Mudawote
JF-Expert Member
- Jul 10, 2013
- 10,771
- 14,129
GTs,
Nadhani kila mmoja ni shuhuda wa yanaoendelea kuhusu nchi yetu. Kuna mambo kadhaa mengi ambayo kila mtanzania anayalalamikia, moja wapo ufisadi, kutokuwajibika, watu kutekwa na wanaojiita polisi na kuuawa etc. Tuhuma zote hizo zinahitaji majibu toka kwa mamlaka husika, ila bahati mbaya ni kinyume inatokea. Nitatoa mifano michache ya jumla.
1. Kuuawa kwa kada wa kile chama cha Mbowe. Ajabu badala ya kuhitaji uwajibikaji ndani ya jeshi la polisi na vyombo vingine basi CCM tumejikita kutengeneza na kusambaza uongo eti ionekane Mbowe ni mtekaji.
Kibaya zaidi watu wengi bado hawajulikani walipo na Mbowe na kigenge chake cha chama wameitisha maandamano wakitaka vitu simple tu, majibu ya hao waliopotea ila cha ajabu sisi CCM tumekazana na kutengeneza vi clip eti wafuasi wa Mbowe wanampinga eti maandamano.
Hivi mtanzania mwenye akili yeyote mwenye uelewa mpiga kura hawezi kung’amua kuwa hizo ni clip zimetengenezwa na wahuni wahuni tena wala siyo wafuasi wa mbowe???
Hivi sisi kama CCM tumekosa kabisa mkakati wa kuona namna ya hawa wenzetu wanavyoumia tuone namna hata ya kuitisha press conference ya pamoja tukakubaliana hata kufanya maandamano ya pamoja hata ya siku mbili kuonesha solidarity ya kweli watanzania wameumizwa na utekaji???
Au kwa nini na sisi kama CCM tusiandae maandamano yetu ya Amani???? Lakini unakuta CCM tunaeneza propaganda ambazo kila mtanzania anaona sisi ni wajinga wajinga tunatetea ufisadi, wizi na utekaji.
Nashauri think tank ya CCM ibadilishwe watu wenye akili ndogo waondolewe waweke watu wenye akili kubwa hapo chama chetu kitakuwa na ushawishi kwa vijana na wasomi.
Ila kwa mtindo wa sasa tutaendelea kupata kura kwa watu wa vijijini tunaowapatia kofia, tisheti na vitenge ila hawa vijana wa sasa tusahau kura zao.