Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe unamfuatiliaga Man ndoga bibie Faiza?Hujaielewa falsafa yake wala hujamsikiliza mandonga akiongea.
Falsafa ya Mandonga ni akishinda au akishindwa ulingoni yote hayo ni ushindi kwake.
Hivi wewe hujaona kuwa mapambano mawili yaliyompatia umaarufu wa kujulikana mandonga alipigwa ulingoni?
Fatilia kidogo.
Mandonga yupo kivingine kabisa na kaelewa namna ya kuitumia hii fursa iliyopo kwenye media.
Wengi wetu mamndonga akishinda hatuna raha. Tunataka anyukwe tuone anavyopanguwa hoja nje ya ulingo.
Mandonga ndiyo mwanamichezo pekee anayeelewa kutumia fursa za kushindwa mchezoni.
Mandonga haingii ulingoni kuuwa wala haiingii kujiuwa, akiona unamzidi anajitupa anahesabiwa, ananyanyuka, kipato kishajiingizia, anapiga porojo nyingi, mnamtafuta kwa promo anaendelea kula pesa kuliko mshindi.
Mandonga akishinda au akishindwa ulingoni anabaki kuwa bingwa.
Katika miaka ya sitini huko, kuna Mkimbiaji wa Tanzania "John Stevens" alipata umaarufu mkubwa duniani siyo kwa kushinda bali kwa kushindwa, alikuwa wa mwisho kabisa kwenye Marathon. Mtafute kwenye mtandao utamuona ni vipi kushindwa kulimpa umaarufu.
Refaree kamuokoa ashukuru Mungu angejifanya kukaza yangetokea ka ya Dodoma lile bonanza la mbungeNaona tangazo la mchezo wa ngumi, ([emoji3037])
Kati ya Karim Mandonga na Golola Moses kutoka pale Kampala Uganda, tarehe 29 mwezi huu wa July, Kwa kifupi promota anayeandaa hili pambano pamoja na Mandonga mwenyewe aliyekubali hili pambano ni kwamba hawana akili.
Golola Moses ni bondia mkubwa sana pale Uganda japo alianzia kwenye Kik boxer, hata Dulla Mbabe hawezi kumpiga Golola, wajaribu kupitia upya wasifu wa Golola.
Mandonga usipokataa pambano hili ndo unaenda kuwa mwisho wako kucheza tena jukwaani
View attachment 2692468View attachment 2692469