Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Kwahiyo mkuu chanzo hasa cha hiyo power ni nini?
 
Hii maada ni fikirishi sana na natamani kuzipa uchaji hizi psychic power na mimi ili niongeze busara zangu.
Mara nyingi nikiwa nawapigia simu ndugu hunambia wametoka kunizungumza,au la wamenikumbuka.pia kuna kipindi flani nilikuwa nikisema flani utajikwaa ni lazima ajikwae na kuna kipindi flani katika kukata majani ya ng'ombe basi nikawa najisemea ngoja nikamate grasshoper bila hata kumuona na kweli nikishuka kwenye nyasi nakuta grasshoper na hii nilifanya almost kwa siku tatu mfululizo.
Nataman ningejua kipaji changu ni kipi ningekiendeleza.
 
Tupia nyota ya MTU alozaliwa mwez wa kumi trh 6
 
Tupia nyota ya MTU alozaliwa mwez wa kumi trh 6

NYOTA YA MIZANI (LIBRA)



Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12

Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 September na 22 Oktoba ya mwaka wowote.

Sayari yao ni VENUS (ZUHURA).

Siku yao ya Bahati ni Ijumaa.

Namba ya Bahati ni 6.

Rangi ya Bahati ni Kijani isiyoiva.

Asili ya nyota hii ni Hewa.


KIPAJI CHA MIZANI

(Extra Sensory Perception)

Wenye nyota hii wana kipaji cha kufumbua mafumbo na kujua siri za watu bila kuambiwa.


TABIA ZA MIZANI:

Wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kupenda usuluhishi, amani na upatanishi. Ni watu wasikivu, watiifu, na wepesi kuongozwa. Ni wenye maumbo ya kupendeza hasa wanawake. Kwa ujumla ni watu wenye roho nzuri na wanajua kupenda na wenye mahaba mengi.

Ni watu wastraabu, wenye adabu heshima na ni wakarimu kwa mtu yeyote na wanajipenda sana. Katika maisha yao wajipenda sana.

TABIA YA MIZANI KATIKA MAPENZI

Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye nyota hii ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye nyota hii wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.

Watu wa mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.

Kwa sababu hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina matatizo na zisizo na raha kwa sababu ya kuoa mapema bila kuangalia. Wenye nyota hii wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.

Katika suala la mahaba (Romance) na ngono (Sex) wao ni mabingwa. Wanajua sana kumpendeza mwanamke kwa maneno matamu yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.

Kwa ujumla wenye nyota ya Mizani wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao waishi katika hali nzuri.


TABIA YA MIZANI KATIKA FEDHA

Watu wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kutokuwa na maamuzi katika masuala ya fedha. Lakini hiyo siyo sababu ya wewe kufikiri kwamba wao ni wajinga.

Wanapofanya hivyo huwa wanapima au kufikiria kuona uwezekano wa fedha kutumika vizuri.

Ni watu wenye mipango mizuri na mara nyingi kwa kutumia uzoefu na kipaji chao kidiplomasia na upole, huwa wanapata mafanikio katika biashara zao.

Wana kipaji cha kuelewa watu wengine wanahitaji nini na wanatumia maneno matamu kuwashawishi wawape wanachokitaka na wanafanikiwa.

Wanapenda sana vitu vizuri na vyenye thamani na wako tayari kutumia fedha yeyote kutekeleza malengo yao.

Kwa ujumla ni watumiaji wazuri na wenye ubinafsi mkubwa.


MAVAZI YA MIZANI

Wenye nyota ya Mizani wanatakiwa wavae nguo yenye kupendeza zenye mapambo na zenye kuashira mahaba.

Nguo ziwe za rangi ya Pinki au rangi ya udongo.

Kitambaa kiwe cha kotoni chepesi na chenye picha picha, kisiwe kile ambacho hakikuchorwa kitu.

Wavae sana mikanda na wapende kuvaa nakshi za maua pamoja na skafu au mitandio iliyoingia. Wanapendelea mavazi ya ushanga na mikufu.


MATATIZO YA KIAFYA

Nyota hii inatawala figo, sehemu ya utumbo mkubwa, kiuno, mpaka sehemu ya juu ya matako.

