Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Kuna mengi ya kufanya lakini nakupa basics kwanza ukifaulu hii hatua ya kwanza nijulishe

Hapo ulipo tafuta Sehemu kimya na utulivu kwa kwenye kiti au jamvi usikunje mgongo weka mikono mapajani kwa kurelax au lala chali kwa kulerax fumba macho halafu anza kuhesabu pumzi

Ili inhale hesabu moja uki exhale mbili endelea na mchakato huo, utaona utakapoanza tu kuhesabu yatakuja mambo kibao utakumbuka mambo ya jana, mipango ya kesho changamoto zako yaani matukio yatakuja kama mkanda wa sinema

Unachotakiwa kufanya ni kustick kwenye pumzi tu, hayo matukio yanayopita ndio takataka zilizojaa kwenye bongo yako


Pia kuna kitu kinaitwa empty meditation: hii unakaa kwakurelax na kuangalia ukuta tu usifikirie chochote zaidi ya kuuangalia huo ukuta, utajikuta huoni ukuta bali unaona mawazoni yako, chanamoto zako mipango yako madeni yako nk nk nk
aya yote ndio takataka zilizojaa kwenye ubongo, Kwahiyo zinacompress mind na kuifanya ishindwe kufanya kazi sawasawa


Unachotakiwa kufanya uwapo kwenye breathing au empty meditation ni kufocus tu kwenye kile ukifanyacho kwa Wakati huo kila kinachojaribu kuja kwenye mind unakifukuza na kurudi kwenye concentration yako ni kazi ngumu mno kutaka kuistation mind kwenye kitu kimoja kwa Wakati mmoja but with serious practice utaona mabadiliko. ...ukiiweza hatua hii ya kwanza nijulishe tuendelee

Mkuu mshana naomba uendelee na hatua ya pili. or ikiwa uliendelea niambie tu ni post no. ngapi.
 
Nakubaliana kabisa na wewe Mkuu Pasco, kipindi fulani katika maisha yangu nilitamani sana kujifunza uchawi mwenye tija, nikajikuta nimeangukia kwenye temple moja south Africa iliyokuwa inafundisha Buddhism Yoga meditation na supernatural powers

Yalikuwa ni masomo magumu ya ajabu na yenye kushangaza kwa jinsi yake, kwa ufupi ni kwamba hakuna chenye nguvu duniani kama bongo(mind) ya binadamu, na tunachokitumia katika mind zetu ni theluthi tu ya kile chote kilichopo

Tunafundishwa kuwa kuna 5senses, lakini Zipo 8 ambapo mtu ukiweza kuzifanyia kazi utafanya maajabu mengi , mind ya mwanadamu imejazwa takataka nyingi mno, illusions na dillusions ukiweza kuziondoa kwenye bongo yako ukabaki na pure and stable mind unakuwa mtu mwingine kabisa mwenye maono na nguvu za ajabu mno

Medition ni kitu cha Mwanzo kabisa kuendea kwenye kudevelop supernatural powers, nilifanya meditation zote, chanting, yoga nikiwa vegitarian kwa miaka mitano nikajikuta nabadilika nikaogopa nikaacha , kwakuwa niliona wazimu kuna mafundisho yanapingana waziwazi na imani yangu

Nimeipenda mada yako sana. Nakaribisha maswali na ufafanuzi nimeisoma sana Buddhism, Taiosm, Satanism na Kshna consciousness

Mwenye kupenda hii mambo atafute kitabu kiitwacho Analects: Way and Its Power.

Hicho kitabu ntakipataje au ni maduka gani yanakiuza
 
Asante sana Pasco kwa mada hii.Hili ni jambo ambalo limenitatiza kwa muda mrefu na nimekua nikitamani nifungulie nguvu hizi lakini bado sijafika huko.Nimesoma sana kuhusu haya mambo na ninashukuru kupata kitabu cha The Master Key hiki ndicho kilichonitambulisha kwenye ulimwengu huu.

Ninaendelea kujisomea kila siku na sasa nimejikita kwenye maandiko ya Tibet hssa hasa mafundisho ya Atisha.Ninatumaini nitagika huko ninakokutazamia kwa maana yote haya ni nguvu ya Mind.

Mkuu habari yako.nakuomba namie msaada wa huo kitabu
 
Mkuu Slow, Mungu alipomuumba Adam, alimpa uwezo!. Yesu alipokuja alifanya miujiza, na kila muujiza alisema "imani yako ndiyo imekuponya!", kasome Marko 10 : 52 - Yesu akamwambia, \"Nenda, imani yako imekuponya, na Mathayo 9:22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu;imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile, au [h=3]Luka 17:19 "[/h]Akamwambia, ``Inuka, uende; imani yako imekuponya..hiyo imani yako ndio "powers from within!". Akasema laiti watu wangekuwa na imani kama punje ya haradali, wangeiambia milima ondoka!, na milima ikahama!", ina maana hizi imani tunazotumia ni ndogo tuu kama mbegu ya mchicha!.

