Hii barabara imejengwa kwa kutumia mahesabu ya civil engineering na physics. Civil engineer anasoma mambo ya force na tension. Anajua kama daraja litabeba magari mia moja kwa wakati mmoja, basi litastahili kuwa na nguzo size gani. Wanafanya testing kwa lab ili kujua kama nguzo hizo zina uwezo wa kuhimili uzito wa magari yatakayopita juu yake. Hakuna guesswork hapa. Ni mahesabu ya force and tension ili kujua ni nguzo aina gani inayohitajika kuhimili uzito wa magari. Sasa kama unadhani hawa engineers wanafanya guesswork basi endelea kungoja daraja liporomoke.