Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

DUH MKUU KUNA ELEMENTS NAMI NINAZO NAWE HAPO UMETAJA
 
telepathy inanihusu asee, nkikaa kimya nkimfikiria mtu haipit hata dakika anatokea , hata kama huyo mtu sio rafiki yangu sana , nkimuwaza tu flani anatokea
 
Well said
 
Mbona hujashusha hiyo kitu??
 
Hii mada nzuri sana ,nashukuru sana nimetokea kuiona.Nimesoma kwa umakini kuhusu Psychic Powers ambayo umeainisha hapo juu.

subiri nitoe ushuhuda wangu japo nilikuwa na plan ya kuandaa Thread ila ntaeleza kwa ufupi tu

Mimi hapa ni mpenzi wa masuala mengi lakini miongoni ya vitu ninazozipenda ni martial arts nakumbuka nilivyokuwa A level nilikuwa nacheza Shotokan sana lakini form 6 nikaacha kabisa kucheza.Kuna walimu kadhaa nimepita mikononi mwao mmoja wapo ni mjumbe wa TASHOKA =Tanzania shotokan association na pia ni muasisi wa chama cha karate cha kimataifa hapa nchini

Huyu sensei kuna matukio kadhaa nilikuwa nayaona kwake yalikuwa siyo ya kawaida mfano kuna siku mmoja wa wanafunzi alipatwa na tatizo la msuli kukaza basi yule sensei aliuchukua mkono wake akawa anaupitisha kwenye sehemu msuli uliokuwa umekaza lakini alikuwa hagusi mahala pale na huku akitamka maneno yake kimoyomoyo huwezi amini kwa dakika chache yule jamaa alipona na siyo huyo tu nimeshuhudia watu wengi wakiponywa kwa mtindo huo.

tukio lingine hili ni la kustaajabisha kabisa tulikuwa tupo kwenye mazoezi yule sensei alimchukua mmoja wetu na kumweka mbali kidogo halafu akawa amekaa kwa hisia kama vile anafanya meditation kisha akaachia kama vile anampiga mtu ngumi huwezi kuamini yule jamaa alirushwa,alipigika ngumi akawa anaugulia

yote hiyo ilikuwa ni inner power sasa mm nikawa nipo obsessed sana kujua ni nini hiyo inner power inayomwezesha mtu kutibu,kumpiga mtu kwa mbali na tokea siku hiyo nikaamini mambo wanayoyafanya akina jet lee kwenye filamu ya taichi ni ukweli

baada ya kugraduate na kukaa kwa muda nilienda china kujiendeleza martial arts sababu nilikuwa napenda sana, kule nilijiunga na chuo/Temple lakini walikuwa wanafundisha Five animal floric maarufu kama Qigong (tiger, kulungu, bear, nyani na ndege) mafunzo yao mengi yalikuwa ya kubana pumzi,hisia,meditation,kata baada ya kujifunza external kata,sasa kuna inner ..na akili yangu ikanambia yale maajabu ya yule sensei huku bongo yalikuwa ni inner power sasa nikawa obsessed zaidi kumaster hiyo inner power

asee sina haja ya kumaliza maana stori ndefu lakini niliingiwa na majini na baadae hali ikawa mbaya nikaamua kurudi na kweli yalikuwa majini nikafanyiwa tiba namshukuru Mungu nilipona

chi/Inner power ambayo ma-master mbalimbali wanatibu,wanauwezo wa kukuua kabisa,upo mbali anakupiga makonde ile yote ni nguvu ya majini kwenye maonyesho utaona mtu anapigwa na matofali makubwa vitu vigumu yote sababu ya inner power..na ibada yote wanayofanya ile ya Budhism yanahusu majini..na nakumbuka siku ambayo yaliniingia ni siku ambayo tulikuwa tunafanya meditation ndio walituingizia inner power kumbe ni jini ..



kuhusu ishu ya kutoa majini kunaretired pastor mmoja alinambia huwa wanatumia mafuta fulani hivi wanapaka kwenye kiganja cha mikono ay kwenye kitamba,ukimwekea mtu kichwani haswa wkenye mishipa basi piga ua lazima atoke..

NB:meditation/chi siyo kitu kizuri na don't practise chi/Inner power,kwenye meditation ukifikia hatua ya kuwa paralzed pale kuna posibility kubwa ya kuwaposessed na jini kama ukitupiwa,

nguvu nyingi hizi haswa hawa Budha ni demons

Mungu akijaalia nitaandika thread kwa utulivu kuhusu experience hii na mengi kuhusu inner power,kung fu na budhism
 
Mkuu ninaifahamu hiyo temple je wanatoza kiingilio ama ni bure? Je meditation huwa wanazifanya siku zipi?
 
Mkuu japo huu uzi ni wa siku nyingi lakini umenivutia sana
 
Pasco ujajua tofauti ya nguvu za Mungu na Shetani na uwezo binafsi pia ujaijya Kali ya ambayo Mungu alisema tumfanye mtu Kwa mfano na sura yetu.ungezijua nguvu zinazofanya kazi nje ya mwanadamu ungerekebisha bahazi ya maneno kwenye Mada yako ambayo ni nzuri.
 
Ahsante sana kaka Pascal Mayala uejitahidi kufafanua jambo ambalo nimekuwa nikijitahidi kuwafahamisha watu muda mrefu ni kweli kila binadamu ana uwezo huo ila shida nikuweza kuzitumia au kujijengea uwezo kuzitumia nguvu hizo.

\
 
# Mshana jr, Pasco hebu njooni mfafanue kitu hapa.... Uwiiii inner power ni jini? [emoji15]
 
Mkuu inabidi ufunguke zaidi utawasaidia wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…