Progressive People's Party of Tanzania

Nne, Chama cha PPPT
Tano, PPPT
Hapa ni chama cha siasa
Hapa ni kampuni ya biashara,PPTL stands for what? mkuu "Progressive Party Tanzania Limited" au?.


Ila ninakupa pongezi kwa kuwa na uwezo wa kumerge mawazo ya Corporate(biashara) kwenye siasa. Hii inaweza kuwa inaashiria kuwa kichwani mwa kila mtu kuna "profit motive" japo ukiiweka katika kuwasaidia wananchi inaweza kuleta maana
 

Sikonge,

Niliposema chama Changu hakina mana kuwa nakimiliki au ni changu pekee. Ni changu kwa maana ya mapenzi yangu, sawa na vile Yanga yangu na Nyerere Wangu.

Nilipoandika hapo nilikuwa pekee, wamejiunga Steve D, Omutwale, Fair Player, hata Kasheshe anaegemea kujitolea na Mkandara anania thabiti kujiunga.

Sasa ukisoma majibu yangu ya baadaye, ndio maana nikasema Steve D atapewa kadi Nambari Wani, na mimi ya kwangu itakuwa nambari elfu moja. Aidha nimeainisha kwa kutamka chama chetu huko mbele.

Kuhusu maadili au ni nani awe mwanachama, tutaangalia kwa undani kuwa ni mtu wa namna gani anayekuja jiunga na chama chetu.

Badala ya kukurupuka kutoa kadi na kujitangaza eti tumepata kadi 20 kutoka CHADEMA, 50 kutoka CCM au 100 kutoka CUF na TLP, sisi wote wanaotaka kuwa wanachama watawasilisha maombi yao, watafanyiwa usaili ili kujua ni watu wa namna gani kwa kupima kama wanaamini itikadi na nia ya chama, kama kweli ni Wazalendo wenye nia ya kufanikisha malengo ya Chama ambayo ni kumtumikia Mwananchi na zaidi ni kuwajua kiunagaubaga chimbuko la msisimko wao wa kuvutiwa na kujiunga na PPPT.

Zaidi, tuwaweka mizani na usaili wa kujua mwanzo wa maato si ya Chama pekee, bali hata ya Wanachama wetu kwa kuhakikisha kwa kutumia vitendo kuwa Watakaochaguliwa kuwa viongozi, wanaweka wazi maisha yao, kuanzia ajira, mapato, mali, mahusiano ya jamii na kila kitu ili tuondokane na ugonjwa ambao umevishika vyama vingine.

Nia si kukata kuwa na Wanachama au kuwa na njozi za Utopia za kuwa na watu TIMILIFU wasio na kasoro, bali nia ni kupunguza shida za huko mbeleni na makosa yaliyofanywa na vyama vingine ambavyo vilikimbilia kukumbatia Wanachama ambao walikuwa wanajiunga ndani ya vyama hivyo kwa utashi na masuala ya ubinafsi na si kwa manufaa ya Watanzania na kulijenga Taifa.

Watakao ingia chamani watapigwa msasa ili waishi kwa mfano katika mitaa yao, na watakapoanza kwenda sambaza habari kwa wananchi kuhusu chama, itawapasa wajue misingi halisi ya chama na kukielewa kinagaubaga.

Kama vile watu wanavyopelekwa Madras au Mafundisho ya Kipaimara au hata kubattizwa, ndivyo sisi tutakavyoanza kujijenga kwa kuhakikisha kuwa anayejiunga, hafanyi kwa ajili ya ushabiki tuu, bali ana amini kile kinachosemwa na chama na yu tayari kusaidiana na Wanachama wenzake kuijenga upya Tanzania.

Lengo si kuchuja wanaotaka kuwa wanachama, bali ni kuwa na wanachama ambao watajua fika kuwa wajibu wao mkuu ni kumtumikia Mtanzania kwa Manufaa ya Tanzania kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Katiba ya Tanzania.
 
Rev.Kishoka,

..nimevutiwa na majibu uliyompatia Mkandara, haswa kuhusu suala la elimu.
 
Rev. Kishoka,
Nilipoandika hapo nilikuwa pekee, wamejiunga Steve D, Omutwale, Fair Player, hata Kasheshe anaegemea kujitolea na Mkandara anania thabiti kujiunga.
Mkuu wangu mimi sasa hivi nachofikiria ni kupata UONGOZI BORA, individuals badala ya chama kipya. Kwanza kinachotangulia sasa hivi ni kuchukua bunge na hata IKULU kama kuna uwezekano na kusimamisha Uongozi bora ambao utamaliza Ufisadi uliopo..
Tatizo la siasa nchini sio vyama ila ni watu, tusipokuwa na watu imara haijalishi tutaunda vyama vingapi.Nachowaomba sana wakuu zangu kwa mwaka huu wa 2010 jiungeni na chama kimoja kwa PAMOJA kisha mkiandae kuchukua bunge mwaka huu 2010. Kisha baada ya hapo ndipo mtaanza kutazama maswala ya vyama na mrengo..

Ni mawazo yangu tu hayana maana mbaya!
 

Hofstede,

Nia ya kuwa na Serikali au kuwa na mfumo wa kiutawala siku zote ni kuhakikisha kuwa nchi inaamka na kujiendesha kwa ufanisi ili kuinua kipat cha nchi na mwananchi wake.

Leo hii, Tanzania na rasilimali zake zote ni nchi masikini, tena kwa kiwango kikubwa ni umasikini wa hiari na si kulazimishwa. Basi PPPT lengo lake la kumtoa Mtanzania na Tanzania kutoka Umasikini kuttokana na mfumo endelevu wa kiuchumi ambao unalenga kumpa Mtanzania uhuru wa mawazo na uwezo wa kuzalisha kwa kutumia utaalamu na teknolojia inayoendana na mazingira yake na huku PPPT ikihamasisha kwa vitendo kukua na kuongezeka kwa Uzalishaji mali kwa kutumia Juhudi Maarifa na ufanisi.
 
Mkandara,

Hayo niliyoandika ukurasa wa nyuma, nilishawahi hapa kuyaandika na kuwataka CHADEMA waje wajadili na sisi. Kuna kundi kubwa sana liliibuka kutaka kuingia CHADEMA kama wakiwa tayari kuwa na DEMEKRASIA ya kweli. Tulimtaka Mbowe kuwa tayari ku-step down mara ikionekana kuwa mambo yanamshinda na abaki kuwa kama kiongozi wa kawaida (Mzee) kama alivyo Mtei.

Kilichotokea kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, wote tulikiona. Walitumia mbinu chafu kabisa zilezile za CCM na hata Zitto alikiri kuwa Walimtenda Wangwe na alimuomba msamaha. Yeye pia, wenzake hao hao walianza kumtenda hadi humu ndani ya JF. Hii ilifanyika ili kumuacha Mbowe abaki peke yake mgombea U-Mwenyekiti wa Chama na NGO ya Mtei ibaki bado mikononi mwa Remote Control yake (mume wa Mwanae).

Kama Zitto ana ndoto za kuwa kiongozi mkubwa mbeleni, kuwa Mwenyekiti ilikuwa ni kujiweka Kitanzi huku ukitembea kwenye kamba nyembamba sana. Uwezekano wa kwenda hadi afikishe umri wa kugombea Urais huku akiwa bado kiongozi wa Chadema ilikuwa ni hatari sana. Angeanza kupigwa madongo ndani ya chama na nje ya chama, tofauti na leo ambapo yeye ni Mbunge tu na "Makamu wa Katibu Mkuu". Amejificha sehemu na madongo yote yanakwenda kwa wale wa juu yake. Ni heri kujijenga na uchukua chama kikiwa kimesimama vizuri, unapiga shambulio la mwisho na kuchukua form za uongozi wa juu wa nchi........ Mchuzi wa Mbwa hunywewa wa motomoto....

Sasa basi ukichukulia ile MIIKO ya viongozi tunayotaka kuiweka kwenye chama, hapa ndiyo unaanza kwa kugonga KISIKI. Mbowe na Mtei MILELE hawatakubali kabisa NGO yao ibadilike kiwe chama cha WALALAHOI. Nasikia mwengine huko kanunua helkopta mbili kwa ajili ya uchaguzi mwakani. Sasa akija kutuwekea makaratasi yake TUMLIPE, inabidi tu tuchukue chama na kumpa chote. Hii ndiyo ambayo hatutaki. Chama kikiwa na wachangiaji wa kawaida, na kupokea michango ya kaiwada, basi kesho hatakuja FISADI kudai anataka kuwa Rostam Azziz wa chama kipya/Chadema.

