Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Unajua acheni kujidanganya,..Nguvu mnazozungumzia nyinyi ni tofauti na na nguvu na miujiza ya Mungu,....nguvu za MUNGU za kutoa pepo hizo huwezi kuwa nazo hovyohovyo tu kama huenendi ktk njia ya kumwamini KRISTO YESU,..mnajidanganya,...kutoa pepo Kwa mtu aliyepagawa na pepo inabidi uwe na uwezo NA NGUVU ZA MUNGU na uishi maisha ya utakatifu,...tEna jina la YESU mapepo wanaliogopa kwasababu ni mwana wa MUNGU,...waganga hawatoi pepo ila wanazituliza2,..na nyi kama mnasema kila mtu ananguvu siku mujaribu kutoa pepo kwa mtu aliyepagawa na nguvu za giza,..alaf utaleta majibu apa,.....
acheni kudanganyaa watu kias hicho,..
 
hawa watu sijui wanatoa wapi maneno yaao,...eti shetani ameumbwa na kwa moto,...daahhhhh hili ni tatizoo kwa watu,..hawajui ukweli wa mambo.....alaf wanaenda kinyume na maandiko
 
ACHA Kudanganya watu,..na idea zako za kucopy google
.
unapoteza watu....
 

mkuu kwanini isiwezekane? najua wapata ugumu kuamini lkn ukweli na uwazi hata kwenye hiyo bible umeandikwa sana.mfano kuna mahala yesu alisema kama ungekuwa na imani kama punje ya aladani tuu ungeweza uamlisha mrina uhame na ukahama kweli,
 
mkuu kwanini isiwezekane? najua wapata ugumu kuamini lkn ukweli na uwazi hata kwenye hiyo bible umeandikwa sana.mfano kuna mahala yesu alisema kama ungekuwa na imani kama punje ya aladani tuu ungeweza uamlisha mrina uhame na ukahama kweli,
sasa lazima ujue kuwa aliwaambia akina nani???????aliwaambia wasioamini ktkt Yesu???????
no aliwaambia wanamwamini Yesu so hiyo imani aliozungumzia pale ni ile kwa walioamini2
 
Salaam wakuu! Mimi Ni mgeni kwa hii jukwa nzuuri of my dream, sasa ningekuomba mzee Pasco unifahamishe Mimi Nina nguvu gani? Mara nyiingi nikifikiria kitu flani na baada ya mdha Tu hutendeka, AMA kamkumbuka mtu na ajitokeze na yawezekana
 
Salaam wakuu! Mimi Ni mgeni kwa hii jukwa nzuuri of my dream, sasa ningekuomba mzee Pasco unifahamishe Mimi Nina nguvu gani? Mara nyiingi nikifikiria kitu flani na baada ya mdha Tu hutendeka, AMA kamkumbuka mtu na ajitokeze na yawezekana
Inategemea umezaliwa Tarehe gani na mwezi gani? nyota yako ina nguvu na una Spirit ndani ya nyota yako ndio maana ukihisi kitu kinatokea .
 

ACHA Kudanganya watu,..na idea zako za kucopy google
unapoteza watu....
Mkuu kwanza naomba nikukaribishe katika uzi huu, kwa vile hii ni post ya 1572, na nawaelewa Watanzania wengi ni wavivu kusoma, hivyo hujaweza kusoma nini kilisemwa huko nyuma, kwa sababu hayo maswali yako yote yaliishaulizwa kule nyuma na yalijibiwa, ila kwa faida ya wengi, na wengine kama wewe ambao ni wavivu kusoma, nitajibu tena!.
Kwanza karibu uzi huu,
"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu ya Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani
Wanabodi,
Huu ni muendelezo makala zangu kuhusu "works of powers", nguvu za kutenda miujiza, "psychic powers!", leo nitajikita zaidi katika nguvu za uponaji "faith healing!". Nitakuwa na maeneo yafuatayo.

  1. Faith Healing ni nini?.
  2. Faith Healing Inafanyikaje?.
  3. Nguvu za Uponyaji zinatoka wapi
  4. Je Wahubiri wa Uponyaji ni Lazima wawe Wakristu?.
Nakuhakikishia, ni Hakika Asilimia 100% kwa 100% Uwezo huo unao, ila kwa vile hujitambui, hautumii!. Jitambue, utumie!.?

Somo la Kwanza, Faith Healing ni Nini?!.Kwa wale ambao ni wageni, nawashauri kabla hujaanza na uzi huu, wapitie kwanza hapa, Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila wao Kujijua!...Na tuanze kwa kukumbushana tuu kidogo the basics!.

  1. Sisi binadamu tumeumbwa na Mungu kwa mfano wake. Ule uhai aliotupulizia, una nguvu za KiMungu ndani yetu!. Haijalishi wewe ni wa dini gani, ni wa imani gani, au hata wasio amini, wote tumeumbwa na Mungu, hivyo uwezo wa KiMungu uko ndani yetu, ni kwa kuutumia uwezo huu, ndipo muujiza hufanyika!.
  2. Faith Healing, ni uponyaji kwa kutumia imani!. Ambapo ule uponyaji huitwa muujiza. Historia ya kupona kwa miujiza ilianza zamani na sehemu kubwa ilijikita katika dini!, huko mimi siendi. Lengo la uzi huu ni kukujulisha wewe kuwa miujiza yoyote inayotokea, inawezekana kwa uwezo iliomo ndani yako wewe mtendewa muujiza na sio mtenda!.
  3. Hii Faith Healing ni kitendo cha mtu mwenye ugojwa fulani, kupona kwa njia ya imani tuu bila kutumia dawa yoyote, hivyo kipona kimiujiza, na uponyaji huu sometimes unahusisha hadi kufufua wafu, au kuzuia kifo, vipofu wanaona, viziwi wanasikia, bubu wanaongea, vilema wanaponyeka, viwete wanatembea, wagumba wanapata watoto, maradhi yoyote yanaponyeka.
  4. Miujiza hii imegawanyika katika makundi makuu matatu, ya kwanza ni ile miujiza inayofanywa na Mungu mwenyewe, muujiza mkuu ukiwa ni uumbaji! wa ulimwengu na kumuumba Adam. Miujiza inayofanywa na Mungu mwenyewe mingine ina sababu na mingine haina sababu, mfano muujiza wa kuiamuru bahari ya Sham kufunguka, ilikuwa na sababu ili Wana wa Israel wapite, lakini muujiza wa Bikiri Maria kupokea mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, haukuwa na sababu kwanini Maria, kulikuwa na mabikira wengi tuu!. Hii miujiza ya Mungu mwenyewe huitwa miujiza mikuu!. Miujiza iliofanywa na Yesu, nayo inaingia kwenye kundi hili la miujiza mikuu kufuatia imani kwa wanaomuamini Yesu ni Mwana wa Mungu, hivyo ni Mungu!
  5. Kisha kuna miujiza inayofanywa na sisi binadamu kupitia uwezo wa KiMungu ulio ndani yetu. Hii inajumuisha miujiza iliyofanywa na manabii, miujiza iliyofanywa na binadamu kwa uwezo wa Mungu ilio ndani yetu na mambo mazuri, na mema yote yanayofanyika duniani, ni kazi nzuri ya roho wa Mungu aliye ndani yetu.
  6. Pamoja na uwepo wa Mungu ndani yetu, mwovu shetani pia naye yupo duniani, na anazo nguvu kama za Mungu kutenda karibu kila kitu ambacho Mungu anatenda isipokuwa Mungu ana nguvu zaidi ya shetani!. jambo moja tuu!, upande wa uumbaji!. Yaani God is the creator and giver of life na ni ndani ya hii life ndimo zilimo nguvu za Mungu ndani yetu. Tofauti pekee kati ya Mungu na shetani, ni "life" shetani hawezi kuumba ila ndie muagamizi wa life. Maovu yote yanafanyika humu duniani ikiwemo miujiza ya uovu, ni kazi ya shetani. Zile sifa kuu tatu za Mungu, Omnipotence, hana mwisho, na shetani pia hana mwisho, tofauti ni Mungu ni wa milele na makao yake ya milele ni peponi, mbinguni au ahera kwenye furaha ya milele, na shetani makao yake ya milele ni motoni, kwenye ziwa la moto, akiungua na kuteseka milele!. Mungu ni Omnipresence, yaani yuko kila mahali, kitendo tuu cha mwanaadamu kupuliziwa pumzi ya uhai yenye Uuungu ndani yake, kunapelekea ndani ya kila binadamu kuna Mungu ndani yetu!, shetani naye alitupwa duniani, yeye na jeshi lake, nao pia wako kila mahali! ila ni nje ya miili yetu!. Mungu ni Omniscience, ana uwezo wa kujua kila kitu kabla hakijatokea, there is nothing new under the sun, hivyo lolote litakalotokea, lilikuwa litokee, ila shetani naye ana uwezo wa kuijua mipango yote ya Mungu na kujitahidi kuiangamiza!.Hivyo faith healing ni uwezo wa kufanya miujiza ya uponyaji kwa kutibu kwa kutumia nguvu za Uungu zilizo ndani yetu, au kwa waliomkaribisha shetani ndani yao, basi ni uwezo wa uponyaji au kutibu kwa kutumia nguvu za shetani zilizo ndani yao!, waganga, wanga, wachawi, wapiga ramli, wasoma nyota etc.
Somo la 2. Faith Healing unafanyikaje na inatibu vipi?.

