Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?


unawexa nisaidia###
 
unawexa nisaidia###

Kukusaidia nini mkuu?? Mana mi nae si lolote sana japo niliwahi kujifunza hii kitu pale chang'ombe maduka mawili, ila tatizo visa yangu ilitoka mapema nikasepa Kabla sijajengeka vizuri.
Mi pia i need msaada sana kwenye hili tena kwa sasa ndo nna uhitaji mno.
Maana napenda nifungue my third eye, pia nataka nianze meditation serious ila sasa hawa jamaa wote hawaonekani. Nahitaji mwalimu pia.
 

When a chela is ready, a guru appears.
 

Bado upo nataka jifunza
 
Pasco naomba kuifufua hii mada japokuwa ni ya siku nyingi. Naomba unipe ufafananuzi kidogo. Kipindi cha nyuma nilikuwa nikitembelea maeneo fulani akili yangu inaniambia nilishaona hilo eneo before. Wakati mwingine nimuona mtu kwa mara ya kwanza lakini kumbukumbu zinanionyesha nimewah kukutana nae kabla. Pia baadhi ya events, naweza kuwa tumekaa sehem na watu kadhaa, akili inanionyesha hii image kama niliiona kabla, pia najua kabisa mtu fulani atasema kitu fulani, na kweli anakisema pale pale. Kinapotokea kitu kama hicho huwa nabaki kama nimeduwaa hivi. Ni nini hasa huwa kinatokea?

Pia nimekuwa nikiota mara nyingi kwamba ninakabiliwa na mtihani shuleni na sijajiandaa kuufanya. Ndoto hii imejirudia mara nyingi sana. Basi najikuta naumia rohoni na kuwa na wasiwasi ndotoni, ninaposhtuka ndo nagundua ilikuwa ni ndoto. In reality sipo shule wala sina mtihani wowote unaonikabili, chuo nimemaliza siku nyingi. Maana yake nini??
 
Last edited by a moderator:
Pasco pita huku tafadhali
 
Last edited by a moderator:
hata mimi mara kibao nimekuwa nikiota
kwamba ninakabiliwa na mtihani shuleni
na sijajiandaa kuufanya roho inauma wee. wakat kwasasa sisomi. loh ndoto inajirudiarudia karibu kila baada ya miez miwili.
PASCO ufafanuzi hapa tafadhali
 
Niko kigoma nahitaji kujifunza nanimewahi kuwa na halizinazofanana na hizo lakini zipotea nahitaji msaada.namba yangu ni 0753299960 email kayuzisaid@gmail.com
 
Mkuu malenga wetu,kwanza samahani, siku hizi huwa sipiti sana pande hizi, na nilikuwa busy kumuingiza mtu wetu ikulu, ila ndio hivyo tena!, sasa ni kazi tuu!.

Hiyo ya kutembea na kujiona uliishafika mahali, au kukutana na mtu ukajiona mliisha kutana kabla inaitwa De javu!. Ni kumbukumbu ambayo iko stored kwenye subconscious mind yako kwa combination ya
Precognition, premonition and precognitive dreams - Perception of events before they happen.
ambapo mwili wa binadamu una sehemu kuu mbili, mwili wa nyama, physical body, na mwili wa roho, spirritual body, au astral body.Movement na actions za Physical body ndio inatumia kanuni za kisayansi za motion zinazohusisha mass, distance time, lakini spiritual body haina uzito, haina time wala distance, ndio inayohusika kwenye ndoto ambapo kuna baadhi ya ndoto ukiota physical body inakuwa imelala, na spiritual inakuwa imesafiri hivyo hao watu, hayo maeneo spiritual body yako inakuwa tayari iliishafika hapo na hao watu mliishakutana spiritually na kumbukumbu zote za spiritual body zinahifadhiwa kwenye subconcious mind sasa physical body inapofika tena, au kukutana na huyo mtu, ndipo subconscious inafunguka kukukumbusha kuwa hapa niliisha fika au huyu mtu niliisha muona. Sometimes ni tukio kabisa ambalo limetokea kwa mara ya kwanza, lakini kina kinachotokea wewe unakuwa kama uliisha kiona!.

Kuna baadhi ya ndoto zinakuwa kweli, unaota kitu fulani au jambo fulani limetokea, mfano msiba, na kesho yake au baada ya siku chache unapokea taarifa za kotokea tukio hilo au msiba. Hapa ni spiritual body yako inakuwa ilitoka ukiwa ndotoni kwenda kushuhudia na kurejea. Kuna baadhi ya ndoto ni matukio ya kweli na nyingine ni ndoto tuu!.

Hiyo ya kujua mtu atasema nini kabla hajasema ni simple telepathy, yaani wakati anafikiria kusema wewe unakuwa umesikia kabla, au mekaa mahali mnamsema mtu fulani mara anatokea!, mtasikika mkisema "una maisha marefu" sasa hivi tulikuwa tunakuzungumzia, mara umetokea!. Au unatembea kwenye kichochoro, unakutana na mtu, ile mnataka kupisha wewe ukipisha huku na yeye anapisha huko huko unarudi huku na yeye anarudi huku ndipo unasimama ili yeye aamue anapisha wapi ndipo mnapishana!.

Kuna kitu kinaitwa preamonition, ni jambo unalisema au unaliota kisha linatokea, hii peamonition ipo inayotokea naturally na kuna nyingine, unaiomba kwa kauli pale unapoisema, hivi ndivyo laana inavyotengenezwa, inatengenezwa kwa kauli tuu!, kauli huumba!.

Hilo la kuota unakabiliwa na mtihani ni ndoto za maono kuwa utakabiliwa na changamoto fulani au mitihani ya maisha, ila unakuwa prepared. Kwenye ndoto kuna direct dreams, unaona umepata pesa, kweli unapata pesa!, unaota fulani amekufa, kweli fulani anakufa!. Kuna ndoto ni inverse or opposite!, unaota uko kwenye sherehe ya harusi, unapata msiba!, unaota unapaa angani, unapata majanga!, unaota umetumbukia kwenye shimo efu, ana unakimbizwa na simba, nyoka etc, unapata neema!.

NB. Mimi sio mfasiri wa nyota, wala sina powers zozote bali ni kutokana na kusoma tuu vitabu mbalimbali!.

Jumapili njema.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…