Habari ya muda huu wanajukwaa.
Nimelazimika kuandika hapa jukwaani kuhusu taasisi tajwa hapo juu. Tangia mwezi oktoba nilijaza fomu za kuomba fao. Nilijibiwa kama taarifa zimepokelewa na mwajiri na pia ofisi za PSSSF
Isitoshe nimewapigia simu wakasema watalipa mwezi September. Hawajalipwa bado. Mara wanasema mhasibu hajapeleka vocha mara subiri mwezi December.
Mzee Abdu Razak Badru simamia haki za watu. Waambie wahasibu wako waache urasimu.
Ninajaribu kujiuliza maswali yafuatayo mara baada ya kuwapigia simu hawa wasumbufu
1: Eti wanasema mhasibu alitoka ofisini akasahau kupeleka vocha benki. Je hiyo ni ofisi au ni duka la mtu? Akisahau leo kesho hapeleki?
2: Wanasema eti wanafanya malipo mwisho wa mwezi. Hapo ndio nimestaajabu. Mwisho wa mwezi kwani huo ni mshahara? Kwanini unakaa na taarifa za mtu kwa muda mrefu kisha ukimaliza unatoa visingizio visivyona mbele wala nyuma?
3: Au mnachukua hela za wateja mfanyie mizunguko yenu kisha ndio mnawaingizia. Mhasibu achunguzwe. Kunajambo hapo.
Ninachoweza kuwaambia PSSSF nikwamba LIPENI HELA ZA WATU KWANI NI NGUVU NA JASHO LA WATANZANIA WENZENU.
Nawatakia utekelezaji mwema.