PSSSF malipo ya pensheni kwa awamu haifai mkiri tu kwamba hamna pesa

PSSSF malipo ya pensheni kwa awamu haifai mkiri tu kwamba hamna pesa

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Tatizo hili lili watokea wengi ma askari waliokuwa wanalipwa pensheni miaka ya nyuma awamu ya tano, kwa uzoefu tulijua pensheni hulipwa zote sasa hii habari imekuwa ni kikwazo sana kwa mtu anayetaka kufanya maendeleo ya haraka.

Kwann PSSSF msitoe tangazo rasmi kuwa pesa hamna vizuri maan itasaidia kuwaandaa wastaafu kisaikolojia na wajue wanafanyaje na kipato cha kwanza.

Mtu una staafu badala ya kuanza tu na mshahara wa mstaafu wanakuacha usote na unasota kweli kweli si mchezo, hawana huruma na watumishi hawa PSSSF.

Tunahitaji mabadiliko aidha kwenye ngazi ya maamuzi au anayehusika kuhujumu PSSSF.
 
Tukiri tu japo tumesema sana ila kipindi cha Magufuli mambo yalikuwa yanaenda.

Wapo wastaafu wana zaidi ya mwaka sasa na hawajui watalipwa lini.
 
Tukiri tu japo tumesema sana ila kipindi cha Magufuli mambo yalikuwa yanaenda.

Wapo wastaafu wana zaidi ya mwaka sasa na hawajui watalipwa lini.
Kwa sasa wanakwambia walikuwa wanasubiri mshahara wa mwisho uwasilishwe na serikali maana ungepunjwa pesa zako baada ya hapo pokea maumivu hamna kitu. Samia na waziri wake wana siri kubwa
 
Tukiri tu japo tumesema sana ila kipindi cha Magufuli mambo yalikuwa yanaenda.

Wapo wastaafu wana zaidi ya mwaka sasa na hawajui watalipwa lini.
Yalikuwa yanaenda poa sana ila tulikuwa tunampigia toka kona zote za nchi kutokana na kuwa kwake msukuma maana msukuma ni mtani wa kila kona. Kila mtu alimwita ngosha na kuzodoa mipango yake huku moyoni akikiri kuwa ngosha anachapa kazi.
Alipofeli ni kushindwa kudhibiti mauaji na utekaji, kununua ndege badala kuweka pesa hiyo kwenye ujenzi wa reli au bwawa la Nyerere ambayo yangewagusa watu wengi kuliko ndege kwa wakati huo/sasa
 
Tukiri tu japo tumesema sana ila kipindi cha Magufuli mambo yalikuwa yanaenda.

Wapo wastaafu wana zaidi ya mwaka sasa na hawajui watalipwa lini.

Huyo magufuli ndio aliofilisi hiyo mifuko au unajifanya hujui
 
Kwa sasa wanakwambia walikuwa wanasubiri mshahara wa mwisho uwasilishwe na serikali maana ungepunjwa pesa zako baada ya hapo pokea maumivu hamna kitu. Samia na waziri wake wana siri kubwa
Muache mama ashuti muvi kwanza ya kiwango cha hollywood.
Atajibu akitoka lokeshen.
 
PSSSF mtawalaumu bure
Kwa mfano; Pesa akichukua Serikali Kuu kosa lao ni nini?.,

nadhani ni sahihi kuelekeza suala la ukwasi wa Taasisi kwa Waziri husika labda.,au kwa Waziri wa Tozo😅
 
Tukiri tu japo tumesema sana ila kipindi cha Magufuli mambo yalikuwa yanaenda.

Wapo wastaafu wana zaidi ya mwaka sasa na hawajui watalipwa lini.
sio kweli mama mambo ni yaleyale pale PSSSF
 
Back
Top Bottom