KERO PSSSF fanyeni malipo acheni urasimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hao hawana haja ya kuchunguza. Wanafaa kutimua tu kuanzia Mkurugenzi hadi hao wavaa sare, ofisi isafishwe hiyo.

Ingawaje sio kama kila aliyepo hapo ni mzembe lakini ofisi imetawaliwa na uzembe.

Mhasibu ndio mzembe. Eti hapeleki vocha benki anajitia tu ubize.
 
Badru sio kiongozi kabisa, PSSSF inatakiwa Serikali iangalie kwa karibu sana if possible ni kumuondoa kabisa Badru
Tena ingebidi achapwe na viboko. Mzembe sana huyo. Kila taasisi anayokaa haiishi kero
 
Kwa mfano ofisi ya Iringa kuna dada yupo pale ku update taarifa za mteja tatizo na kiburi juu
Halafu utakuta hata shule hana. Rushwa tu ndio wayotaka. Dunia imebadilika watu wamejielewa kwa kiwango kikubwa
 
Hiyo ni kweli. Bora muda mchache wenye ufanisi kuliko huo utapeli wanaowafanyia watu na hela zao
 
Kwa mfano ofisi ya Iringa kuna dada yupo pale ku update taarifa za mteja tatizo na kiburi juu
Nadhani OFISI zao nyingi ziko hivyo.

Huyo ndugu yangu alikuwa na ma gap ya michango kwa miezi kadhaa jambo lilimfanya asiwe na sifa za kupata fao la uzazi. Mwajili ana confirm kwamba michango yote ashapeleka.

Baada ya kufatwa ndio jamaa wanajaza zile gaps tena kwa miezi inayotosha kulipa hilo fao, miezi mingine wameacha gaps tena!

Sasa unajiuliza, ina maana hiyo michango wanakaa nayo ukifatilia ndio unajaziwa na usipofatilia unapoteza?
 
Huu uzembe unaanzia serikalini. Hata waziri husika wa hiyo taasisi atakua kanyaga twende. Sio mfuatiliaji maana malalamiko ni mengi
 
Hawa PSSSF wana shida si bure, wana sema sasa utume taarifa online lakini response yao imekuwa shida sana.
Nimeshuhudia kama wawili wameclaim mwezi October lakini mpaka leo hamna kitu.
Wakimaliza wanataka vitu vya kipuuzi. Mara barua sijui ya kuthibitishwa sijui kitu gani kutoka kwa mwajiri nk
Huo ni urasimu tu
 
Wangeweka mfumo mambo yote yawe automated na system. Mambo yakudili na watu wa serikali inakua ni kufungua milango ya Rushwa ili kurahisisha kazi sasa hawa wa NSSF usipokua mwepesi wa kunyoosha mkono sio kwamba tu utachelewa, hata kupata unaweza usipate kabisa.
 
Wanao mfumo mkuu, unaonyesha kila hatua naona shida ipo kwenye kuapprove kila hatua.
 
Hao PSSF nao kuna dada alikua anafuatilia fao la uzazi kwa miezi mitatu.

Na mpaka amewalambisha ndio eti wanamfanyia haraka ku process malipo yake!

Sasa unajiuliza kwani lengo la kutoa fao hilo ni nini? Fao la uzazi hadi mtoto anaanza kukaa ndio unalipwa.

Huo ni wizi wa dhahiri.
 
Wanao mfumo mkuu, unaonyesha kila hatua naona shida ipo kwenye kuapprove kila hatua.
Wana roho za kikatili tu. Wana approve nini wakati ukiwauliza wanasema wanaingiza kati ya tarehe 22-25 mhasibu ameshakamilisha taratibu zote, Halafu wakimaliza hawaweki hela!

Sasa tatizo huoni kama lipo kwa mhasibu na mkurugenzi?

Nasema tena Badru ni tatizo. Ajitathmini.
 
Mfumo upo tena hausumbui ukiwa na documents zote unamaliza fasta
Hapo ndo kasheshe inaanzia hapo.

Afisa Utumishi wako aipitishe ndio ipelekwe PSSSF ikifika huko inaandikwa processing kila siku, yaani ni shida!

Ukipiga simu ndio unaambiwa mara Mhasibu katoka, mara Fulani Yuko safari au likizo. Ni shida tupu.
 
Bado sasa huo sio mfumo automated, wamehamishia majukumu yao kutoka physical kwenda online ila means wasipofanyia kazi mfumo hauna msaada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…