  1. The most powerful thing kwenye mwili wa binaadami ni "will powers", "where there is a will, there is a way!. Hii "Will power" ni nguvu ya Mungu iliyo ndani yetu yenye uwezo wa kufanya kila kitu, ikiwemo miujiza!. Ili hii "will powers iweze kutenda miujiza, it has to be invoked!.
  2. Prescription ya faith healing, ni imani kuamini, na inafanyika kwa aina nyingi na kwa namna nyingi. Aina maarufu ni ile ya kuombewa na wahubiri/wachungaji/mitume/manabii/masheikh/viongozi wa dini/walokole/wanajimu/waganga wa kienyeji/watoa tiba mbadala etc, etc, dawa pekee kwenye tiba hii ni imani!. Kitendo cha kuamini ndicho kina invoke zile doors za forces of will to act upon a specific desease and cure it!.
  3. Kinachofanyika ni kwanza kutengeneza imani ya kuamini unachotakiwa kuamini. Kwa wale wa imani ya Kikiristu kwanza ni kuamini kwa dhati kuwa Yesu anakoa, Yesu anaponya, hivyo anayekuhubiria kwa kulitaja jina la Yesu, "Katika Jina la Yesu Zishindwe!", "Katika Jina la Bwana", etc, etc. Kitendo cha kuamini kuwa Yesu anaponya, kunafungua milango ya "powers of will" zilizo ndani yako ndizo zinazokuponya!. Kinachoponya ni nguvu ya Uungu iliyoko ndani yako, lile jina la Yesu, limetumika kama ufunguo tuu wa kufungulia hizo potentials zilizoko ndani yako!.
  4. Wale wahubiri wa miujiza, wanachofanya ni kuutumia uwezo wao wa kuconvince ili kuifungua imani yako, ili ifungue hazina ya nguvu za uponyaji zilizoko ndani yako ndizo zinazotenda miujiza na sio yule mhubiri wala hilo jina!. Mhubiri ni make believe tuu na Jina la Yesu ndio ufunguo wa imani yako ili kufungua nguvu zilizo ndani yako kukuponya baada ya kuamini kwa dhati umeponywa!.
  5. Wako watu kibao wanatibu kwa faith healing bila kulitaja jina lolote na watu wanapona!, kinachotakiwa ni kuamini tuu!, ndiko kunakofungua milango ya "powers" na haijalishi unaamini nini, iwe Mungu, Allah, Budha, Mti, jiwe, milima, kichuguu, hirizi, mganga or whoever, whataver as long as unaamini utapona, unapona!.
  6. Namna ambayo hizo powers of will zinavyofanya kazi, ni un explainable scientifically, biologically, or medically, ila kinachoonekana ni matokeo tuu, viziwi wanasikia, vipofu wanaona, na viwete wanatembea na vilema wanaponyeka! ndio maana inaitwa miracles, miujiza na jina rasmi la kibinaadamu inaitwa ni kazi ya Mungu, au miujiza ya Mungu, na kwa vile nguvu zinazotumika ni nguvu za Mungu zilizo ndani yetu, hivyo ni haki kuita hii ni kazi ya Mungu.
  7. Wengi hukumbilia kwa wahubiri kuomba kuponywa wakati tayari wameathirika!. Kwa kujua kuwa hizo nguvu za uponyaji ziko ndani yetu, unaweza usisubiri hadi kuugua ndipo uinvoke will power ikutibu, ikiisha jitambua tuu, its you, and no one else, then unaweza kuivoke hiyo will powers ikazuia usipate ugojwa, yaani prevention is better than cure!.
  8. Hivyo kwa kuanzia anza kwa kujiandaa kuamini ili hiyo imani yako ifungue milango ya nguvu za Mungu za kufanya uponyaji zilizo ndani yako sio tuu zikuponye, bali pia kuzitumia as shield kuzuia magonjwa yoyote yasikufikie wewe na familia yako!.
Somo la 4: Jee Nguvu Hizi za Uponyaji zinatoka wapi?.

