Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com anayetambulika kwa jina la Mkumbwa Jr kulalamikia huduma ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) upande wa Dodoma kuwa siyo nzuri, mamlaka hiyo imetoa taarifa ya ufafanuzi.
Kusoma hoja ya Mdau bofya hapa ~ PSSSF Dodoma tofautisheni msaada na Haki ya Mtu
UFAFANUZI KUHUSU MALALAMIΚΟ YA MTU AMBAYE HATUJAMTHIBITISHA KAMA MWANACHAMA WA PSSSF
Januari 31, 2025
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umebaini mjadala unaoendelea kwenye jukwaa la Jamii Forums kuhusu utendaji wa PSSSF, ambapo mtu anayejitambulisha kwa jina la Mkumbwa Jr ameonyesha kutoridhika na huduma zetu.
Kwanza, tunatoa pole kwa Mkumbwa Jr. iwapo kweli alipata changamoto yoyote alipotafuta huduma katika ofisi zetu. PSSSF inajitahidi kila siku kutoa huduma bora na kwa wakati, kwa kuwa tupo kwa ajili ya wanachama wetu.
Hata hivyo, hadi sasa, hatujapokea rasmi malalamiko yanayofanana na yale yaliyoelezwa na Mkumbwa Jr. Zaidi ya hayo, kutokana na kutotumia majina yake halisi, tumeshindwa kuthibitisha uanachama wake au kufuatilia suala lake kwa usahihi.
Tunamkaribisha Mkumbwa Jr. au mtu yeyote mwenye malalamiko kufika katika ofisi zetu au kuwasiliana nasi kupitia namba 0800 110 040 (bure) ili atupatie taarifa muhimu kama namba ya uanachama, zitakazotuwezesha kufuatilia na kutatua tatizo lake haraka.
Pia, tunapenda kuwakumbusha wanachama wetu kuwa tangu Agosti 2024, PSSSF imehamasisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika uwasilishaji wa madai na upatikanaji wa huduma.
Tunaamini kuwa mwanachama yeyote anayeweza kushiriki kwenye majukwaa ya mtandaoni pia anaweza kunufaika na huduma zetu za kidijitali kwa urahisi. Kwa maelezo zaidi, tafadhali piga 0800 110 040 bila malipo.
PSSSF inaendelea kujitahidi kutoa huduma bora za hifadhi ya jamii kwa wanachama wetu na Watanzania kwa ujumla, tukiwa waaminifu kwa maadili yetu ya kumjali mteja, uaminifu, weledi na uwazi.
Yessaya Mwakifulefule
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma.