1. Jifunze kwanza
Fundamental za Computer Programming kama umetokea kwenye Non-CS background anza na Python kama introductory language
Kwa kua unaenda mdogo mdogo huna haja ya haraka,
Pata misingi kwanza ya Computer Science / Programming kupitia Python
Sababu:
i.Utajua nini maana ya Programming, Jinsi gani Computer ina chakata( excute) Programs, etc..
ii.Itakupa Confidence na kufanya uamini uwezo wako, kwa sababu ukishakua vizuri kwenye language moja hata kama utatumia one year kuifahamu Language (Python) unaweza kujifunza language yoyote baada ya hapo ndani ya mda mfupi hata (hata wiki kadhaa) kwa sababu concept ni zilezile tu, hizi wiki utatumia kuwa Familiar na Syntax na hio language mpya
Usianze kujifunza Programming na languages kama Javascript au PHP (Maoni yangu tu) nitatoa sababu chini
iii.Python ni language nyepesi kueleweka (intuitive) na ina nguvu,
Tunaita General Purpose language, yaani lugha inayoweza kutumika kutengeneza aina yoyote ile ya Program/Software
Languages kama Javascript na PHP ni muhimu haswa kwenye Web Development lakini hazifai kujifunzia programming kwa mara ya kwanza, zitakuchanganya haswa kama unajifunza bila mentor
Baada ya ku master fundamentals za Computer Programming Then Njoo sasa ujifunze
2.HTML
HTML ni simple 'mark up' language inayotumika kutengeneza webpage
Ni rahisi haifai hata kuwekwa kwenye CV yako
Hii itakuchukua Wiki kuisoma, kama ukiisoma kila siku
Then ukimalizana na HTML
3.Jifunze pacha wake CSS
Kazi ya HTML ni kutengeneza webpage (ambayo kimsingi ni document tu) na ku display data zinazohitajika kwenye hio page
But utahitaji ku design page yako katika namna ya kupendeza, hakuna user atakaye taka webpage yenye design mbovu
So utatumia CSS kupendezesha (style) webpage yako
Hii ni complicated kidogo kuliko HTML, kuwa complicated haina maana kuwa ni ngumu, no ila ina vitu vingi vya kuzingatia
Ila usihofu kwasababu huna haja ya kukalili chochote
Kwa sababu, wewe si wale wanaosoma kwa ajiri ya course works
Jifunze tu fundamentals za CSS kabla hujaamia kwenye
4. CSS Framework
Ukiwa unajifunza CSS itakulazimu kuandika codes zako wewe mwenyewe
Ila baada ya kuelewa kazi na misingi ya CSS ni mda sasa wa kujutua mzigo na kujifunza CSS Framework
Framework ni kama mkusanyiko wa codes,katika case yetu 'Codes za CSS' ambazo zimeandikwa na developers wazoefu kuliko wewe, wewe unachofanya ni kuzitumia kwenye kila project yako
Hii itakufanya uwe productive zaidi kuliko kuandika codes za CSS from the scratch kwa kila project
Kujifunza na kutumia codes za developers wengine ndio siri ya kujua na kuwa productive kwenye programming,
5.Baada ya hapo jifunze basics za Internet na WWW.
Hapa jifunze kuhusu Client Server Architecture
(Client ni computer inayo omba webpage yako, na Server ni computer inayo sikiliza ombi la client na kutuma webpage iliyoombwa)
(Client anapo omba webpage yako anatuma GET request, anapotaka kutuma data kwenye website yako anatuma POST request ikiwa na data alizohitaji, etc...)
6.Baada ya hapo jifunze SQL
Hii inajulikana kama 'Structured Query Language '
Website yoyote ile inayoruhusu watumiaji kutengeneza data zao (ku upload video, photos,chats etc) zinahifadhi hizo data zote kwenye special program inayojulikana kama database
So SQL ni language inayotumika kuzungumza na hio database
Kwa ufupi, SQL ndio language inayozungumza na database ya aina yoyote ile duniani, yet ni rahisi sana
Ukiwa unajifunza SQL utajifunza pia kitu kinachoitwa Database Management System(DBS),
Newbie wengi wanachanganya kati ya DBS na database
Usi fall kwenye hio trap
Ukijifunza SQL pia utajifunza ku interact na DBS yoyote itakayo kuwa kwenye Application yako, anza na hii moja inaitwa MYSQL
7.Mpaka kufika hapa, hakuna tena kitakacho kuzuia,
Hapa ni mda wa kuchagua silaha ipi utaitumia kwenye Web Programming
Na hapa ndipo confusion zinapoanza
Mpaka sasa utakua unaifahamu Python kwa uzuri, kama nilivyokwambia Python ni general purpose, inaweza tumika vizuri ku program web application
Ila nilikwambia kuwa kuna Framework kwenye CSS, vile vile kuna language zina Framework Ikiwemo Python
Popular web framework ya Python ni Django
Kumbuka Framework zipo kukurahisishia kazi, so usihizi una mzigo tena wa kujifunza
Mimi situmii Python kwenye web natumia PHP, kwa sababu nilianza kujifunza PHP kabla ya Python, wewe tumia Python kwa sababu umeanza na Python
8.Mwisho maliza na Javascript kwasababu hii ni defacto language ya web bila kusahau Javascript framework kama Reactjs na Vue, mpaka kufika hapa utakua na utashi wa kuamua ipi tool ujifunze
9.Kisha kifunze kuhusu Git na Github
10. Design pattern & Architecture
11.(Extra) Machine learning na A.I
Web app zinazotengeneza pesa nyingi duniani hazikosi hii kitu
Na hapa utakuja kunishukuru kwanini nilikwambia uanze na Python