Hayo ndiyo haswaa yananifanya mie nisite kujiunga CHADEMA hadi leo. Ntajiunga kwenye chama ambacho WOTE karibu tutakuwa sawa. Hakuna kuburuzana zaidi ya Demokrasia. Kama mtu ataanza kutembeza PESA zake huko ili kujichukulia ushindi, basi huyo aondolewe mapema kabisa. Huyu atakuwa ni FISADI mtoto.
 
Mkandara,

Kwanza umeuliza kwa nini tusijiunge CHADEMA, pili ukaongezea kwa kuuliza kwa ni ntusijiunge na Chama kingine na kuleta mabadiliko ikiwa suala ni Uongozi Bora.

CCM, CHADEMA, CUF, TLP, NCCR, UDP, na wengine, tayari wana Sera zao, Itikadi zao na Katiba zao ambazo zimeundwa kukidhi nia ya Waliounda vyama hivyo.

Sisi tunaunda Chama chetu, chenye Itikadi, Sera na Katiba ambayo ni tofauti na hivyo vyama vingine.

Lengo si kukimbilia Uchaguzi Mkuu au kupigiwa kura mwaka 2010, lengo ni kujenga Chama kitakachokubalika kwanza na wanaotaka kujiunga nacho, Wanachama wake na Watanzania. Lengo la PPTL la muda mfupi si kupata Ubunge wa haraka haraka wa kiti kimoja kimoja, kugombea ruzuku au kugombea Urais ili kuking'oa CCM au kuwa chama maarufu cha Upinzani kwa jina.

Lengo letu litaoana sana na Waraka wa Mchungaji kwa Mtanzania. Nia si kupewa dhamana ya haraka kuongoza kisa tumeichoka CCM. La hasha, nia ni kuwaelimisha Watanzania kwa vitendo kuwa Chama chetu ni chama Mbadala ambacho kiko kwa ajili yao kwa kutumia vitendo na si kauli na hotuba kwenye majukwaa au kujivunia historia ya waasisi wa kuliongoza Taifa letu kuwa ndio kigezo cha PPPT kuaminika na kupewa dhamana ya kuongoza Tanzania.

PPPT kitakuwa chama chenye msukumo na mvuto wa kuchapa kazi na uzalishaji mali. Tutayatimiza haya kwa vitendo na si vijitabu au ilani zenye tenzi nyingi na maneno mengi.

Ndio maana tunakataa kujiunga na vyama vilivyopo ambavyo vimeshajenga usugu wa mawazo kuwa walicho nacho katika Katiba zao, Ilani na Sera zao ni mwanzo na mwisho na hakuna atakayeweza kubadilisha au kuleta mapinduzi mapya ya kuamsha Sera na Itikadi mpya au kuzifanyia marekebisho.
 
Mchungaji,

Nimekupata. Nasubiri kwa hamu kukiona. Wanasema siku zote shetani huwa amelala kwenye details. Ila kama kitakuwa kweli chama cha Watanzania bila ya Wajanja wachache kuwa WENYE CHAMA, basi andaa kabisa kadi yangu.
 
Sikonge,
Mkuu wangu hata mimi swala la Zitto kugombea uenyekiti sikuliafiki kwa sababu huo ndio Uti wa chama. He has so many enemies within kutokana na kupanda chati haraka, hivyo kama angekuwa mjanja angejiweka kando kabisa na kiti kile. Nakumbuka kuna mtu humu aliweka principal za kufanikiwa kupata POWER.. Zitto alicheza kinyume na ndio maana yote haya yametokea, after all kuwa mwenyekiti haina maana wewe ndiye mgombea wa Urais kwa tiketi ya chama.

