Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Wanabodi,
Kwa kuanzia naileta tuu kwanza hii hoja hapa, ikipata watu wa kutosha, tutaomba kwa mode, ifunguliwe jukwaa lake, tutalitafutia jina muafaka, "Mambo ya Powers"
Ulivyomtaja tu Mungu mara Yesu mara Roho Mtakatifu ndani ya hoja yako ikabidi niipime Hoja zako kwa Kutumia Maandiko matakatifu kwa sisi wakristo tunaita Biblia!,kuna uongo mwingi sana umeandika kumuhusu Mungu hata sijui chanzo cha huu uongo wako umetoa wapi! hapa chini ni baadhi ya maeneo uliyodanganya baada ya kulinganisha na biblia.

1."MUNGU NI NGUVU"-Huu ni uongo biblia haisemi Mungu ni Nguvu hakuna mahala katika biblia panasema Mungu ni nguvu ndani ya Biblia imeandikwa Mungu ni ROHO!(Yohana 4:24)
2."Chochote mtu atakachokiona kuhusu Mungu iwe ni kupitia Roho Mtakatifu au kupitia Malaika wake, it's just the manifestation of God's power" -Uongo,ndani ya biblia kuna watu wamemuona Mungu FACE to FACE! na sio manifastation ya Nguvu zake(Mwanzo 32:30,Isaya 6:1,)
3.
4.

naweza weka hadi namba 100 za maeneo uliyodanganya watu,wacha niishie hapo,ila Hoja yako ingependeza sana kama usingehusisha Dini ya aina yoyote ile bila kutumia hayo majina ya Mungu,Yesu na Roho mtakatifu ingekuwa ya kusisimua sana na ya kusadikika ila once ulipoanza kuhusisha imani za watu hasa sisi wakristo sijui na nguvu za kuzaliwa nazo sijui kutumia jina la yesu na mauchafu ya aina hiyo unatukosea sisi tunaoamini Biblia na mafundisho yake
weka hoja yako katika namna ambayo hutahusisha misingi ya dini zingine bila ku misquote maandiko ya dini husika
 
Kwa vile reference yak ya Mungu ni The Holly Bible only, please end off there, Mungu ni zaidi ya Bible!, Mungu ni Omnipotent, Omnipresence, na Omniscience. Mtu asikudanganye, hakuna kiumbe chochote kimemuona Mungu face to face!, God is Power, kinachoonekana ni powers too za Mungu.
Kwa vile huu sio mjadala wa dini, nakuomba endelea kuamini kile tuu unachokijua wewe, na kila usichokijua, be free kukiita ni Uongo, maana hata kwenye Bible ya mwanzo, ile dunia iliyoumbwa na Mungu, ilielezwa ni umbo la ubapa, Galileo Galilei aliposema dunia ni duara, alihukumiwa kifo kwa kumkashifu Mungu, na kweli aliuwawa, ndipo baadae sana ukweli ukabainika dunia ni duara.

P
 
Hivi ukiamka siku ukawa unaona kila unachokifanya siku hiyo kama sio kigeni(yaani ni kama hiyo siku ulishaishi huko nyuma japo huna kumbukumbu) hiyo ni nini mkuu? Hii nayo ni precognition?!
Hapana, hiyo inatwa dejavu, ni glimpses za life before life na life after life. Precognition ni uwezo wa kutambua jambo kabla halijatokea.
P
 
Onyesha kwa matendo kuwa unajua, Kama anakupenda kweli, ataacha.
P
 
Uko wrong again! reference zoote za Kimungu unazipata kwenye maneno yake mwenyewe na sio kwingine kokote thats why nili-refer biblia,Ni kweli kabisa Mungu ni zaidi ya biblia na huwezi kumjua katika ukubwa wake just kwa kuisoma bibilia, Guess what?! naye alilijua hilo so akatufunulia mambo yakututosha tu sisi wanadamu kwa uwezo wetu wa kibinadamu yaliyofichwa Ni ya Mungu (Kumbukumbu 29:29)! sasa wewe ni nani unakuja na vitu vipya? yaani tukuamini wewe bwana Paschal Mayala na hivyo vijitabu vya kishirikina ulivyounga unga hapo tuache kuamini maneno ya Mungu mwenyewe??,ulichoandika wewe ni ushirikina tu kwa lugha ya kiingereza kama tukitafasiri kwa kiswahili fasaha,mtu anayekuwa possessed na mashetani,majini ndio anakuwa na hizo nguvu,watu wa aina hiyo hata kwetu kule Tukuyu wapo wanaitwa Manyafu ni wachawi tu akiangalia maziwa kwa hisia kali yanaganda sasa kwa kiingereza ndio umeita Psychic Power 😀😀😀,sijui ana nguvu za kuzaliwa sijui vile usidanganyike na vitabu vya falsafa mzee!
Kwa hiyo huo mfano wako wa Galileo unamaanisha Biblia imedanganya?? usi qoute biblia ki Falsafa biblia ina tafsiri zake ndiomaana huelewi,ndani ya biblia kuna viumbe wengi tu ambao ni binadamu wamemuona Mungu FACE TO FACE nimekupa maaandiko bado HUTAKI!
Narudia tena Hoja yako ni nzuri sana kama ukitoa hizo reference zako za Mungu,Yesu na Roho mtakatifu ila ukihusisha hivyo vitu vitatu Hoja yako yooote inakuwa FLAWED unahusisha vitu viwili ambavyo vinapingana unataka kutuaminisha kuwa ni kitu kimoja! na hayo mafundisho yanapendwa sana na mashetani Fremasonry na wengine wa aina hizo,Eti unaweza kuwa yoyote yule ukiamua!,sijui unaweza ku unlock nguvu zilizopo ndani yako! .Hakuna cha nguvu mwilini mwako Piga kazi na Omba uzima tu hayo mafundisho yako unatudanganya
 
Pathetic liar...haya endelea kua maskini
 
Mkuu Makoshi, Mungu aliumba mwanadamu kwa mfano wake kwa kufinyanga udongo uliofanya physical body ambayo ni mavumbi na mavumbini utarudi. Kisha akaupulizia huo mbili wa udongo pumzi ya uhai, life force, mwili ukapata uhai, roho, hii roho ni Gods spirit, ina nguvu za Uungu ndani yake, it is eternal na haifi.