  1. Msingi wa Nguvu za uponyaji ni Mungu, kwa jina lolote lile. Siku Mungu alipotuumba, alituumba kwa mfano ambapo mwili wetu una sehemu kuu mbili, mwili na roho. Mwili ni hii body inashikika, inaonekana, ina uzito, ina tabia zote za maada/matter. Sehemu ya pili roho, ni pale alipotuumba kwa ,mfano wake na kutupulizia pumzi ya uzima, life, life force, spirit, spiritual body, astra body, roho, uhai. Kinachofanyika ndani yangu kuzuia malaria ni kufuatia ule uoga wangu kuogopa kuteseka na dawa za malaria, ninapo jisikia dalili tuu za awali kabisa, kwa mwili kuwa hypasensitive to touch, nikijigusa tuu vinyelea vya mkono, you feel something, then nasema kwa imani, it can't be malaria!. Hii inaitwa "denial the negativivity", kwa kujitamkia tuu maneno hayo kimoyo moyo, hiyo malaria stops there and then!.
  2. Hizo powers zipo ndani yetu zimehifadhiwa, namna ya kuzifungua ni kwa imani tuu!. Ukiamini, Milango ya powers inafunguka, "powers from within" zinaufanya mwili kuwa stronger na vile vidudu vya malaria harmless ila vipo!. Kadri siku zinavyokwenda vijidudu vinazidi ku pile, ila ni harmless. In ten years time vikawa vingi sana but harmless, nilipopimwa mpimaji anashtuka, daktari anashtuka, mimi niko ok.


  3. Hata wale wanaotibiwa maradhi kwa imani, haina maana akiumwa ndio asiende hospitali ati kwa sababu tuu anamtegemea Mungu!, au alikuwa na ukimwi, kifua kikuu, cancer, akatibiwa kwa imani, akapona, basi hospitali ndio basi!, no!. Faith healing is not a substitute to medical treatment, but rather a complementary!.
  4. Namalizia kwa msisitizo, kuponywa kwa miujiza, nguvu za uponyaji zinatoka kwako wewe mgojwa mwenyewe na sio hiyo anayekuombea!. Wachungaji wengi au waganga, hujifanya wao ndio wenye hizo nguvu za kuponya!, No way, wao wanakupatia tuu ufunguo wa kuzifungulia hizo nguvu zilizo ndani yako ndizo zinazoponya. Hata kile kikombe cha Babu, what you drink is nothing!, imani kuwa kikombe kinaponya ndio imewafungulia njia wenye imani, nguvu zao zilifunguka zikawaponya, na wale wenye imani haba, it was a waste, wastage of time and resources!.
  5. Ukiwa na very strong faith kuwa sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, hivyo tunazo nguvu za Mungu ndani yetu, chochote utakachopanga kwa imani, kitafanikiwa!, sky is the limit!.
Anza sasa kuzifungua hizo nguvu zako na kuanza kuzitumia kufanya mambo madogo madogo.
Somo la 5: Je Wenye kuweza Kuponya wa Miujiza lazima wawe Wakristo?!.