Inawezekana, nilisoma humu kuwa kweli kwamba nafasi ya Zitto alitakiwa kupewa Rwakatale na Zitto akaishtukia mapema njama hiyo. Well ndani ya chama vitu hivi ni vya kawaida kabisa, tatizo lenu nyie wengi wenu ni vijana ambao hunfahamu mazito yanayokuwemo ndani ya vyama. Chama is a system, kama Mafia vile kuna Don mtawala na vyombo vyote vya usalama na kadhalika. Huwezi kuwa mwenyekiti ikiwa siri za juu huzifahamu ama huna influence nje ya chama hasa ktk vyombo vyote vya Kiusalama na Kiuchumi. Vyama vya siasa ni Cartel inayojijenga kwa maswala yote..

Chadema bado ni chama kichanga lakini kinakua na majaribio kama haya ni muhimu yawepo. Ndio demokrasia ktk ujenzi wake..Kama ungekuwepo TANU enzi za Uhuru ukaelewa majungu na vijembe vilivyotokea enzi hizoi hadi watu wengine kupoteza maisha na wengine mali zao wala tusingezungumza ya CCM leo..Ni part of learning.

Nina hakika Chadema, milango yao wazi tena unaweza chupa kupitia dirishani watakupokea tu. But for real ni lazima uijue system inavyokwenda na mchango wako utapewa nafasi yake. Mimi siziwezi siasa.. nasema saaana nje ya ulingo huo kama mbwa koko lakini nafahamu fika kinachoendelea. Politics is a game (win or loose), na uchezaji wake ni mgumu kuliko mchezo wowote duniani.
 

May I refer to this as shock and awe political doctrine?!
 

Mkuu, Vision yako kwa Tanzania ni nzuri sana lakini mkuu umesahau kutuambia msimamo wa chama kwa shirikisho la Africa Mashariki. Maana kwa malengo yako yatimie tutakuwa tayari tupo ndani ya shirikisho la EA na pengine Museveni au Kagame mmoja wao atakua Rais wa shirikisho!
 

Hatupo kwenye kutawala East Africa kichama rather than ki serikali. Chama ni ndani ya nchi sio nje ya nchi
 
Hatupo kwenye kutawala East Africa kichama rather than ki serikali. Chama ni ndani ya nchi sio nje ya nchi

Fair Player,

Nashukuru sana, maana mara nyingine inaelekea watu hawajui kutambu ni nini cha muhimu kwanza kifanyike kuijenga upya Tanzania.

Suala si kuwa na Majimbo, Mahakama ya Kadhi au EAC, tutakuwaje na kukimbilia kujiingiza katika mambo kama hayo huku hata uwezo wa kujilisha hatuna?

Tukiweza kujilisha kwa nyenzo zetu wenyewe, basi ndipo tutaanza kufikiria hayo mengine. Cha kwanza ni kurudisha imani kuwa tunaweza kujilisha kwa LISHE bora na kujitawala kwa HAKI na kuheshimu UTU na nafasi ya kila mtu!

Mengine ni matokeo!
 
Rev. Kishoka:

Je chama chako kinakuwa na military wing? Wengine tunaziosha AK47 zetu.
 
Ngoja niulize hivi mtu aliyeikimbia nyumba yake na kwenda kuhamia nyumba ya mwenzake eti kwa sababu mwenzie alikuwa na uwezo wa kuthubutu na kufanya maamuzi sahihi na kuijenga nyumba yake anakuwa na uwezo wa kurudi kwa mbwembwe?

Nyie wazamiaji kwa sababu mbali mbali ebu acheni kutusanifu jamani badala yake muendelee kumshukuru Mungu kwa kuwapa nafasi ya kufaidi maamuzi ya watu wengine. Sisi wenzenu ambao tuna uwezo wa kuzamia kama nyinyi na kuwa huko lakini tumechagua kubaki na kupigana humu hatuitaji hizo kejeli zenu.

Kwa kweli laiti kama mngejua maisha yetu yakoje kwa sasa huku mtaani nadhani huu utani usinge pewa nafasi
 
May I refer to this as shock and awe political doctrine?!
Right on bro.. it is and strange enough would work right.
Mkuu wangu msome Shalom kisha fikiria nje ya box utanielewa. Ninajua mna makusudio mazuri sana lakini kama mtakavyoanza ni muhimu kuzingatia WATU wenyewe na katika MAZINGIRA yapi.. sasa hivi wananchi wote wanalia SOS, wanahitaji Nabii wa kuwaokoa kama alivyofanya Mussa. Baada ya kuwavusha toka hatarini ndipo alipowapa sheria za Amri 10. Ndicho nachokishauri.

