Au wakati mwingine unamtakia mtu neno hata kwa utani hee inakua kweli, hadi mwingine ananiambia tafadhali niongelee kwa mazuri. Hii ni nini Pasco?
Kusema jambo ambalo linatokea, hiyo ni power of speech!. Kama nilivyosema tangu mwanzo wa uzi huu, sisi binadamu tumeumbwa na nguvu za kiMungu ndani yetu. Wengine nguvu hizo zinajibainisha wazi sana na wengine zimejificha na kuibuka in times of need ila kila kiumbe chenye uhai kina powers.
Miongoni mwa maeneo makubwa yenye nguvu hizi ni nguvu ya kauli, "kauli huumba!" "the power of speech" ambapo maneno huumba!. Mungu alipoumba ulimwengu alitumia kauli tuu, na iwe mbingu, na iwe viumbe, na iwe ardhi, vitu vingine vyote vimeumbwa kwa kauli isipokuwa binadamu ndio amemuumba kwa mavumbi kwa kufinyanga udongo na kumpulizia pumzi ya uzima, pumzi hiyo ndio uhai, ndiyo yenye nguvu za Uungu ndani yake!.
Hata Yesu alifanya miujiza mingi kwa kauli tuu!. Wengi wa wahubiri wa uponyaji hutumia kauli kama "Katika jina la Yesu", "Jina la Bwana", "Zi shindwe", "Toka!". etc!.
Kitu kinachoitwa laana ni kauli tuu!, albadir, au itkaf ni kauli tuu, ndio maana kuna mara nyingi watu watasema usitoe kauli mbaya dhidi ya binadamu mwingine ni kuchuria watu!. Unapo wish mabaya fulani yamkute mwingine. Unakuwa umejifungulia njia kwa mabaya kukurudia wewe kwa njia ya "karma".
Kuna watu wengi wanakwama kimaisha kutokana na kauli za kukamishana, moja wapo kubwa ni kuukubali umasikini, kuna masikini wengi, ni masikini tuu kwa sababu wamejiumbia umasikini huo kwa kauli za kuukubali umasikini bila kujitambua!, na kuna matajiri wengi wamefanikiwa sana kutokana na kujiundia utajiri kwa kauli za utajiri!.
Power hii ya speech, huweza kutumika hata kuzuia magonjwa au kutibu magojwa na kujiletea mafanikio, inaitwa "affirmatives", toa kauli njema zitakazoleta neema, baraka na mafanikio!. Ukitoa kauli mbaya dhidi ya wengine, sio tuu zinaleta majanga bali pia unajiundia majanga yatakayo kurudia. "What goes around, comes around".
Mimi japo usafiri wangu ni boda boda, niliwahi kuwish kuja kuendesha Benzi!, nikajizungumzia kwa kauli, hivyo nikaumba kuendesha Benz na kweli ikaja kutokea kuendesha Benzi tena E-Class!. Sasa nimejinuizia kuendesha gari jingine fulani (naomba nisilitaje kwanza kuwaepuka wanga, wasije nichuria).
Katika kutoa kauli, sii lazima kutamka kwa sauti, ile genuine wish tuu ya dhamira ya dhati ndani ya mayo wako na nafsi yako, inatosha kabisa kufungua "powers of will" zilizo ndani yako kukufanyia mambo yako yawe mazuri!, yawe supper!. Na kuna wengine wenye ill motives, ambao kauli zao zina powers, wakikutolea kauli mbaya, mabaya yanakukuta na kweli una rosti na kuwa arosto!.
Ni muhimu sana kuchunga kauli zetu wakati wote zinakuwa regulated na kitu kinachoitwa "karma", tenda mema, fanya mema, sema mema, utavuna mema!. Sema maovu, fanya maovu, tenda maovu, utavuna uovu!.
Paskali