TANZIA Pumzika kwa amani Mzee Gregory Shigella

Status
Not open for further replies.
Huyo Mzee ni Mstaafu (82) alikuwa anaishi Ukonga stakishari, mie ni mjomba wangu na yeye ndiyo alikuwa Mzee wa familia kwa ukoo wa Majebele kwahiyo kila jambo mfano, harusi, misiba nk lazima ash.

Ndugu na jamaa walichanga kwenye msiba mpaka kamati ikataka kusitisha zoezi la kupokea rambirambi, hakika watu walijitoa sana.

Changamoto ilikuwa wapi azikwe, wengi wana ndugu walipendekeza Kinondoni na hata kamati ilipendekeza Kinondoni ila kutokana na jinsi alivyokuwa anaishi vizuri jamii ya kule pamoja na Kanisa la mt. Thadei waliomba azikwe jirani basi familia ikakubali kumzika kwenye makaburi ya Kinyerezi Zimbili.

Hiyo yote kuonyesha jinsi gani mzee wetu alivyokuwa anakubalika kwenye jamii licha ya kutokuwa na utajiri wa mali na pesa. hakika nimejifunza mengi kwenye huu msiba wa mzee wetu.

Pole sana kwa familia na shukran kwa waliojitoa.

Pumzika kwa amani Mzee Shigella
Poleni sana kwa msiba.
 
Kaka! Kila mtu akianza kuleta misiba ya kwao itakuwaje?
 
Makaburi ya Segerea ndiyo yamejaaa , tulimpumzisha kwenye makaburi ya Kinyerezi Zimbili, sema yanaelekea kujaa ila ukiwa na issue sema nikupe contact !!!!!!!! bado kuna nafasi 4 .
La hadi makaburini kuna madalali nchi hii kiboko
 
Huyo Mzee ni Mstaafu (82) alikuwa anaishi Ukonga stakishari, mie ni mjomba wangu na yeye ndiyo alikuwa Mzee wa familia kwa ukoo wa Majebele kwahiyo kila jambo mfano, harusi, misiba nk lazima ash.

Ndugu na jamaa walichanga kwenye msiba mpaka kamati ikataka kusitisha zoezi la kupokea rambirambi, hakika watu walijitoa sana.

Changamoto ilikuwa wapi azikwe, wengi wana ndugu walipendekeza Kinondoni na hata kamati ilipendekeza Kinondoni ila kutokana na jinsi alivyokuwa anaishi vizuri jamii ya kule pamoja na Kanisa la mt. Thadei waliomba azikwe jirani basi familia ikakubali kumzika kwenye makaburi ya Kinyerezi Zimbili.

Hiyo yote kuonyesha jinsi gani mzee wetu alivyokuwa anakubalika kwenye jamii licha ya kutokuwa na utajiri wa mali na pesa. hakika nimejifunza mengi kwenye huu msiba wa mzee wetu.

Pole sana kwa familia na shukran kwa waliojitoa.

Pumzika kwa amani Mzee Shigella
Kwa makala haya ya hiki kifo serious....

Nilichojifunza ni kwamba kama huna hela wala mali au power then "wema" na "unyenyekevu" kwa wanadamu ndio your currency

Wema na Unyenyekevu wanaotaka wanadamu ni wewe uache kua yourself uingie kwenye sekta ya kua mnafiki uuvae uhusika wanaoutaka wao kuwaridhisha wao

Huo upumbavu I'm sorry, I will never do, instead nakusanya mali za kutosha which guarantees respect regardless!

In this life its even harder turning an actor without movie roles

I will be me, myself, and if you got problem with it, then sorry I cant help your feelings, but u will respect me regardless!
 
Kwa makala haya ya hiki kifo serious....

Nilichojifunza ni kwamba kama huna hela wala mali au power then "wema" na "unyenyekevu" kwa wanadamu ndio your currency

Wema na Unyenyekevu wanaotaka wanadamu ni wewe uache kua yourself uingie kwenye sekta ya kua mnafiki uuvae uhusika wanaoutaka wao kuwaridhisha wao

Huo upumbavu I'm sorry,I will never do,instead nakusanya mali za kutosha which guarantees respect regardless!

In this life its even harder turning an actor without movie roles

I will be me,myself,and if you got problem with it,then sorry I cant help your feelings,but u will respect me regardless!
Mkuu,

Nakuelewa. Mimi pia napenda kujitambua na kufanya ninachotaka, si ninachopangiwa na jamii.

