Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Sasa kama ni utaratibu uliowekwa na Dayosisi hizi re-shuffle za wachungaji zina maana gani?
Watumishi huwa wanahamishwa, nadhani hata serikalini au taasisi uoyote hayo yapo na kila taasisi inafanya kukingana na miongozo na taratibu zake, kimaro alikua kariakoo akaletwa kijitonyama na sasa ameondoka atapelekwa pengine akaendeleze utumishi wake

Sasa mnataka akae kijitonyama milele?

Mnapiga kelele wakati hata Dayosis haijatoa statement mjue upande wa pili wa shilingi ukoje, mmekua wepesi kuhukumu
 
Watumishi huwa wanahamishwa, nadhani hata serikalini au taasisi uoyote hayo yapo na kila taasisi inafanya kukingana na miongozo na taratibu zake, kimaro alikua kariakoo akaletwa kijitonyama na sasa ameondoka atapelekwa pengine akaendeleze utumishi wake

Sasa mnataka akae kijitonyama milele?

Mnapiga krlrl wakati hata Dauosis haijatoa statement mjur upande wa pili wa shilingi ukoje, mmekua wepesi kuhukumu
Polee
 
Kwa hali hii kama KKKT hawatakaa chini waongee vizuri na Mch Dr Eliona Kimaro, watapoteza big time. Nawashauri wafikirie upya uamuzi wao wa kutaka kumfukuza mchungaji huyu wasije wakalia na kusaga meno hapo baadaye.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Yani walie kisaa washirika wataondoka kumfata kimaro au?? Walie kisa sadaka kushuka au??? Walie kisa nini... yani kimaro kkkt ni kama chembe ya mchanga kwenye dunia.
 
Watu mnamjazaa sana ujinga Kimaro alafu nae ni mtu mzimaa ilaa haoni hata akioneshwaaa hao washirikaaa Watabaki Kijitonyama na yeye ataiacha kijitonyama maana yeye sio wa kwanza hapo na wala hatakuwa wa Mwisho...!! Uhuniii kama huu wa kutaka kujikutaa Mungu mtu kwenye kanisaa hauruhusiwii kabisaa..
 
Aaa wapi!

Kazi ya Mungu itaendelea bila hata ya Kimaro. Hawa ni watumishi tu na msiwakuze sana kiasi cha kuwapa utukufu. Mungu Atainua wengine na pengine bora zaidi. Tufike mahali tuache kuabudu watu na waabudiwa hawa nao watambue kuwa wanaweza kuondolewa na hata kufa wakati wo wote lakini kazi ya Mungu itaendelea!

Kimaro ajirekebishe. Ajishushe. Aombe msamaha na aendelee na wito wake - Kijitonyama au kwingineko. Na Mungu Atazidi kumtumia.
Umesema vyema. Tatizo kubwa watumishi wanataka waabudiwe badala ya kuhuburi utukufu wa Mungu, imefika mahali waumini wanaona bila mtumishi fulani hatuwezi....hii sio sawa
 
KKKT mnajimaliza. Tunawaonea wivu Kwa dhahabu mnayoichezea. Unajua Kwa nn hakuna projects za maana Kwenye misikiti mingi? Governance!
Sasa hapo tunajimaliza na nini, kila usharika una projects kubwa na hayo ni maono ya KKKT kama taasisi na sio maono ya mtumishi mmoja, mbona makanisa mengi ha KKKT yana miradi mikubwa mbali na kijitonyama? Hebu acheni fitna
 
Watu mnamjazaa sana ujinga Kimaro alafu nae ni mtu mzimaa ilaa haoni hata akioneshwaaa hao washirikaaa Watabaki Kijitonyama na yeye ataiacha kijitonyama maana yeye sio wa kwanza hapo na wala hatakuwa wa Mwisho...!! Uhuniii kama huu wa kutaka kujikutaa Mungu mtu kwenye kanisaa hauruhusiwii kabisaa..
Mbona unamshutumu Mchungaji? Una uthibitisho kuwa yeye amepingana na maamuzi ya Uongozi,au unamshushia lawama kutokana na maoni ya watu humu jamvini?
 
Kimaro ajirekebishe. Ajishushe. Aombe msamaha na aendelee na wito wake - Kijitonyama au kwingineko. Na Mungu Atazidi kumtumia.

Kumbe Kanisa limetoa sababu za kumpatia hiyo likizo ya siku 60? Na kama limetoa ni sababu zipi hizo unaozomshauri mpaka aombe msamaha?
 
Mbona unamshutumu Mchungaji? Una uthibitisho kuwa yeye amepingana na maamuzi ya Uongozi,au unamshushia lawama kutokana na maoni ya watu humu jamvini?
Hapana nimemjibu anaesema bila kimaroo kanisa litadodaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Sasa kimara ni nani kwani kkkt???
 
Msasani ni tofauti na yale majengo ya kijitonyama na mbezi beach nadhani based on location
Wachungaji makini alipaswa in kufikiria kabla ya kwenda kuchukua mkopo benki (white elephant projects)
 
Kumbe Kanisa limetoa sababu za kumpatia hiyo likizo ya siku 60? Na kama limetoa ni sababu zipi hizo unaozomshauri mpaka aombe msamaha?
Kwani likizo ni muda gani??? Nani anaepanga utararibu wa likizo kwa wachungaji?? Mnataka kulipangia kanisa mpaka utaratibu wa likizo kisa kimaro acheni uhunii
 
Kumbe Kanisa limetoa sababu za kumpatia hiyo likizo ya siku 60? Na kama limetoa ni sababu zipi hizo unaozomshauri mpaka aombe msamaha?
Ndio maana ameambiwa apishe kwa muda wa siku 60 uchunguzi ukamilike, sasa nyie mmeanza kushuyumu maamuzi ya kanisa kabla hata uvhunguzi haujakamilika na watu kupewa taarifa

In and all KKKT kama taasisi huwa inatoa taarifa ya maamuzi yoyote kwa waumini wake kwa hiyo tujipe muda
 
Hatujui kwa hakika tuupe muda wakati.. Lakini unapokuwa kiongozi wa kiroho punguza kidogo ya kimwili
Msikilize na mchungaji Hananja, amesema mengi yanayoonesha angalu issue ni Nini. Wivu na unafiki kaviongelea pia
 
KKKT ni taasisi na sio Mali ya mtu binafsi

Anawajibika Kwa taasisi ambayo ndiyo mwajiri wake

Taasisi ndiyo inajua kwanini imempa likizo ya siku 60

Umaarufu wake hauondoi mapungufu yake
Aende akafanye hayo mazuri sehemu nyingine. Hiyo ndio ilikuwa mifumo ya wamisionari. Unapelekwa sehemu ngumu ukiweza kuleta maendeleo unajamishwa na kupelekwa sehemu mbovu zaidi.
 
Hapana nimemjibu anaesema bila kimaroo kanisa litadodaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Sasa kimara ni nani kwani kkkt???
Umesema "watu wanamjaza Mchungaji na yeye anajaaa".Ndiyo maana nikakuuliza.Mchungaji nimeona video yake akiwaaga waumini na akaweka bayana anatii mamlaka,sasa haya mengine ni maoni tu ya watu na have nothing to do na Mchungaji Kimaro.
 
Hatujui kwa hakika tuupe muda wakati.. Lakini unapokuwa kiongozi wa kiroho punguza kidogo ya kimwili
Ni kweli mshana, mtumishi wa kiroho lakini anaongozwa na mwili hafai kabisa
 
Back
Top Bottom