Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
-
- #461
Mkuu Nsalu, hiyo ni kawaida tuu ya mtu kujihisi umemsemesha, kuna wakati unawea kabisa kusikia mtu amekuita kwa jina, huku hakuna mtu.Kaka Pasco, mimi naweza nikawa nimekaa kwenye daladala au tu nimekaa na mtu pembeni yangu nikawa nawaza mambo yangu kimoyo moyo lakini utaona mtu anageuka ananiuliza unasemaje? na wakati sijamsemesha mi nawaza mambo yangu tu. Na huwa inanitokea mara nyingi tu. Sasa hiyo nayo ni nini hebu nifafanule.
kiukweli mkuu mm naungana na ww ila nakupingana na ww pia .
ujue hapa nimesoma coment za wadau hasa mkuu Pasco kiukweli mwenyewe kasema kuwa kuna mambo ya kimungu na kishetani na hizi power huwa zinapotea sana hasa kwakufanya mabaya na kila mtu huwa anazaliwa nazo sasa jinsi anapokuwa ndio huwa zinapotea sasa hapa ndio kwenye main point ukiangalia sana mtoto mchanga huwa anakuwa hana dhambi na hatendi dhambi sasa anapokoa shida ndipo huanza huanza kutenda mabaya na hasa machukio kwa mwenyezi mungu na ndipo nguvu hupotea na kama umesoma soma bible kuna sehem kunamistari inasema kama tungekuwa na imani japo hata kiduchu tuu kama punje ya mchanga (hadarani) hakika tungeweza omba moto toka mbinguni na ungeshuka.
ila sasa binadam asilimia 99 hatuna imani na mambo ya kumpendeza mungu ndio maana tunaangukia kwenye mikono ya shetani na wafuasi wake ndio maana hizi nguvu zinakuwa za kishetani lkn kama tungekuwa wacha mungu basi tungekuwa na nguvu za kimungu.
Mkuu Amri kuu ni Upendo, kuna vitu havijaandikwa popote kuhusu source of power za Mungu au za Shetani!.
Hii n i tafsiri yangu binafsi.
Kwa maana hiyo vita vyote vya Mungu na shetani, vyote vinapigwana ndani yetu, Mungu is always there ila anayewakaribisha watu wake ni wewe kwa sababu Mungu yuko ndani yetu!. Na shetani pia yupo!, anayewakaribisha watu wake ni wewe mwenyewe!. Ukiwa imara katika Mungu, shetani hawezi kufanya kitu, hata wakuloge, hulogeki hata wakutupia majini, mapepom mashetani, hayawezi kukuingia!. Anayamkaribisha Shetani ni wewe, na anayemfukuza pia ni wewe regardless unatumia jina la nani!.
- Wengi wanadhani kuwa Mungu ndio aliumba vitu vyote!, sii kweli, Mungu hakuumba vitu vyote!, bali ameumba dunia na vyote vilivyomo. Nje ya dunia, sio vyote!. Shetani yuko nje ya dunia!.
- Mwanzo wa Mungu, pia ndio huo huo mwanzo wa shetani!. Alikuwa ni 2nd in command akiwa 2nd with powers, mpaka leo mpaka kesho shetani ameondolewa tuu ile position ya 2nd in command but not his powers!.
- Mungu ni omnipotent na omnipresent, so does shetani!. Hivyo kwa vile Mungu ni power za mwanga (light) ukiwa nazo unaitwa "enlightened", na shetani pia ni power!, nguvu zake ni za giza "powers of darknes" kwa vile Mungu yupo ndani yetu, vivyo hivyo shetani yupo ndani yetu!. Ukitenda mema, ndio unatumia nguvu za Mungu, ukitenda maovu unatumia nguvu za shetani!.
- Mungu ana watumishi wake, mwanaye Yesu Kristo, Malaika na Roho Mtakatifu ambavyo vyote pia ni powers na ukitenda mema, huwakarinisha ndani yetu. Shetani pia anakundi lake la malaika wabaya, mapepo, majini, maruhani, liroho!.
- Ukimtumiakia Shetani, wenyeji wa mwili wako wanakuwa ni watumishi wa shetani, ndipo unaposikia fulani ana mashetani, majini, anatumia nguvu za giza!, wale watumishi wa Mungu, wanakukimbia!. Ukitumia nguvu za Mungu, watumishi wa shetani wanakumbia, na ndio hao mapepo wanaotolewa!. Kinachotolewa kwako ni watumishi tuu wa shetani au watumishi wa Mungu, sio Mungu mwenyewe wala sio shetani mwenyewe!.
Pasco.
Mimi ni mwananchi tuu!, wananchi tunawadanganya viongozi?!, ila kama unazungumzia lile "jiwe walilolikatta waashi!", subiria kwanza mpaka litakapofanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!", ndipo tuje tuulizane!.
Ili kiongozi uwe kiongozi bora, unapaswa kuwa na "powers from within!". Tanzania tunaviongozi wachache sana wenye "powers from within", Nyerere alikuwa na powers!, Sokoine alikuwa na powers!, sorry kuhusu Mwinyi, Mkapa kidogo kwa kuforce, aliyepo ni nil!, ajaye ni very powerful!.
