Project proposal: Bustani ya dawa za asili

Project proposal: Bustani ya dawa za asili

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
8,647
Reaction score
9,604
Nina wazo la kibiashara la kuanzisha bustani (shamba) kubwa ambalo nitakusanya mimea mbalimbali toka nchini ambayo hutibu maradhi mbalimbali!
Lengo la mradi huu ni kuweza kufanya utafiti wa dawa za asili ambazo zimeonyesha uwezo wa kutibu magonjwa mengi endapo zikifanyiwa utafiti wa kutosha! mf tatizo la nguvu za kiume limeonekana linatibika zaid kwa dawa za asili kuliko za viwandani; Pia kuhifadi mimeaDawa iliyo katika hatar ya kutoweka.

Baada ya mimea ya hapa nchini nitahamia nchi za Africa na duniani kote! Ipo mimea inayopatikana bara America kusini na asia ambayo pia inaweza kumea Tanzania.

Kupata mimea hii kwa urahisi unaweza kuwatumia wafanya biashara.
Mami Yenu Ni Muhimu
Kidadari
 
Khaa!! Wakati wewe umekuja jf kutafuta maoni wenzako wako porini wanatafuta mbegu.. Wazo ndiyo jambo lenyewe
 
ndo mwanzo
Khaa!! Mwanzo ndiyo unakuja JF? Nilitegemea uje hapa uombe ushauri wa kutatua changamoto zinazokukabili kwenye utekelezaj?. Majirani zetu siku hizi wala hawafanyi utafiti tena. Wanakuja kwetu wanachukua zile tafiti tulizozifungia makabatini wanarekebisha kidogo ziendana na mazingira yao wanazifanyia kazi bila gharama kubwa, na hii ndiyo maana kasi ya uchumi wao ni ya kupaa wakati sisi tunaendelea kushabikia waendesha bodaboda na kina mamalishe kama ndiyo ajira kuu hapa kwetu :glasses-nerdy:
:glasses-nerdy:
 
Mkuu umenena jambo kubwa sana.Hatuna kawaida ya kutumia tafiti zetu.
 
Idea yako ni nzuri mkuu. Ila kama ulivyoshauriwa hapo juu.. Inaitaji immediate implementation.
...vinginevyo usijeshangaa jirani yako hapo unapokaa, ambaye pia ni member wa jf sasa hivi baada ya kusoma wazo lako ameanza kushughulika na sasa amepanda miti 7 tayari...
 
Nitafute nikupe orodha ya miti asili ya Tanzania , iko zaidi ya miti 6000, kama unaweza kuikusanya japo 25% ya idadi hiyo utakuwa na Bustani kubwa sana.
 
Wazo zuri.Siku moja nilikuwa naangalia TV nikaona wamarekani wanafanya Project kama hiyo wao walichukua mimea ya Jangwani ambayo ipo hatarini kutoweka wakaijengea kwenye Green House.Unaweza boresha wazo lako kwa hilo.Ila siku nyingine kuwa makini aina ya mawazo kuyaweka public huchukulika kirahisi sana kama hili.nakumbuka katika hangaika zangu za kitaa,nilikuwa mshiriki wa "Ndoto za Kitaa" nilikuwa na wazo zuri sana lakini nilipewa "Comment" kuwa wazo langu likionekana tu kwenye TV basi kesho yake utakuta mtu keshafanya.So zingatia ushauri Mkuu.
 
Back
Top Bottom