Sababu kubwa ya maradhi yao ni kwamba wanapenda sana kutafuta amani na suluhu hata wakiudhiwa au kukasirishwa. Matokeo yake wanavunjika moyo na kujinyima yale wanayoyapenda. Sana na hiyo inawafanya waudhike na wajisikie vibaya na inawasababishia maradhi.

Magonjwa yao makubwa ni figo, kibofu cha mkojo, ugonjwa usioambukiza wa ngozi unaowasha na unapojikuna huvimba (Eczema),maradhi ya misuli ya kiuno na matoki.

Tatizo lingine kubwa ni unene.Watu wa mizani wanapenda sana kula na hiyo inatokea sana wanapokuwa wameudhiwa. Wao wanaona ni bora zaidi kuondoa hasira zao kwa kula chakula.

KAZI ZA WENYE NYOTA YA MIZANI

Wenye nyota hii wanapenda sana kutumia uwezo wao wa kuzaliwa na inawawia vigumu wakati mwingine kutafuta kazi wanazozipenda.

Wanapenda kufanya kazi katika mazingira ya amani na yasiyo na usumbufu.

Kazi zao hasa zinakuwa za uhusiano wa jamii ushauri wa ndoa, biashara ya sanaa, ushauri wa mambo ya urembo au mwanasheria.


FAMILIA ZA MIZANI

Wazazi wenye nyota ya mizani wanapenda sana unadhifu na wanapenda watoto wao wawe nadhifu na wenye mavazi mazuri.

Wanapenda kutumia muda mwingi na fedha nyingi kuwafunza watoto wao tabia nzuri. Kwao ni muhimu sana mtoto akikubalika na kila mtu.

Wanapenda amani katika nyumba zao na wana tabia ya kuwapangia watoto wao namna ya kuishi na kufanya vitu ambavyo wao wnyewe wameshindwa kuvifanya.


MADINI YA MIZANI

Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa LAPIS LAZULI. Mawe kama nye rangi ya Bluu iliyokoza, wamisri wanayaita mawe ya peponi. Yakiwekwa kama kito kwenye pete ya dhahabu yanaleta mizani kwa wenye nyota hii.


UHUSIANO WA KIMAPENZI

(Punda na Mizani)

Tabia ya Punda ya haraka haraka. Vishindo na kutumia nguvu bila kufikiria, hulainishwa au kuzimwa na diplomasia, uerevu na ujanja wa mizani. Punda vile vile hupendezwa na uwezo au kipaji cha mahaba walichonacho wenye nyota ya mizani.


VYAKULA VYA MIZANI:
Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula au Matunda yafuatayo ambayo ndio yanayotawaliwa na nyota yao,Tufaha (Apple), viazi Mviringo (Potatoes), Chaza (Oyster) na Nyama ya Njiwa.


NCHI ZA KUISHI ZA MIZANI:
Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii ya Mizani.
Miji hiyo ni Copenhagen (Denmark) na Vienna (Austria) na nchi ni Canada na Japan.

RANGI ZA MIZANI
Wenye nyota hii wanapenda rangi zilizopakwa juu juu ra.na laini hivyo wanashauriwa watumie rangi ya aina yeyote lakini iwe hafifu katika nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara.


Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili Herbalist mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Herbalist MziziMkavu
 
Tuliozaliwa 23 October, ndio tupo nyota gani mkuu!??
 
Unapataje satanic power?
 
Dkt.Pasko

Kuhusu telepathic powers zako na kuwanasa wadada warembo.Utatuaminishaje kuwa uliwanasa warembo sababu ya telepathic power na si hali yako ya mvuto ulio nao?

Pili nini tofauti ya telepathic powet na psychiatric delusions ambazo wagonjwa wengi wa akili wanayo mathalani schizophrenia?
 
Mkuu Mzee, kwanza isiniite Dkt,
Pili telepathy ni communication through mind. Ili umnase mtu kwa mvuto lazima kwanza akuone, ndipo avutike, mtambulishane, mzungumze, mzoeane, mpange, ndipo mtekeleze!.

Lakini kutumia telepathy, hakuna kuongea lolote, unamtazama mtu, macho yakigongana tuu, unatoka, anakufuata, mnamalizana, bila hata kupanga, na mkimaliza, mtu anaona noma.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…