  1. Baada ya kwanza kukubaliana kuwa Muumbaji wa Vitu vyote ni Mmoja, God!, The Creator!, haijalishi mtu una imani gani, au hata kama huna imani, maadam uliumbwa na Mungu na Mungu ndiye aliyeziweka hizi nguvu kwa viumbe wake, hivyo mbele ya Mungu, binadamu wote ni sawa, na wote wanazo hizi nguvu, na wote wanaweza kuzitumia na wamekuwa wakizitumia!.
  2. Kufuatia msimamo huu, watu wote wana uwezo wa kuponya na sii lazima wawe ni Wakristu ila kasi ya uponyaji kwa kutumia imani, imekuwa more popular na Wakristu kwa sababu wanaamini mwenye hizi nguvu za uponyaji ni kupitia kwa Jina la Yesu Pekee!. Ukweli ni kuwa, nguvu za uponyaji, ziko ndani yetu!, Ili uweze kuzitumia ni lazima kwanza uzifungulia milango "open the gates" hizi nguvu zilizofungiwa ndani yako, ndipo ziweze kufanya uponyaji, kitendo cha kuamini "Ni Katika Jina la Yesu!", hiyo ni catalyst tuu ya kuzifungulia milango!. Watu wengine wowote, wenye imani nyingine yoyote, pia wanaweza kuyafanya haya yote alimradi wazifungulie milango hizi nguvu kwa imani yoyote!.
  3. Wakristu wanaamini kawa muujiza wa kwanza wa uponyaji ulifanywa na Yesu, alipomfufua Lazaro, na kaendelea kuponya wagonjwa kwa vipofu kuona, viziwi kusikia, na wenye ulemavu mbalimbali kutakaswa, hivyo powers hizi za uponyaji zimehusishwa na Jina La Yesu, ndani ya Ukristo kama kulivyo na madhehebu mengi tofauti na yote yakimwamini Yesu, vivyo hivyo imani hii ya uponaji inatofautiana sana kati ya dhehebu na dhehebu, ambao Kanisa Katoliki liko makini sana na tiba hizi za imani, wakati makanisa ya wokovu, wakizikumbatia powers hizi kama fimbo ya kukamatia waumini na wafuasi.
  4. Kanisa Katoliki linaamini Mungu hufanya uponyaji pale tuu anapoamua kupitia nguvu alizowapa Makasisi wake ndani ya sala, hivyo hakuna utaratibu wa kuwapeleka wagonjwa au wenye matatizo makanisani kuombewa, kwa sababu maisha yetu sii ya dunia hii, kinachotakiwa kufanyika kwa mgonjwa mahututi, ni kumpatia sakrament ya Upako Mtakatifu ili kumuondolea dhambi zake zote hapa duniani ili akifa aingie mbinguni au peponi moja kwa moja!. Na Baada ya kuzuka kwa wimbi kubwa la uponyaji, Askofu Milingo wa Zambia alitumia powers za asili kuponya makanisani, aliitwa na kupewa kifungo huko Vatican, na kwa hapa kwetu Tanzania, Padri Nkera nae alitimuliwa na kikundi chake cha Wanamaombi kikapigwa marufuku, lakini kufuatia wimbi kubwa la kupoteza waumini wanaokimbilia makanisa ya Wokovu, hatimaye Kanisa Katoliki limelegeza masharti kwa kuwaruhusu watu wanaoitwa Wana Karismatiki kuendesha maombi ya uponyaji bali sio ndani ya nyumba za ibada!.
  5. Kwa vile tumetawaliwa zaidi na dini kuu mbili Ukristo na Uislamu, na hizi sio dini zetu za asili, nguvu za uponyaji wa miujiza zilikuwepo tangu zamani, enzi za mababu zetu, na wazungu na Waarabu walipokuja kutuletea dini zao, walitukuta na uwezo mkubwa, ila wakatuhadaa kuwa hao miungu wa asili tunaowaabudu, sio Mungu wa kweli, bali Mungu wa kweli ni Mungu wao God na Allah, hivyo wengi wetu kujikuta tumezaliwa kwenye hizi mbili kuu bila choice na wote huishia kujikita katika imani ya dini uliyozaliwa nayo tuu, lakini ukweli wa nguvu za uponyaji zaidi ya kwenye Ukristu, pia kwenye Uislamu upo, kwenye Hindu upo, kwenye Budhiism upo kila mahali na hata wengi waganga wa kienyeji, wale ambao ni waganga wa ukweli, ukiachana na hawa wa longo longo, nao wanazitumia nguvu hizi hizi za uponyaji zilizomo ndani yetu, ile kupiga manyanga ndio catalysti yenyewe ya kuzufungulia nguvu hizi za uponyaji zilizo ndani yako, ndizo zinazokuponya bila wewe kujijua huku ukiamini ni huyo Mganga!.