Pasco.
Mzizi Mkavu
Tupia nyota ya 13 january
| [TABLE="class: ecxyiv1610786350contentpaneopen"] [TR] [TD="colspan: 2"] NYOTA YA MBUZI (CAPRICON)
KIPAJI CHA MBUZI(GRADUAL) Wenye nyota hii wana kipaji cha kuchambua mambo kidogo kidogo au kufuatilia kitu bila watu kujua na kupata ufumbuzi wa uhakika mwishoni. TABIA ZA MBUZI Wale wote waliozaliwa katika nyota hii ni watu ambao wanapenda kuwajibika, ni wenye bidii ya kazi, katika kazi yeyote watakayofanya hata kama ikiwa ni ya kipuuzi. Ni viumbe waaminifu sana na ni watu wastahamilivu na wenye kuweza kuvumilia matatizo yeyote. Kwa upande mwingine ni watu wenye tamaa kubwa ya kimaisha na kimaendeleo, na kwa sababu ya kutekeleza malengo yao basi huwa wanakuwa wabinafsi na wenye uroho na uchu. TABIA YA MBUZI KATIKA MAPENZI Watu wenye nyota hii wanakuwa ni watu wenye aibu sana kwa wapenzi wao lakini aibu ikishawaondoka huwa ni wapenzi wa kutisha, kwa maana ya kwamba kwa vile wao ni waaminifu wanataka wapenzi wao wawaunge mkono katika hisia zao za kimapenzi. Ni watu wanaoogopa sana kuachwa na wapenzi wao hivyo basi huwa wanakuwa waangalifu sana katika kuchagua wapenzi. Jambo jingine ni kuwa huwa wao wenyewe hawajiamini kimapenzi, mara nyingi wanashindwa kuingia katika mapenzi kwa woga tu hivyo kukosa nafasi nzuri ya kupendwa. Kwa ujumla ni wapenzi makini na huwa hawaoi mpaka wapate uhakika wa kutosha kutoka kwa wapenzi wao. Ni wapenzi makini, waaminifu na wanaoweza kuaminiwa. Lengo lao katika mapenzi ni usalama. TABIA YA MBUZI KATIKA FEDHA Kwa watu wenye nyota hii fedha ni kitu muhimu sana katika maisha. Watu wa Mbuzi wanaamini kabisa kwamba fedha ndio zitawapa uwezo wa kuweza kupambana au kukabiliana na mazingira ya Dunia, hivyo basi suala lolote la fedha na mali wanalichukulia kwa uzito mkubwa sana. Inawachukua muda mrefu kutekeleza malengo yao ya kifedha lakini wakishazipata basi huwa hawatetereki tena. Wana uwezo wa kuhifadhi walichonacho. Ni watu wabahili sana na hata kama wakiwa na fedha nyingi utaona wanaishi maisha ya kawaida na wala huwezi kuwajua. Fedha zao zinatoka kwa sababu maalum ya dharura na wala siyo katika starehe au vinginevyo na hiyo ni kwa sababu hupenda kukumbuka walikotoka katika hali ya umasikini au ufukara. {mospagebreak} MAVAZI YA MBUZI Wenye nyota ya Mbuzi wanatakiwa wavae nguo za mitindo, zilizoshonwa kwa ustadi. Nguo hizo ziwe za rangi ya kijivu au Kijani iliyoiva au hudhurungi nzito. Kitambaa kiwe cha kitani (Linen) au cha ngozi. Nguo ziwe ni suti na ziambatane na saa za mikononi. MATATIZO YA KIAFYA Nyota hii inatawala Mifupa, Magoti na Ngozi. Matatizo yao makubwa ya kiafya huwa yanasababishwa na muda mrefu ambao wanafanya kazi au kujishughulisha. Hii ni kwa sababu hawamwamini mtu mwingine afanye shughuli zao ambazo zina mipangilio ya muda mrefu, nguvu nyingi, na akili hutumika. Shughuli zao nyingi za mizunguko na kufikiria huwaletea maradhi kama Baridi Yabisi (rheumatism). Maradhi yao mengine makubwa ni ugonjwa wa ngozi, matatizo ya Magoti na maradhi ya mifupa. KAZI ZA MBUZI Wenye nyota ya Mbuzi kitu muhimu katika maisha yao ni kazi na maisha mazuri na yanayoeleweka ambayo yako katika mpangilio wanaoutaka wao. Ni watu ambao wanazingatia sana muda wa maisha na wana mpangilio maalum kwamba katika umri fulani awe amepata nini au awe na fedha kiasi gani. Ni wenye kupenda utekelezaji wa kazi wa hali ya juu na wao wanapoagizwa hufanya hivyo. Kazi zao zinazowafaa ni zile za kutumia akili, Uhandisi, Usanifu Majengo, Saveya, kazi za Serikali, Siasa na Daktari wa Meno. FAMILIA ZA MBUZI Wazazi wenye nyota ya Mbuzi ni watu ambao wamepangilia kabisa mipango ya watoto wao kabla hawajazaa. Ni wazazi ambao wanayachukulia kwa uzito mkubwa majukumu yao ya kulea na hawakubali kabisa watoto wao kufanya michezo michezo ya kipuuzi. Wanapenda kuwahimiza watoto wao kuwa na malengo ya maana. Wanapenda sana nidhamu katika familia zao. Mara nyingi wazazi wa kiume huwa hawapati muda kuwa na watoto wao kutokana na kazi nyingi walizonazo lakini kwa wazazi wa kike wanakuwa wanatumia akili ya hali ya juu katika kutatua matatizo au hisia za watoto wao. MADINI YA MBUZI Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinayoitwa Black Jet. Jiwe hili inaaminiwa lina uwezo wa kuongeza ujasiri na kumletea mvaaji mafanikio ya kibishara. UHUSIANO WA KIMAPENZI (MBUZI NA KAA) Tabia ya Mbuzi ya ubahili na kutopenda anasa hulainishwa na tabia ya Kaa ya upendo, mapenzi na huruma. VYAKULA VYA MBUZI Wenye nyota ya Mbuzi wanashauriwa wapende kula vyakula au matunda yafuatayo. Ambayo ndio yanatawaliwa na nyota yao. Wapende sana vyakula vya Nazi na Nyama yeyote. Vile vile wapendelee kula Viazi Vitamu na Samaki Gamba (Shellfish). NCHI ZA MBUZI Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa watu wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee miji au nchi zifuatazo ambayo inatawaliwa na nyota ya Mbuzi. Miji hiyo ni Brussels (Ubelgiji) na Oxford (Uingereza) au nchi za Mexico na India. RANGI ZA MBUZI Wenye nyota hii wanashauriwa wapake rangi zifuatazo kwenye nyumba zao, rangi ya Kahawia (Brown) Rangi ya Kijivu (Grey) au Nyeusi |
We live with the Super Power within !!Tufanye mtu kwa mfano wetu!!!There are things in life that are very difficult to explain....
Nyota ya 9/11
Ndugu MpiganiaUhuru naomba unijibu haya maswali yangu mawili la kwanza hili
(1)Unapouacha mwili wako huwa unaenda wapi na unatumia mwili upi tofauti na huo uliouacha hapo ulipokuwepo kabla ya kujinyofoa ndani ya huo mwili.
(2)unapouacha barabarani watu wanauona au hauonekani na magari yakipita hayaugongi huo mwili?
Habari Roby2006,
Sorry, sijatembelea JF kwa muda sasa, Nikujibu maswali yako kama ifuatavyo:
1. Baada ya kuuacha mwili wangu situmii mwili wowote kufanya actions, ni kama unavyoota ndoto kuwa upo sehemu fulani unafanya jambo fulani (mwili wako wakati huo unakuwa umeuacha kitandani) tofauti hapa ni kuwa ukiwa kwenye ndoto huwezi fanya action yoyote ikaonekana lakini hapa unaweza fanya kitu na kikaonekana kwa kutumia spiritual power! (nguvu za kifikra / kiroho)
2. Ninapouacha barabarani watu wanauona na wanajua kuwa ni mimi niliyekamilika (kwa wale wanaonifahamu), mwili ni ule wa kawaida hivyo unaweza fanywa lolote (baya au zuri) inatakiwa umaakini wa hali ya juu ili usijezurika, pia yapo mawasiliano kati ya mwili wangu na roho yangu hivyo kukiwa na hali ya hatari utashtuka na kurudi haraka, haijalishi upo wapi kwa wakati huo, lakini tahadhari pia ni muhimu, huwezi ukauacha popote tu, ni hatari sana na ndio maana sipendi ku-practice suala hili mara kwa mara!
Ahsante!
Haya ndio matatizo ya kuangalia horror movies kwa wingi!
Matokeo yake unajiona na wewe unaweza kufanya kama hao actors!
Teh teh teh teh.
Mkuu hizo movies ni fake SIO KWELI!
Wasio amini mungu hawawezi kuwa right katika chochote? Na unapokubaliana au kutofautiana nao, unakubaliana au kutofautiana nao kwa sababu ya jambo au kwa sababu hawaamini mungu?
Asiyeamini mungu akikukuta mathalani umepigwa mapanga na majambazi (wanaoamini mungu na kuomba dua kabla ya kukuchabanga mapanga by the way) na akataka kukusaidia, utakataa kwa sababu tu haamini mungu?
Utamuuliza mtu "wewe unaamini mungu au huamini?"
Kwa nini unaendekeza "ad hominem" attacks zinazoangalia mtu badala ya masuala?
labda hukunielewa
my point ilukuwa yeye kama 'muumini'
hawezi pick vitu fulani vya kuviamini na vingine akaamua haviamini
halafu bado still ajiite 'muamini mungu yupo'
wakati imani inamtaka aamini kila kitu na sio kuchagua....