PSRS interview questions (written, pract & oral)

Mwamba una nafasi yako ya kipekee pale mbinguni.ulinipa hints za written alafu nikapita nazo juu juu sikuwa siriasi alafu nikayakuta japo nikumbuka mojaoja lkn it was great

Ubarikiwe..

Tupe nondo za oral broo
Tuishi humo kiongozi tunasemaga saidia unapoweza mzee kwahiyo kama nakijua kitu nitakwambia tu
 
Mrejesho:


Kwakweli ni kwamba mimi kwa mara ya kwanza nilifika utumishi kwaajili ya written interview. Niseme tu nilifika Dodoma saa saba usiku kutokana na mazingira ya kusafiri kuwa magumu.Mara baada ya kufika sijuwa na sehemu ya kufikia,hivyo ilinilazimu nikeshe barabarani sehemu ambapo watu wapo muda wote.Asubuhi nilinunua maji nikanawa uso na kuchukua toyo mpaka UDOM.

Nilipofika nilihamaki uwingi wa watu! Nikasema Mungu hiki ni nini? Nikajisemea nimekuja kufanya nn huku? Nikiwa ninaonekana mshamba na upweke nisiye na hata rafiki wa kujadili naye chochote nikiwa nimesimama pembeni ya lecture theatre 1 kule college of business and education.


Baada ya muda walifika wasimamizi wakaanza kagua vyeti,nikafoleni nikaingia nikiwa na unyonge,ushamba,uchovu na usingizi mkubwa huku nikiwaza kuwa I am just trying.

Kweli paper ikaletwa,tukaelekezwa then tukafanya.Kiukweli ilikuwa NGUMUUUUUUUU! Ila inafanyika kwa wale wasomi na wafuatiliaji wazuri wa sera ya serikali katika utoaji wa mikopo kwa elimu ya juu.Ufanyaji wangu ulikuwa ni wa kujikongoja,huku nikihakikisha kila swali nagusa.


Nilijibu short and clear. Huku nikiwa nimekata tamaa. Ila kuna wanaume na wanawake haswaa waliomba hadi karatasi ya pili.Nilitoka na kuwahi stand nikapata chochote na kuanza safari ya kurudi kijijini kwetu nikiwa sina matumaini Yoyote.

Matokeo:

Leo nimeshikwa butwaa et nipo SELECTED FOR ORAL! Sikutegemea kabisa.Msimamo wangu ni kuwa nitarudi tena Dodoma kuwasikiliza maboss wakandaji live,nitakwenda KUJARIBU hiyo Oral.Sijawahi simama kwaajili ya Oral ila niwakute hukohuko hao wakandaji.Nikikosa basi,nitashukuru Mungu kwa kila kitu.


Kila lakher kwa woteeee mnaopigania huko,Mungu awafungulie njia.
 
Kila la heri
 
All the best mkuu
 
Mwamba una nafasi yako ya kipekee pale mbinguni.ulinipa hints za written alafu nikapita nazo juu juu sikuwa siriasi alafu nikayakuta japo nikumbuka mojaoja lkn it was great

Ubarikiwe..

Tupe nondo za oral broo
Umepita kwenda oral lakini?
 
Hongera Sana hyo Ni yako
 
Utumish facken sana nimepambana nimepata above 50 ila cutting point above 56 [emoji23][emoji23][emoji1373][emoji1373][emoji1373]
Hahahahaa, pole sana mkuu.

Yaani mnafukuzana kuimprove, wewe ulipoimprove na wao wakaimprove cut off.

Usikate tamaa mkuu, siku yako ipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…