  6. Nguvu hizi za uponyaji, zinasemekana kuweza kuponya magonjwa yoyote yaliyoshindikanika mahospitalini ikiwemo AIDS, cancer, ugumba, vipofu kuona, vilema kutembea, viziwi kusikia, etc etc ila mimi kama mhanga wa ajali, nimefuatilia kwa karibu baadhi ya hawa wahubiri wanaojifanya wana uwezo wa uponyaji, sijaweza kufanikiwa kuuthibitisha uwezo huo!, nyingi na hivi mnavyoviona kwenye TV kama ni uponyaji, asilimia kubwa ni viini macho tuu, ila pia uponyaji wa ukweli upo kwa sababu unatokea ndani ya yule mgonjwa mwenyewe, ambaye anaponywa kwa imani yake huku mhubiri akichukua credts.
  7. Wengi wa hawa wahubiri wa makanisa ya Wokovu, wameishajua powers za uponyaji ziko ndani ya kila mtu, hiyo wanaihifadhi kama siri yao ila wanaitumia imani yako kukuponya and in return kuvuta fungu kwa hoja ya kufanya kazi ya Bwana, na mengi ya magonjwa yanayoombewa ni yale yasiyoonekana!, mapepo, magonjwa na ndani etc, sijapata kushuhudia popote hapa Tanzania kipofu anaona, kiziwi anasikia, kilema miguu inanyooka anatembea!, wengi wa hao mnaowaona kwenye TV ni stage acting to make believe!, ndio maana utaishia kuwaonea pale majukwaani tuu!, hakuna any follow-up ya uthibitisho wa ndugu, jamaa au majirani kuthibitisha huyu alikwa kilema sasa anatembea zaidi zile shuhuda za madhabahuni!,
  8. Kwa vile nguvu hizi za uponyaji ni za kutoka kwa Mungu, process nzima ya uponyaji bado haina scietific proof ya ni nini haswa kinatokea, mtu amekuwa diognaized with aids then anaombewa, anarudi kupimwa, aids haipo tena!, kufuatia kukosekana kwa uthibitisho wa kidaktari ugonjwa huo umeponaje!, nasisitiza mtu ukiwa unaumwa chochote serious, pamoja na posibilitiy ya kujitibia kwa imani, nenda hospitalini ukapate ushauri wa kitabibu na sio kuzitegemea nguvu hizo pekee!. Kuna wengi walioitegemea imani pekee, wakaishia kupata maafa ya kufiwa, kufiliwa na kuwapoteza wapendwa wao, kwa magonjwa ya kawaida tuu ambayo mahositalini wangetibiwa na kupona!.
  9. Pamoja na kuwepo kwa uwezo huu wa uponyaji miongoni mwetu, pia sometimes utapeli wa iaina fulani pia upo!, utakuta wahubiri wetu hawa hawa, wanapofanya zaira za mahubiri nje ya vituo vyao vya kawaida, ndiko wanakofanya miujiza mikubwa ya ajabu!. Tumewashuhudia wahubiri wetu wakipokelewa na kukaribishwa Ikulu za watu wengi huko huko wakifanya uponyaji wa ajabu ambao hapa nyumbani hawaufanyi!, hizi ni make belive tuu na mwisho wa siku kitu muhimu kwao ni ile number ya M=Pesa/Airtel Money/Tigo Pesa au Z-Pesa ndio mpango mzima!.
  10. Na mwisho kama nilivyoeleza kwenye mada zangu zilizotangulia, Mungu yupo ni mwenye nguvu na ndiye aliyetupatia huu uwezo ndani yetu!, ila pia shetani naye yupo!, na yeye pia ana uwezo!. Yesu alipoondoka alituasa kuwa "Watakuja watu, watafanya miujiza ya uponyaji na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sio wangu!", hivyo wale wenye imani haba, wanaweza kujikuta wanapotezwa maboya na hawa wahubiri wa miujiza wakidhani uwezo wao unatoka kwa Mungu, kumbe unatoka kwa shetani, na nguvu wanazotumia ni nguvu za giza!. Hivyo kuna uponyaji unafanyika kwa nguvu za Mungu na mwingine ni kwa nguvu za giza!.Jee utajuaje kama hizi ni nguvu za Mungu au ni nguvu za giza?!. The ony way kutambua ni kwa ku "listen from yourself!", " only the voice from wthin ndio inaweza kukuonyesha kweli!.
Nasisitiza hizi mada ni kwa watu ambao ni open minded!, Nawaomba sana wale wahafidhina na ma conservatives wa imani za dini zao, shikilieni mafundisho ya dini zenu, na wenye nia ya kuanzisha malumbano ya dini, tukutanie Jukwaa la Dini, tuwekane sawa!.

Natanguliza Shukrani.

Pasco.
 
Nina swali!Je kuna binadamu kizazi hiki anaweza akafanya muujiza wa kutembea juu ya maji kwa kutumia hizo nguvu kama YESU alivyofanya?
 
Je inawezrkana kusoma mind y mtu?!au kuiongelesha mind ya mtu yaani remotely?
 
Hebu nisaidie kitu kimoja brother PASCO.kama hivyo ndivyo,hii kwenda makanisani,misikitini,mitini,mapangoni,sangoma nk..ni kujaribu tu kustalabiana tuheshimiane au kuogopa kutenda na kutendewa mabaya au ni nini???coz kama nguvu tunazo na kila kitu MUNGU MUUMBA alifanya ndani yetu why twende huko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…