Amini maneno yangu na mfikirie sana what is at stake right now, Swala la UONGOZI BORA ni muhimu kuliko mengine yote na hatuwezi kufanikisha hivyo pasipo kutumia njia ambazo wengi hawazioni umuhimu wake.
Kama nilivyosema hapo mwanzo UONGOZI BORA ni swala la Dharura, kama ilivyo Umeme na kuanzishwa kwa PPPT ni suluhisho la muda mrefu ambalo pia wananchi wanalisubiri. Right now mfanye kama ya Yesu kuwapa watu mkate na mvinyo kisha wafundisheni Gospel..akili zao haziwezi kufanya kazi wakiwa na njaa, machungu na adha isokuwa na kifani.

Kwa nini sikuwaomba mjiunge na CCM ni kwa sababu chama hicho ni sawa na Dowans, pamoja na dharura tulokuwa nayo hatuwezi kuchukua madudu ya CCM na kutegema vinginevyo, na hata kama mtaweza leta mabadiliko ndani ya CCM gharama yake kwa wananchi itakuwa kubwa sana. CCM itabadilishwa na viongozi wake wenyewe. Nimemsoma Rev. Kishoka na kila naposoma inanipa sura ya kwamba, PPPT haitegemei wala kupania Ushindi mwaka 2010. Wananchi can't wait that long, amini maneno yangu wakuu zangu.

Wekeni nguvu zetu kwa vitu vilivyopo kwani huwezi kuishinda CCM mkiwa mmegawanyika na hata siku moja msifikirie kuwafikia watu vijijini ni kazi ndogo. Ni kazi kubwa sana kuliko kukitangaza chama mjini kama ulivyo usafiri wetu. safari ya kwenda Ukerewe ni lazima ukatambikie kwanza na hujui utafika lini ndivyo habari za ujio wa PPPT utakavyochukua muda.

Sizungumzi hivi kwa sababu mimi ni mwana Chadema au nimetumwa na mtu yeyote isipokuwa ni mawazo yangu huru baada ya kuchanganua matatizo yetu na ipi njia rahisi ya kuyaondoa.. Hata hivyo shukran mkuu wangu kwa kunisoma.
N.B - Au tufanye hivi nipandisheni chat na mimi basi, kuwa Mkandara kaweza kuwavuta Wapiganaji toka ndani na nje kuja kuliokoa taifa! haa haaa haaa!
 
lol, this is some classy humor!! 🙂


dont get me wrong, i did suggest the same as they are easy to pronounce. Lakini majina ya watoto ya siku hizi si unayajua tena, utagundua kuwa chama kitakuwa na jina rahisi, sio utani.
 
Shalom, leo hii ukimuuliza mtu yeyote kuwa mwasisi wa JF yuko wapi, kama hajapata kusoma au kuambiwa profile yake, mtu huyo atasema Maxence yuko nje ya nchi. Unakumbuka wakati ule amekamatwa, hq police hawakuamini kuwa ni kijana wa makamo tu na yupo hapa hapa Bongo ndiye amefanikisha kuwawekea Watanzania mbalimbali pahala pa kujadiliana na kuchambua mustakabali wa Taifa lao.

Sawa, wengi wa wachangiaji wako nje ya nchi, lakini leo hii unasau kabisa kuwa mkonge wa fibre optic umeanza kuwa na impact, walau kidogokidogo kwa Dar. Kuna vijana wengi sana wako hapa hapa bongo siku hizi na wanakuwa logged on kwenye net kwa muda mrefu, wakiwa makazini na wengine kupitia mitandao ya simu za mikononi.

Mambo ya sisi against wao katika mambo ya kitaifa hayafai pale unapozungumzia commitment ya Watanzania, majukumu yao, na mirengo yao kwa kuangalia tu pahala walipo kwa sasa. Tukianza kufanya hivyo ndipo tunapojiingiza kwenye sera za uzawa against wahamiaji, na walavumbi vs wabeba box.
 

Steve D:

Hivi uhuru Msumbiji ungepatikana bila wengine kuwa nje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…