Jana nilienda kumpeleka dogo, skuli ndio anaanza kidato cha tano! Kwenye inspection walikuwa wanakagua mambo kadhaa wa kadhaa. Vyote vilikuwa sawa ila kwenye upana wa suruali nadhani wanahitaji kujitafakari!
Walikuwa wanahitaji upana wa chini wa miguu uwe 20 inchi. Katika wanafunzi wote waliokuwepo wakati huo kama 13 hivi hakuna hata mmoja aliekuja na vipimo hivyo. Na hata waalimu na wazazi tuliokuja hakuna hata mmoja aliekuwa amevaa suruali yenye vipimo hivyo.
Mimi nadhani kuna haja ya kureview hitaji hili. Sijiwi ni nini kinachowasukuma kufanya hivi, au labda ni sehemu ya upigaji? Maana kuna mwl aliandaliwa ambae unamlipa tsh 2,000 kwa ajili ya kutanunua kila suruali.
All in all kuwavalisha watoto mabuga kama hayo sio fair, natoa wito kwa waalimu wawe wanaenda na wakati walau kidogo, inch 20 is too wide. Tuwatendee wenzetu vile ambavyo na sisi tungependa tutendewe.