Shetani pia ana powers, ikumbuke hapo mwanzo shetani ndiye aliyekuwa malaika mkuu, alipoasi, alifukuzwa ila hakunyang'anwa zile powers, ndiye aliyemrubuni Eva kule lile "tunda!". Nguvu za shetani hufanya maovu, nazo pia zimo ndani yetu kama hizo nguvu za Mungu!.

Kitendo cha kuamini, ni kufungua tuu milango. Mimi ni Mkristu Mkatoliki, kwa sababu nimezaliwa huku. Wengi hufuata imani fulani kwa kujikuta ndiko walikozaliwa na wanaendelea kujifungia humo humo kwa kuto look beyond!. Nilipokuwa India, nikasoma kidogo imani za Hindu ndipo nikagundua kumbe Christianity ni dini ya juzu juzi tuu, kwa taarifa tuu, dini za kale zaidi ni shamanism na animism, ambazo zilikuwepo miaka 300,000 kabla ya Kristu ila baadae zilifutika!. Kwa sasa dini ya kale zaidi iliyopo ni Hinduism ikifuatiwa na Buddhism zote za India ndipo ikaja Judaism ya Mashariki ya Kati, Israel, ikaja Taoism ya China na Shitoism ya Japan ndipo ikaja Christianity!. Hapo dini zetu za asili, hazitajiwi kabisa kwa sababu hazikuandikwa!.

Uki take time kutoka nje ya box la Ukristu au Uislamu ambamo ndiomo wengi wetu tumejifungia humo, ukachungulia ndani ya Hinduism au Buddhism, ndiko utakutana na real powers za "enlightenment!", kwa sababu dini hizi zinaamini kwenye "higher powers" bila kumtaja Mungu, Ukristu na Uislamu umezifungia milango, ili ukifuatilia uthabiti wa imani, discpline, na nguvu za kusali, utagundua sisi Wakristu na Waislamu tunatania tuu!.

Kiukweli ukizama sana kwenye hizi powers, unaweza kuingia kanisani na kujikuta unashutukia jinsi watu wanavyofungwa kamba, unaweza ukaacha kwenda!. Mimi bado ni Mkatoliki Die hard japo kuna mambo tunafanya ndivyo sivyo, ukishayangundua, unaachana nayo, bali unaendelea kuenenda kanisani kwa kufuata mafundisho ya Biblia na sio lazima yale yote ya kanisa ambayo umeisha yastukia kuwa sio!.

Wengi wakistuka, huamia makanisa ya wakovu, huko pia huwa nina hudhuria Mama yangu ni Esemblies og God, huko nako ndiko sio tuu unakuta kamba nene, bali watu wanapurushwa na kukamuliwa mpaka wanabaki mifupa!. Wale Wachungaji wameishajistukia jinsi ya kutumia hizi powers kucontrol waumini wao!. Wale wanaopataga mwanga hustuka na kujihamia kimya kimya, wengine wenye imani upofu, ni watumwa wa Wachungaji wao na wachungaji hao huwafanya lolote ikiwemo kuwa nani hii wake zao!, wao wakijua ndio baraka zenyewe kumhudumia mtumishi wa Mungu!.

Bwana wetu Yesu Krisu alisema wazi, watakuja watu, watahubiri kwa jina langu, watafanya miujiza ya uponyaji na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sio wangu!. Ukifuatilia sana the working of powers, unaweza kuogopa kuendelea ku practice, ila ukiisoma vizuri Bibilia, utagundua mahali mengi pameandikwa "nguvu imo ndani yako"!. Mungu alituumba kwa mfano wake, na katupa nguvu ambazo ndizo hizo powers from "within".
Pasco.

Mkuu hapa umenigusa sana na ningependa tutafutane.
Ya ni kweli raia wengi dini zao wamezaliwa wakakuta wazazi wao wanaabudu nao wakaenenda ivyo ivyo bila kuangalia upande mwingine wa shilingi.

Mie ukoo wote ni waromani ila mie nimechepuka ni msabato na huko nako ni kukosoa wengine a kidogo nataka nihamie uislamu na laiti kama ningebahatika kuwa huko ningejifunza hizo dini z mashariki.

Yani nimeipenda lecture yako sana kaka .

Pia Yesu aliawambia kuwa ufalme wa mbinguni upo miongoni mwenu na hakuna hata siku moja mtu atakuja akuambie au apointi kuwa tazama ufalme ule pale kama vile mtu akuonyeshapo upinde wa mvua kuwa ule pale .ila powers hizo tunazo wenyewe.

Pia imeandikwa kuwa twaangamia mana kwa kutokuwa na maarifa na ikasisitizwa kuwa mshikeni sana elimu usimuache na hapa elimu ilikuwa ni ya mbingu ila wachungaji wanaipotosha kwa kudai kuwa ni elimu ya masomo ya darasani.

Mara nyingi sana kujifungia kwenye dini moja kunakudumaza sana na unashindwa kujifunza wengine wanajua nn.
Ila utakuwa ndani ya box na utaambulia na chuki inayopandikizwa kwa waumini kuwa hawa ni mashetani wanaabudio mara hawa ni makafiri au wanaabudu masanamu n.k.

Please msije mkaleta malumbano ya dini jamano hapa tunabadilishana maarifa
 
Precognition, premonition and precognitive dreams - Perception of events before they happen.
Energy medicine
- Healing by channeling a form of energy.
Psychic surgery - Removal of diseased body tissue via an incision that heals immediately afterwards
Divination - Gaining insight into a situation via a ritual.[SUP][7]
[/SUP]Clairaudience - receiving messages in thought form from another frequency or realm. It is considered a form.

Baadhi ya waganga ni kweli wananguvu hizi, ila wengi zaidi ni wasanii, wameishajua the powers anazo mgojwa, anachofanya ni make belive kuwa kaoteshwa, anachokupa is nothing, wala hakitibu!, kinachotibu ni imani yako!, kama kikombe cha Babu!. Anayeponyesha sio mganga, bali mwili unajitibu na kujiponya kwa nguvu zako mwenyewe, anachofanya yeye ni kukusaidia tuu wewe kufungua milango ya nguvu zako kufanya mambo!.
Pasco.

Hata madaktari wanafundishwa kuwa imani ndo tiba ya kwanza na ndo mana huwa wanakupa imani sana au matumaini sana.
PIA KUNA MGONJWA ALIKUWA ANATIBIWA BILA YA KUPEWA DAWA SEMA WAKAWA WANA ACT KAMA ANAPEWA DAWA NA HATA SMT SINDANO HEWA ILA MWISHO WA SIKU HUYO MGONJWA AKAPONA.

SO KITU IMANI NDO KILA KITU NAMIE NAKUBALIANA NAWEWE KAAMA KWENDA MOTONI KISA NIMEUNGANA NAWE NGOJA NIENDE
 
Mbeky, hili la Steve Jobs na Buddhaism silijui, ila powers hazina dini!. Ya india nitayawekea thread yake infuture ili nikiwa Dheli nilikuwa napost threads humu jf, sema sizikumbuki.

Kiukweli sijawahi sikia miujiza yoyote ya Dalai Lama, ila hawa monks wa Tibet wana fly na kujigeuza invisible tatizo, hawasemi, wala hawaonyeshi!. Kinachofanya wanafly, wana uwezo wa kustop gravitational force kwenye miili yao hivyo wana float hewani!, ukiwaona utawaona kama wanatembea maana wanachapa miguu ukidhani wanakanyaka ardhi, kumbe wanakanyaka upepo, huko kutembea ni ili tuu watu wasijue kuwa they fly!.
Pasco.

Hii anti gravity nshawahi kuisoma before mkui
 
Mkuu Pasco kwanini kula kiapo cha kufanya usiri? Kuna nini nyuma yake? Kama ni kitu kizuri kwanini wadiweke wazi watu wengi wakafahamu na kutumia nguvu hizo kwa faida na ustawi wa mwanadamu???

Wote mkilingana hakuna dhana ya maisha kaka.

Mana wengi wataijua na kuitumia na kufanikiwa na mwisho wa siku wanataka wamani pulate na controll dunia ili iwasujudie kaka.ndo mana hata technology ni siri na inafichwaje .
 
Mkuu Yerusalemu, miili yetu ina sehemu kuu mbili, phisical body na spiritual body. Inaokufa ni physical body tuu, spiritual body haifi!.

Wakristu wakatoliki tumeaminisha ukifa, kama unakwenda kuzimu, au toharani kusubiri ile siku ya ufufuo wa miili na hukumu ya mwisho, ndipo uhukumiwe kwenda mbinguni au motoni!, kwa wale wa motoni ni moto wa milele, na wa mbinguni ni uzima wa milele!.

Wakristi wengine wanaamini ukifa unahukumiwa na kwenda mbinguni au motoni kwenye jehanum ya milele.

Waadventista Wasabato, pentecoste na Watch Tower wanaamini mbinguni na peponi ni hapa hapa duniani.

Hindu na buddha wanaamini kwenye life after life na life before life chini ya process ya reincarnation. Ukifa, mwili tuu ndio unakufa, spirit inahamia kwenye mzaliwa mwingine!. Ukitenda wema unazaliwa budha, krishna, ukitenda maovu unazaliwa mbwa, paka, punda etc!.

Kile anayekufa, anauona mwili wake na kila kinaendelea, akizikwa kwa heshima, astra body yake ina rest in peace!.

Ikitokea astra body ikakuta physical body haipo, then inageuka Ghosts au Wandering Spirits- ...
sambamba na wote wanaokufa untimely death, mfano za ajali, risasi au watu wanaokufa na miili haijapatikani, spirits zao zinabaki zikitanga tanga!, ndio hizo huitwa ghosts, na nyumba zao huitwa "Haunted Houses"
au Haunted Places!

Mfano ilipozama MV Bukoba, au Spice Islander, miili yote ambayo haikupatikana, spirts zao zinabaki zikiwa wondering spirtis!. mimi nikiwa biker, nilikuwa nasafiri kwenda popote saa yoyote. Wakati wa usiku, kuna maeneo nikipita, vinyweleo hunisimama!, basi mara moja hutambua hilo ni eneo lenye wondering spirits!. Hsawa maeneo yenye misitu mimine, au madaraja!, inamaanisha kuna watu waliuliwa, wakatupiwa humo bila kuzikwa!. Sometime hawa wondering spirits wanakuwa evil!, wana sababisha ajali za mara kwa mara!. Ni vile tuu, we don't keep record ya maeneo yanatokea ajali za mara kwa mara na sababu ni nini!.

Pasco

Wasabato imani yao ni sawa na waromani kuwa kuna ufufuo akija yesu afu twaenda kuishi milele mbinguni
 
Pasco,
Thanks! I wonder how do you know these things! Umesomea? Nitajaribu ku-exercise kama ulivyonishauri. In-fact mara nyingi nimekuwa na wazo la kuwa mimi ni mtu wa kipekee ingawa bado sijawa na uhakika wa upekee huo, labda sasa umeanza kunipa mwanga! Sasa nitaanza kujifunza na ku-practice ili nione exactly what I have inside me!

NB:
Nashukuru kwa kunipa jina la ile nguvu ya pili (second sight) kwa kongezea tu ni kuwa ninapowaona watu hao walio uchi ni kweli kuwa wenyewe hawaoni wala kusikia lakini ukifanya jambo (kwa vitendo au maneno) kuwahusu wao wanashtuka na ku-take action! Hilo nimelishuhudia mara kadhaa. Mfano kuna mmoja nilimwagia maji akashtuka, akageuka na kutokomea.
Mwingine aliingia chumbani kwetu (tukiwa watoto) kupitia kwenye ceiling board, nikapiga kelele kuwaambia wazazi kuwa kuna mtu hapa ameingia chumba chetu wakawa hawamuoni, nilipokomaa kumchunguza akanipiga ngumi ya mdomoni nikapiga kelele wazazi wangu wakawa hawaamini baada ya dakika chache mdomo ukaumuka (vimba) wakaanza kuogopa na kupiga kelele kuomba msaada toka kwa majirani na tangu siku hiyo wakaanza kuniamini!

Pole kwa kupigwa ngumi
 
All in all, ushauri wangu msijaribu kwenda kufungua jicho la tatu, wengine huona raha wakidhania watakua spiderman au superman wanayemuona kwenye movie... Hii sio movie, wala si science, hakuna kitu kama science unavoona kwenye science fiction ati ubongo una initiate a certain energy inayokufanya unaona future, huu ni uchawi tu sema wajanja wameu-modernize uonekane kama science, ndio maana wakaanza kwa kuwapa movie kwanza ziwachanganye akili. There's no science in these stuffs, vyote ni uchawi tu. Don;t open the third eye maana wengi ambao wakifungua hua wana-vibrate katika frequency ndogo sasa hujikuta huona mizimu na maviumbe ya kutisha (yote majini hayo) hadi ujue kuvibrate kwa frequency ya kutosha utakua ushateseka sana... Just a warning, kama hutaki unadhani its fun basi fungua hilo jicho la tatu ukidhani utakua spiderman, utajionea madhara yake mwishoni.. n its an addiction kuliko hata madawa ya kulevya. Huu ujuzi wote subiri mbinguni tutavijua, vilifungwa hapa duniani kwa kusudi maalum

Kidogo unanishawishi
 
Ngoja naingia Church nikitoka takupa full version lakini pia angalia post nyingine hapo chini kwa kuanzia
Mkuu mshana jr kwani ukifanya haya mambo bado unaweza kuendelea kuwa muumini? ninaowafahamu wakifanya haya mambo wamekuwa hawana muda tena wa kusali

cc: Pasco
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom