instagram kuona Project zake
Seriously? I'm not down playing the guy lakini how uta standout na bus simulator playstore? Sehemu ambayo imejaa mamilion ya kitu hichohicho?
 
Umasikini.
Exposure.
Creativity na Ideas.
Low Quality products.
Market.

Sababu ya kwanza inayofanya Tanzania tusiwe na advanced au successfully software products au companies ni lack of exposure ya kidunia kwa wananchi kiujumla, lakini hasa vijana. Watanzania wana exposure ndogo sana juu ya maendeleo ya kidunia, ikiwemo technology au hata movie production. Na njia pekee mtu anaweza kufanya vitu exceptional ni eidha awe na inborn curiosity na natural creativity. Au ajifunze kutoka kwa wengine. Hiyo ndio sababu exposure ni muhimu sana.

Lack of exposure inapelekea kukosa ubunifu au creativity kwa kiswahili, na advanced ideas. Hence unapata mediocre na low quality products ambazo hakuna mtu anahitaji, hivyo lazima ukose market dunia nzima. Sababu wenzako wako beyond hiyo level. Ili u-successed ni lazima u-adapt viwango vya dunia.

Na kukua kutoka hapo ni long process. Mfano mzuri ni angalia entertainment industry ya Tanzania inavyozalisha movies mbovu za ajabu ajabu zinazojirudia kila siku. Zero creativity. Wakati wenzetu wanatengeneza Sci fi, fantasty, horror na genres nyingine nyingi. Unaangalia movie kama Inception by the legendary Christopher Nolan unabaki mdomo wazi, unajiuliza huyu mtu alikuwa anafikiria nini? It's an insane level of creativity and imagination. Njia pekee ya director wa kitanzania kuja na idea na product kama au zaidi ya Inception ni kujifunza kutoka kwa mtu kama huyo. Nimetoa mfano wa Movie sababu sijawahi kuona video games kutoka Tanzania, let alone a successful one.

Ukitaka kujua umuhimu wa exposure angalia nchi Advanced za Asia. Tunasema wachina wanacopy alafu tunawacheka kitu ambacho ni ujinga. Sababu ili kukua rapidly kutoka level moja kwenda waliyoko wenzako ni kujifunza kutoka kwao au... Ku-copy na ku-paste. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuadvance zaidi. There's no shame on that except to a few conservative idiots.

Kuna Game inaitwa Black Myth Wukong, limetengenezwa na wachina. Limeuza 10 million copies in its first 3 days. Ni game lilobase on Chinese myths na limeuza vizuri dunia nzima. Why? Sababu ni product inayokidhi vigezo vya quality worldwide. Exposure always leads to advanced creativity, au advanced thinking. It's why watoto wanaenda shule.

Kukosa Exposure pia kunapelekea kukosa soko la ndani. Ni asilimia chache sana ya Watanzania na Waafrika wanatumia software products regularly. Na ukilinganisha products za ndani ni mbovu, unaishia kukosa soko ndani na nje.

Umasikini ni factor kuu inayosababisha wananchi kukosa exposure, kitu kizuri exposure ni effective fundamentally, haujitaji utajiri kuwa creative au kujifunza.
 
I am also a developer, tatizo namba 1 ni hela nakuhakikishia hilo, ninafanya kazi startup ina miaka kadhaa hela wanayotumia kuendesha kwa server cost tu inatia kizunguzungu na ni kampuni ndogo kwa tech ambayo hakuna aliyewahi kuisikia.

Angalia hata US baada ya interest rate kuongezwa na serekali pesa ya investment ikawa ngumu kupatikana tech market ilivyoshuka hasa kwa kampuni za startup ambao wanategemea VC funding.

Unasema quality na marketing kama vile ni bure, quality inatokana na watu wenye uwezo na experience ambao wako well paid, marketing ni gharama kila kona ili kupata instals zinazotabirika lazima utumie hela tena sio ndogo kama nilivyoeleza before.
Tena siku hizi market imeshakomaa sio kama siku za mwanzo wa app stores hakuna organic downloads lazima uipush app kwa kulipia ads.

Ni kweli kuna indie devs wanaohit ndo maana nikataja flappy, mobile game labda nyingi "haziuzwi" lakini zinatumia kila aina ya monetization kama in app purchase ambazo ni yale yale bado mtu inabidi atoe pesa yake.

Vast majority ya indie devs hawatengenezi pesa, hatuwezi kuchagua a few lottery winners tukasema kucheza lottery inawezekana kupata ushindi. Gemu kama Among Us ni phenomena inayotokea almost randomy na mara chache sana hauwezi kuplan biashara kwa kusema ninaweza nikahit kwa vile watu wako lockdown.

"Kuna factor zengine" hebu tutajie hizo factor basi!
 
Mimi pia napenda kweli kujifunza haya maswala ya programu, na hata kuja kutengeneza app itakayofanya vizuri hapo baadaye. Inabidi uje na uzi humu walau nijifunze kitu miaka 7 sio mchezo, najua ulipitia mengi fanya hivyo bro maana wengine elimu zetu ni form 4, walau naweza nikapata kitu kikanisaidia katika safari yangu ya kuja kuwa programmer
 
Nimezaliwa BUHIGWE Kigoma.
Nursery: No
Primary: Buhigwe P/s
O'Level : Buhigwe S/School
A' Level : Kibondo

Huko kote, computer nilikuwa naiona stationery tu..
At the age of 20+ najiunga na chuo, nachukua kozi ya Computer science.
Rasmi ndiyo naanza, kushika computer..ghafla naanza masomo.

Sielewi ila uwezo wa kukariri ninao.
Assignment natuamia AI, majibu yote napata.
Namaliza chuo, najua Kubadilisha Windows na ku install Ant virus kwa usahihi ila vingine hadi niende youtube ila bado nafeli, nilipo ajiriwa kazi za maana wanaletwa wahindi kuzufanya sisi tunapewa kusimamia tu.

Ila huko majuu...mtoto wa maima 10 ni programmer mzuri sana, unakuta ana fahamu lugha zote muhimu ( Java, python, C++ and n.k).

Bongo jitu linafika umri wa 20 lakini hajui kama kuna python anakuja kufahamu vitu muhimu ubongo ukiwa umeanza kulemewa na mapenzi, stress za maisha na bado naanza kukesha na pS bila ratiba maalum.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…