Lakini pia huoni kwamba inawezekana kabisa mtu akalelewa katika jamii inayofundisha wema na unyenyekevu, na yeye akaukubali wema na unyenyekevu kifalsafa, si kwa sababu anataka kuifurahisha jamii, si kwa sababu anataka sifa, bali kwa sababu yeye mwenyewe ameukubali wema na unyenyekevu kifalsafa?

Na ikiwa hilo linawezekana, huoni kwamba hapo mtu kuwa na social currency kutokana na wema na unyenyekevu hakuna conflict kati ya jamii inachotaka na anachotaka yeye?

Yani, huoni kwamba mtu huyo, he doesn't have to act or be a hypocrite to get that social currency? Huoni kwamba he can get that currency just by being his true self?
 
Pole kwa wafiwa, ila huu ushamba na ulimbukeni wa ''live streaming'' ya mazishi ni ujinga uliopitiliza. Mazishi ni kitu cha private hakitakiwi kuonyeshwa kwenye internet. Huu ulimbukeni unaivamia jamii yetu kwa kasi kabisa.
 
Mkuu,

Nakuelewa. Mimi pia napenda kujitambua na kufanya ninachotaka, si ninachopangiwa na jamii.

Lakini pia huoni kwamba inawezekana kabisa mtu akalelewa katika jamii inayofundisha wema na unyenyekevu, na yeye akaukubali wema na unyenyekevu kifalsafa, si kwa sababu anataka kuifurahisha jamii, si kwa sababu anataka sifa, bali kwa sababu yeye mwenyewe ameukubali wema na unyenyekevu kifalsafa?

Na ikiwa hilo linawezekana, huoni kwamba hapo mtu kuwa na social currency kutokana na wema na unyenyekevu hakuna conflict kati ya jamii inachotaka na anachotaka yeye?

Yani, huoni kwamba mtu huyo, he doesn't have to act or be a hypocrite to get thst social currency? Huoni keamba he can get thst currency just by being his true self?
Hili nalo ni neno. Mtu anaweza kuwa alivyo siyo kwa sababu ni unafiki wa kufurahisha watu bali ndivyo anavyotaka na ku-enjoy.
 
Pole kwa wafiwa, ila huu ushamba na ulimbukeni wa ''live streaming'' ya mazishi ni ujinga uliopitiliza. Mazishi ni kitu cha private hakitakiwi kuonyeshwa kwenye internet. Huu ulimbukeni unaivamia jamii yetu kwa kasi kabisa.
Live streaming siioni kama ni ulimbukeni. Ni tukio la mara moja wahusika wakuu wengine hawapo hivyo tukiamua kuwaonyesha kinachoendelea sio vibaya.
Kama ingekuwa ni ulimbukeni hata jeneza tungetoa hivyo, hata mortuary tungeita hivyo
 
Ni ulimbekeni tena ushamba mkubwa. Kwani walioko mbali hawawezi kuona recorded video? Angalia nchi zilizoendelea zenye watu wastaarabu huu ujinga hawafanyi na mazishi mengi husema ni private matter. Kwetu tumefikia hadi ukatili wa kuingia wodini kuhoji wagonjwa walio taabani eti ni ''waandishi wa habari''. Ujinga.
 
Hili nalo ni neno. Mtu anaweza kuwa alivyo siyo kwa sababu ni unafiki wa kufurahisha watu bali ndivyo anavyotaka na ku-enjoy.
Na mara nyingi ukiona mtu kakubalika na watu wengi sana inakuwa ni hivyo.

Hawa wa ku fake na ku act tu kuna sehemu movie inawashinda. Halafu watu wanaona huu unyenyekevu ni wa kimkakati tu.

Na kuna kitu kimoja wengi hawaelewi.

Kuwa mnyenyekevu maana yake si kukubali kila kitu unachoambiwa, unaweza kuambiwa kitu, hukubaliani nacho, ukakipinga kinyenyekevu na kujenga ushawishi mpaka huyo unayempinga mwenyewe akakukubali kwamba huyu jamaa ni very smart.

Sasa, ukishaweza kufika level hiyo, kuwa mnyenyekevu maana yake si kukubali kila kitu unachopangiwa na jamii, bali kuwa nabuwezo wa kukataa kinyenyekevu na pengine kujenga ushawishi mkubwa kwa kutumia akili pale wengine wanapotumia fedha nyingi.
 
Pole kwa wafiwa, ila huu ushamba na ulimbukeni wa ''live streaming'' ya mazishi ni ujinga uliopitiliza. