SoC04 Programu ya Ujenzi wa Miji Salama ngazi ya Kata: Adhima kuboresha Makazi katika Mitaa na Vijiji

SoC04 Programu ya Ujenzi wa Miji Salama ngazi ya Kata: Adhima kuboresha Makazi katika Mitaa na Vijiji

Tanzania Tuitakayo competition threads

Jerry Farms

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
202
Reaction score
167
UTANGULIZI
Kufuatia ukuaji wa miji, changamoto mbalimbali zimekua zikishuhudiwa siku baada ya siku. Changamoto mojawapo ikihusisha ukosefu wa usalama katika makazi.

Kidunia suala la ukuaji wa miji salama limeangaziwa katika nyanja mbalimbali chini ya shirika la Makazi( UN-Habitat). Kwa mujibu wa ripoti toka UN-Habitat takribani 60% ya wakazi katika nnchi zinazoendelea wamekumbana na adha ya uhalifu katika jamii zao, 70% ya wakazi wa Latini Amerika na Afrika wakiwa ni waathirika,(hhtps://unhabitat.org>programme).

Kufuatia hali hio programu ya miji salama zimeanzishwa katika majiji na miji 77 katika nnchi 24. Utekelezaji wa programu hii ukiwa umegawanyika katika awamu tatu.

Awamu ya kwanza
•Mazingira
•Uthibiti uhalifu kwa makundi maalumu(watoto,wasichana na wanawake).
•Uongozi ngazi ya chini( mamlaka ya serikali za mitaa).

Awamu ya pili
•Umiliki ardhi na udhibiti wa maafa na majanga ya asili

Awamu ya tatu
•Mipango, usimamizi na uongozi
Msisitizo ukiwa umewekwa katika uongozi imara kusimamia usalama wa maeneo na uthibiti wa maeneo ya umma na mitaa.

Katika andiko hili nitajikita zaidi kuzungumzia usalama wa makazi na wakazi katika ngazi ya kata/shehia.

Changamoto ya makazi yasiyo salama katika Kata/shehia.
Katika kata mbalimbali nnchini changamoto ya usalama hafifu katika mitaa na vijiji ni suala mtambuka. Visa vya mlipuko wa magonjwa,maafa, uhalifu, uwepo wa makundi ya kuhalifu mfano "watoto wa mmbwa" -Mwanza, "Panya Road"-Dar es Salaam, "Teleza"-Kagera na "Wadudu"-Arusha, ukatili wa kijinsia, wizi, ubakaji na mengineyo mfano wa haya.

Visa vingi vimekua vikiripotiwa kutokea usiku na kwa uchache mchana katika maeneo ya vijiji na mitaa. Matukio haya kwa kiasi kikubwa yamechagizwa na mmomonyoko wa maadili katika jamii, uendelezwaji holela wa maeneo, miundombinu isiyorafiki maeneo ya umma na ushirikikishwaji hafifu wa umma katika maamuzi.

Athari za matukio ya uvunjwaji wa hali ya usalama katika makazi.
•Upotevu wa amani kwa wakazi katika eneo husika hivyo maendeleo hafifu kwa wakazi.
•Kukwamisha shughuli za maendeleo na uwekezaji katika eneo kutokana na hofu.
•Kutweza utu wa waathiriwa, vifo,vilema na mengineyo.
•Mdororo wa uchumi kwa wanajamii na wakazi wa maeneo.
Kufuatia madhira hayo hapo juu, serikali kwa kushirikiana na jamii na wadau wengine wa maendeleo haina budi kuja na mpango wa programu za maendeleo ya miji salama katika kata/ shehia.

Programu ya ujenzi wa miji salama katika kata/shehia kuboresha makazi
Hii ni programu maalumu itakayoratibu shughuli zote za maendeleo katika eneo husika. Serikali kuu kwa kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa haina budi kukumbatia programu hii ili kufanikisha adhima ya makazi bora na salama kwa watu wake.

Hatua kuelekea makazi salama
Kuhakikisha ubora wa makazi na usalama wa makazi mambo yafuatayo hayana budi kufanywa kupitia programu.

•Maboresho kwa vitengo vya maendeleo ya jamii na polisi kata katika kata husika. Maboresho yahusishe; nyenzo za kuwawezesha watendaji katika ofisi, kuongeza idadi ya watumishi karika idara husika na mafunzo ya mara kwa mara kuendana na kasi ya mabadiriko ya sayansi na teknolojia.

•Uanzishwaji wa vitengo vya wataalamu wa Sheria na Ardhi ngazi ya kata.
Hawa watashirikiana na wajumbe wa mabaraza ya ardhi ngazi ya kata kusimamia, kuratibu shughuli za maendeleo na kutasfiri sheria kwa umma katika kata husika.

Utekelezaji wa programu ya makazi salama katika mitaa na vijiji
Baada ya maboresho hayo madogo kufanyika katika kata/shehia mambo yafuatayo kwa kufuata utaratibu ulioamuliwa na ofisi ya kata/shehia yatafanyika:

•Kufanya utafiti kutambua viashiria vyote vya uvunjifu wa usalama katika eneo.
  • Maeneo hatarishi yote katika kata/shehia yatambuliwe.
  • Umma ushirikishwe kutambua vihatarishi katika maeneo yao.
•Tathimini ifanyike baada ya kukusanya visa vyote vya uhalifu na vitu vinavyohatarisha usalama katika makazi. •Ripoti maalumu ya mtaa/kijiji iandaliwe kutoa maelezo ya hali ya usalama katika eneo.
•Maeneo yenye uhitaji wa mpango wa dharula yaainishwe katika kata/shehia kwa ajili ya kuandaliwa mpango kazi kurekebisha hali.
•Mpango kazi na utaratibu wa uendelezwaji salama wa maeneo uandaliwe. Bajeti katika halmashauri kuwezesha zoezi zitengwe kwa kuzingatia mahitaji ya kata.
•Ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo ili kutambua viashiria vya vitendo vinavyochochea mmomonyoko wa usalama katika eneo.
•Uratibu wa mfumo wa upashanaji habari katika kata, mtiririko mzuri wa taarifa toka familia-mjumbe/balozi-mwenyekiti hadi kata uundwe.

Utekelezaji wa programu ya makazi salama katika mitaa na vijiji
Ili kufikia lengo kuu la makazi salama katika kata/shehia mambo yafuatayo hayana budi kufanyiwa maboresho.

Maboresho katika maeneo ya vitovu vya biashara katika mitaa na vijiji.
-Ufungwaji wa taa za barabarani kuzunguka maeneo ya kibiashara(masoko na maeneo yenye maduka mengi mtaani/kijijini).

-Maboresho ya mifumo ya ulinzi katika maeneo ya biashara ikihusisha uwekaji wa kamera za ulinzi kuratibu usalama.

Uanzishwaji wa vituo vya polisi katika kila kata
Polisi kata kwa kushirikiana na mgambo hawatoshi peke yao kutoa huduma za ulinzi katika maeneo ya kata nzima.

Uimalishaji wa ulinzi katika maeneo ya umma yasiyokaliwa na watu.
Maeneo ya makaburi,maeneo ya kukusanyia taka na maeneo ya wazi yamegeuka kuwa vituo vya uhalifu katika maeneo mengi. Jitihada za ulinzi ikiwemo uwekaji taa, ujenzi wa uzio na ulinzi havina budi kuanzishwa katika maeneo haya.

Maboresho miundombinu ya barabara katika mitaa na vijiji.
Kuweka utaratibu wa uwekaji wa vidhibiti mwendo kwa barabara ndefu ndani ya mitaa na vijiji. Kila baada ya mita 100 pawekwe matuta kuzuia mwendo kasi na ajari katika makazi. Uwekaji wa matuta unaofanywa na wananchi wa maeneo husika si salama kwa watumiaji wa barabara. Vidhibiti mwendo huwekwa na wananchi pasipo kufuata vipimo maalumu na kuweka alama za tahadhari hivyo kugeuka kuwa hatarishi kwa watumiaji wa barabara.

Mamlaka za ujenzi hazina budi kuweka vidhibiti mwendo hivi maana wao ndio wataalamu wa miundombinu ya barabara na si wananchi.

Picha ya Tuta lililowekwa na wananchi barabarani pasipo vipimo na alama ya tahadhari.

IMG_20240608_152904_1.jpg
Chanzo: Mwandishi wa andiko
Ushirikishwaji na ushiriki wa wanajamii katika mitaa na vijiji
Sheria zitungwe kuwasimamia/kuwataka wananchi wote kushiriki katika shughuli mbali mbali katika maeneo yao(nzengo). Sheria hizi zitaratibu ;utambulisho wa wakazi( usajiri wa wakazi ngazi ya mwenyekiti wa eneo), kutoa mwongozo wa taratibu za kufuatwa katika kuchangia gharama amuliwa katika shughuli za maendeleo na taratibu nyingine za kushirikiana na jamii.
Maboresho katika muongozo wa utolewaji wa vibari vya ujenzi
Muongozo wa sasa sura ya 4 kipengere 4.3(Utoaji wa cheti cha Kutumia jengo). Msisitizo umewekwa katika majengo makubwa na ya ghorofa,(Mwongozo wa utoaji wa vibari vya ujenzi na usimamizi wa ujenzi wa majengo kwenye mamlaka ya serikali za mitaa 2018). Hali hii imeachia wigo wa matumizi ya majengo madogo yasiyokuwa yamekidhi vigezo kama ilivyo chambuliwa hapa chini.
-Muongozo hautoi maelezo ni kwa muda gani mjenzi wa nyumba ya kawaida afanye ujenzi na hatua zipi achukue pindi atakapositisha ujenzi wa jengo.
-Muongozo upo kimya juu ya majengo yasiyoendelezwa kwa muda mrefu hivyo kugeuka makazi ya vibaka na vikundi vya kiharifu katika mitaa na vijiji.
-Baadhi ya majengo yaliyotelekezwa kutofunikwa makaro ya vyoo kwa muda mrefu hivyo kuhatarisha usalama katika mitaa.
-Baadhi ya majengo kutokuwa na taa za nnje hivyo giza nyakati za usiku na kuunda maficho ya wezi na vibaka.
Picha ya mtaa wenye makazi yasiyo na taa za nnje kwa usalama wakati wa usiku.
IMG_20240608_193538.jpg
Chanzo: Mwandishi wa andiko
Maboresho pendekezwa
-Muongozo utoe maelekezo juu ya ulinzi kwa majengo yasiyokamilika ujenzi kwa muda mrefu( wajibu wa mmiliki wa jengo husika uainishwe).
-Ukaguzi wa majengo ya kawaida ufanyike kabla ya kuanza matumizi( ukaguzi usiishie katika majengo makubwa na ghorofa pekee). Hapa pawekwe vigezo vya msingi ambavyo jengo hata kama halijakamilika basi viwe vimefikiwa ili kuruhusu matumizi huku taratibu zingine za ukamilishaji wa ujenzi zikiendelea.
Kuandaa taratibu maalumu kushughulika na majengo yaliyotelekezwa/maghofu katika mitaa na vijiji.
Uwepo wa majengo haya si afya kwa usalama wa jamii inayoyazinguka kwani mengi ya majengo haya yamegeuka kuwa makazi ya wezi na vibaka. Taratibu maalumu hazina budi kuanzishwa kushughulikia maeneo haya( ubomoaji wa majengo ya zaidi ya miaka 10 ama ulinzi wa maeneo( mmiliki wa jengo awajibike) na njia zinginezo zitakazo amuliwa katika mtaa/kijiji.
Picha: Jengo lililotelekezwa kwa muda mrefu katika makazi.
IMG_20240608_075943_1.jpg
Chanzo: Mwandishi wa andiko.​

Upangaji na upimaji wa maeneo
Upangaji na upimaji wa matumizi bora ya ardhi kuzunguka eneo la kimvuto katika makazi. Mazoezi haya yaamuliwe na vichocheo vya makazi katika eneo na kizingatia kasi ya ukuaji wa eneo. Vitengo vya usimamizi wa ardhi ngazi ya kata vianzishwe na vishirikiane na mabaraza ya ardhi kata na ofisi ya mtendaji kuratibu shughuli zote za maendeleo katika kata/shehia.
Faida ya Programu ya makazi salama katika kata/shehia chini ya mwamvuli wa ujenzi wa miji salama.
•Kuleta amani na usalama kwa wakazi katika maeneo.
•Kuzuia hatari ya milipuko ya magonjwa na athari zinginezo za majanga ya asili.
•Kujenga hali ya umiliki na uwajibikaji kwa wakazi wa maeneo husika.
HITIMISHO
Makazi salama ni moja wapo ya ngazi muhimu ya maendeleo katika taifa. Uendelezwaji wa maeneo kwa kuzingatia usalama huleta mwamko chanya wa maendeleo katika eneo lolote.
Usalama wa makazi hauna budi kuzingatiwa katika maeneo yetu ili kufikia maendeleo enderevu.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom