Nafikiri kuna kitu hakipo sawa kwenye uendeshaji wa hii mifuko
Chukulia mfano KENYA ambao wapo serious na uendeshaji wa mifuko yao. Wafanyakazi wa Serikali huchangia 5% na private 10% wakati huku Tanzania tunachangia mara mbili yao halafu kikokotoo chetu ndio kimekuwa cha mawazo kuliko cha kwao wanao changia nusu yetu.
Nafikiri wakitaka mifuko (PSSSF & NSSF) inufaishe wastaafu, waanze kwanza kuhakikisha
1. Hela zilizokopwa zinarudishwa (hata kwa awamu hadi ziishe)
2. Miradi ya hovyo hovyo (magorofa ambayo hayana tija) nk yauzwe hela irudi kwenye mifuko japo kwa gharama za uchakachuaji za hiyo miradi huenda tukaishia kupata nusu yake.
3. Wawekeze kwenye miradi yenye tija na gharama ziwe halisi. Kuna magorofa niliona Arusha barabara ya Kijenge yapo barabarani hata sijui walipataje kibali cha kujenga hapo wakati miaka 10 ijayo barabara inaweza kupanuliwa na hayo magorofa ya mabilioni kushuka dhamani
4. watumishi wa hiyo mifuko wanaojikopesha hela bila riba huku wenye mifuko wakiteseka wachukuliwe hatua
Wakifanya hayo; kulipa wafanyakazi 50% ya mafao na kuendelea kuwalipa pension ya kueleweka inawezekana...
Mbona tunakopy na kupaste vitu vya ulaya LAKINI hatukopy vikokotoo vyao???