herikipaji
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 1,198
- 1,369
Leo mkuu wa nchi ambae ni Rais ameagiza na kuruhusu mashirika kuajiri watumishi wa umma moja kwa moja.
Hii ina maana sasa hayo mashirika mfano TRA, TANESCO na mengine yaliokuwa yatumia PSRS sasa yamepewa ruhusa kuajiri tena bila kupitia PSRS.
Maoni yangu hii haitokuwa vizuri.
Sababu mwanzoni kabla ya mfumo wa PSRS haya mashirika yalikuwa na fursa ya kuajiri lakini yalishindwa kuendesha mchakato wa ajira kwa taratibu yenye kufata misingi ya haki na maslahi ya taifa.
Kurekebisha ukaanzishwa mfumo wa sasa wa PSRS.
Mfumo huu wa kupitia PSRS wanaajiri upo kisheria, sasa hayo mashirika kuajiri tena ni kwa sheria ipi au wanafata maagizo ya mtu mmoja kama kawaida ya Tanzania?
Hivi nchi inaongozwa kwa kufata katiba na sheria au maagizo tu ya mtu?
Mfumo wa PSRS umekuwa msaada kwa wengi, wako ambao wamepata ajira bila kupitia njia za kujuana au kupeana rushwa, njia za ujanja ujanja, lakini wamepata na leo wako makazini.
Awali mashirika yalikuwa yanaajiri kukaonekana shirika moja linaweza kuwa na watu wa kabila fulani tu ngazi ya juu hadi chini, ubabaishaji, rushwa, kujuana na wengine wasio na mtu referee au wasotoa rushwa hata interview hawakuitwa kurekebisha hayo ukaekwa mfumo wa PSRS.
Sasa agizo la kuruhusu mashirika yaanze tena kuajiri anataka kuturudisha kule tulikotoka kwenye ubabaishaji, ajira za kujuana na mengine ya namna hiyo?
PSRS wana mapungufu hayo inatakiwa yafanyiwe kazi lakini si kurudisha ile corrupt system ya kuajiri kama anavyoagiza irudi.
Tumeona na hata dunia inafahamu hulka za Watanzania walio wengi, hawana uadilifu, majizi, wapenda rushwa hata hayo mashirika yamekua yanajiri pasipo kupitia PSRS mfano TANROAD lakini vijana wengi wameishia kulia kutokana na madudu yanayofanyika katika mchakato wa ajira kwa hayo mashirika.
Hayo mashirika yakiajiri hayatendi haki.
Yalikuwa yanaajiri hayakutenda haki, ukaletwa mfumo wa PSRS angalau umekuwa unaajiri kwa haki ukiachana na mapungufu madogo madogo yaliyopo.
Sasa kurudi kule Babylon kuajiri kupitia mashirika yaleyale tena inakuaje sasa yamebadilika?
Nini kimebadilika kwa hayo mashirika yalokua hayaajiri kwa haki na sasa yanaruhusiwa tena kuajiri?
Kama hilo agizo la rais likifanyika wengi watalia, wengi watakosa kupata hizo ajira wataishia kuajiriwa ndugu, wenye kutoa fedha kuhonga rushwa, ukabila.
Kimsingi bila kufahamu vema ni anaruhusu madudu yarudi tena mambo yakuwajaza watu uwanja wa taifa kupigania ajira ambazo washapewa wachache yatarudi tena, subirini muone.