Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Nimesharekebisha. Usikwepe hoja ya msingi.

Huu ni mtihani kwa Kimaro na jinsi atakavyouchukulia ndiyo itaonyesha kama ni mtumishi wa Mungu kweli au ni mtu aliyelewa umaarufu na majivuno kiasi cha kudhani kuwa bila yeye kazi ya Mungu haiwezi kuendelea.

Mungu na Amsaidie [emoji1545]
Umeeleweka Mkuu.Tumuombee Mchungaji aweze kulimaliza salama[emoji120]
 
Nimekufuatilia sana nikagundua wewe mfia kkkt na haukubaliani ma mabadiliko ya kiroho.
Bado unaipenda kkkt iliyodumaa kiroho na hukupendezwa na huduma za uamsho za Kimaro.
Nimekugundua kuwa umhafidhina na sio imani sahihi ya Kikristo.

Kkkt ni dude kubwa ambalo halina msaada katika jamii bado lipo kuwanyonya wa kkkt kimapato ilhali mrejesho katika jamii ni hafifu sio kiriho wala kimwili.

1. Shule za kkkt ziko kipigaji ma ziko taabani
2. Hotel ya corodor spring wakunwa walipiga zaidi ya 3B waumini wamechangishwa karibu wafe na wakakimbia walio wengi.

3. Selian hospital nahitaji kusema zaidi?

Bora Kimaro mara 1000 kuliko hao wachungaji na maaskofu vihiyo.
Upigaji upo huko wa kutisha.
 
Wewe ndio ziro kabisa. Mfano wa Yesu mbona ni tofauti na Kimaro?. Mchungaji unadai vijana wa kikikristo wote sio waaminifu. Kisa umeibiwa na vijana wako wa kanisani kwako?

Alitakiwa kuaanda semina ya kufundisha vijana kuhusu uamnifu na sio kutoa kauli ya jumla kwa vijjana wote. Yule sio mchungaji ni motivational speaker
Unafikiri uchungaji ni kama mwalimu akiamka anaenda kufundisha somo kufuata silabasi
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]daah naona sasa mmeanza vita na RC
Hakuwasaidii kumaliza matatizo kibao waliyonayo kkkt.Wamalizane na Kimaro,wamgeukie wa Kimara.Kanisa lina heka heka muda wote [emoji3][emoji3]
 
Hivi kumbe ni project zake binafsi, mimi najua ni project za kanisa na zimejengwa kwa nguvu ya michango ya waumini na ni utaratibu wa makanisa yote ya KKKT hata hapa mbezi beach tuna similar projects na zinafadhiliwa na michango ya washarika
Meku amekamata watu nyota...
 
KKKT mnajimaliza. Tunawaonea wivu Kwa dhahabu mnayoichezea. Unajua Kwa nn hakuna projects za maana Kwenye misikiti mingi? Governance!
KANISA LILIKUJA DUNIANI KUMUOKOA MWANADAMU, NA MWANAADAMU KUITANGAZA INJILI ILI TUMJUE MUNGU, LEO KANISA LIMEKUWA KAMA KAMPUNI, WANAKIMBIZANA NA MALI MATOKEO NDO HAYA UGOMVI USIOISHA WATU HAWAGOMBEI INJILI WATU WANAGOMBEA MALI (MASLAHI BINAFSI) MUNGU HANA TENA NAFASI, HAKUNA NENO LA MUNGU HAPO, MALI MALI MALI, MUNGU ATUOKOE, TURUDI KANISA LA ZAMANI, ELIA NA ELISHA WALIKATAA MALI LEO WACHUNGAJI NA KANISA KARIBU WATATOANA ROHO KISA MALI ZA KANISA, MCHUNGAJI KALETA HIKI NA KILE ANATAKA KUDHIBITI KANISA LINATAKA KUDHIBITI, YESU ALITANDIKA WATU KANISANI WAKIBADILI FEDHA LEO BANK ZA KANISA KILA KONA.

USHAURI
TUWAPE WAHINDI VITEGA UCHUMI VYA KANISA WAVISIMAMIE/WAVIENDESHE WAKRISTO WALIOBAKI WOTE TUCHAPE INJILI, KUANZIA ASKOFU,MCHUNGAJI, MWINJILIST, MSHARIKA... HAKUNA KUGUSA SINGLE CENT... HADI KIAMA NO KESI,

WASALAAM.
 
Watumishi huwa wanahamishwa, nadhani hata serikalini au taasisi uoyote hayo yapo na kila taasisi inafanya kukingana na miongozo na taratibu zake, kimaro alikua kariakoo akaletwa kijitonyama na sasa ameondoka atapelekwa pengine akaendeleze utumishi wake

Sasa mnataka akae kijitonyama milele?

Mnapiga kelele wakati hata Dayosis haijatoa statement mjue upande wa pili wa shilingi ukoje, mmekua wepesi kuhukumu
Makundi kujijengea makundi..
 
Kwenye kila baraka kuna laana
Kila penye mafanikio pana mapungufu
Kufanya mambo fulani hakukufanyi kuwa mkubwa kuliko taasisi
Mtazamo wangu mimi kwa nyinyi mnaosema hakuna mkubwa kuliko taasisi mimi nasema wapo wakubwa kuliko taasisi maana taasisi hili ikuwe inahitaji watu makini na bora zaidi wa kuikuza.

Uwezo wa kimaro ni mkubwa sana anaweza anzisha taasisi yake na akapata wafuasi wengi kuliko.
 
Binadamu wanamuabudu binadamu mwenzao.

Yaani huyo mchungaji tu watu wanadiriki kusema taasisi itayumba kisa yeye hayupo.

Aisee ni hatari hii
 
Kila usharika KKKT una baraza la wazee, sharika ngapi zimefanya hayo yote? Nenda Usharika wa Sinza, hiyo Youtube Channel ikiwa live viewers wakizidi sana 15 na bado wanapambana na Deni mpaka kesho, Mwenge hali kadhalika.
NB: Kimaro hata apelekwe GEZAULOLE ataonyesha maajabu, jiulize kabla ya Kimaro-Knyama hapo Kinyama mbona kulikua jiiiii
Naam mkuu, na mimi nimekwisha tangulia kuwaambia hapa kwamba hili taasisi ikuwe inahitaji watu makini na bora zaidi kama akina kimaro,

Ndio maana mimi uwa ninamtizamo wangu wa kwamba kuna watu ni wakubwa kuliko taasisi.
 
Japo Kimaro huenda alivuma kupitia KKKT umri unamruhusu kuendelea na mengi ya mbeleni. Amechelewa kutoka huko mpaka kapewa 60 za nguvu
 
Tujikumbushe, projects kadhaa ambazo Mchungaji Dkt. Kimaro amezifanya akiwa Mchungaji Kiongozi, KKKT Usharika wa Kijitonyama,
1. School of Healing (Morning & Evening Glory) -Youtube Channel (mwanzoni ikiwa Eliona Kimaro TV baadae KKKT Usharika wa Kijtonyama) inayowafikia watu wote Duniani.
2. TAMASHA LA MBINGU KUJAA SIFA (kila mwaka)
3. Jengo jipya la Sunday School (lililogharimu yapata takribani 200m TZS)
4. Ununuzi wa Kiwanja pembezoni mwa kanisa yapata 300m TZS
5. Kusomesha yatima yapata 100
6. World Pray Online (WPO), Call Centre ya maombi masaa 24, siku 7 za wiki.

NB: Ikumbukwe waliokuwa wanasali hizo Morning & Evening Glory wengi hawakuwa waumini wa KKKT bali wa madhehebu mengine na Waislam kuondoka kwake Dkt Kimaro tutarajie mabadiliko kiasi.

***Mchungaji Kiongozi (Mpya) Anna apewe ushirikiano kuendeleza alipoishia Dkt Kimaro.

Hata Mussa aliazisha safari ya kutoka misiri kwenda kanaani ila hakufika ,so mm naona watu wengi mnasumbuliwa na ujinga uliojaa giza nene kuhusu imani,,,can you imagine mtu mzima na akili yako eti unalia na kuandamana eti kisa mchungaji kuhama aisee!!!Mungu atusaidie,,lia Mungu akikuacha unamlilia mchungaji????? Huu ndo uenda wazimu uliopita kawaida.
 
Back
Top Bottom