Mtu anapokufa, kinachokufa ni ule mwili tuu nyama ambao unazikwa unaoza na kurudi mavumbini. Kufa ni kitendo cha roho kuacha mwili, kukata roho, kwa vile roho haifi inaendelea kuishi kwenye ulimwengu wa roho.

Hii roho kwa vile ina nguvu za Uungu ndani yake, it is responsible for everything in life. Wale wahubiri wanaoponya kwa miujiza, wanachofanya ni opening up powers doors zako na kinachokuponya ni your own powers zilizomo ndani yako ambazo kila binadamu amepewa ile siku ameumbwa.

Ile siku ya mwisho ya ufufuko wa miili na uzima wa milele, kinachofufuliwa sio ile miili ya mavumbini bali the spiritual bodies zenye eternal life.

Kwenye mambo ya spiritualism, Christianity ni dini ya juzi tuu, Hinduism, na Buddhism (Eastern Sciences), zilitangulia sana ndio maana they believe in life after life na life before life yakiwemo mambo ya reincarnation, hivyo ukijilimit kwenye The Holy Bible alone or Quran Tukufu, you will miss the point ya bandiko hili.

Toka mwanzo nimesisitiza read this thread with open mind but stick to what you believe.

Ni kweli kwenye reference nimeweka sacred writings za kila kitu ukiwemo kila aina za uchawi for information purposes na elightghment na nikasisitiza ukimjua Mungu, shetani hawezi kukudanganya, na nikasema humu shetani ndio the second being mwenye powers next to God, everything God can do, satan can do, except creation Hivyo God is the Creator and devil is the destroyer. Satan, the devil is the best impostor and most of the times he disguised himself as God, hivyo kuna dini nyingi sana humu duniani wanajidhania wanamwabudu Mungu Baba, kumbe actually wanamwabudu shetani bila wao kujijua, hata Bwana wetu Yesu Kristo alituhusia " sio wote wanaoita Bwana Bwana ni wangu, watakuja watu watafanya ishara na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu", alipoulizwa utawatambuaje, Yesu alijibu " Utawatambua kwa matendo yao".

Hivyo nakuomba sana usiite watu humu ni wakongo, unless you're very sure wewe unajitambua umesimama wapi usijekujikuta utamtumikia shetani ukiamini ni Mungu.
P
 
Hapa ndio tunatofautiana Kaka Mayala "How did you come to the above conclusion Brother'?? hakuna dini ndani ya bible inaitwa christianity ni watu tu waliamua kusema kuna hiyo dini inaitwa christianity hata ndani ya biblia Mungu hajasema tuwe wakristo tangia enzi za akina Mussa imeandikwa tuwe WATAKATIFU thats all so unapolinganisha the so called christianity na hizo aina zingine za dini ndio unapata other sources za kufanya reference sababu umesema zilikuwepo kabla kwa tafasiri kuwa ukristo ulianza baada ya Yesu,ila hukujiuliza akina Adam,Henoko na Mussa walikuwa dini gani na kama kulikuwa na dini nyingine kabla yao
Kurahisisha tu kama umeamua kuchanganya haya maswala ya kiroho na dini/elimu mbalimbali hata kama zinapingana am out,ila kwa sisi tunaofuata maandiko matakatifu tupo limited kwenye kitabu kimoja tu na si vingine sababu kimejitosheleza
 
Amani iwe nawe.
P.
 
Kama Yaaani kama mm u kifungua mm mwana chama wako
 
hapo naona umeeleweka asee
 
Kaka nnazo baadhi ya hizo power nafanya kuzikataa kwanguvu kupitia imani yangu ila waganga,wachawi, na viongozi wa dini wameniambia na hua wanataka kushirikiana na mimi ila binafsi sina muda nao.....and they told me i could be great and famous person duniani but i don't care i don't know why!
But i i had mate with mysterious being usiku kwenye uwanja wa mpira akaniambia nimshikilie Yesu nisimuache at that time niko meditation na mbinguni while am walking.
Sijasomea haya mambo ila yapo ndani yangu sema sioni umuhimu wake... Iabda unisaidie
 
Sawa kabisa na wakati ukimshikikia Yesu Angelia na hizo picha zitasaidia kubadili au kuongeza nguvu kwenye Imani yako
 

Attachments

  • 74410773-1B18-43B5-B533-9B3377C4EA9A.png
    145.2 KB · Views: 39
  • B169CCF7-A80C-43D8-B21D-0F22A3A1AB7C.png
    264.2 KB · Views: 38
  • AC4CF2AE-9F32-49B2-80B7-E23CA21F1412.png
    162 KB · Views: 39
  • 334E8F9E-8B6A-4884-AC2C-66CABE1529EB.png
    145.6 KB · Views: 37
Jam Jamani duniani kuna mambo , ngoja na mm nianze na kufungua jicho la 3 then kutoka nje mwili
 
ASANTE
Nami ni abilia wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…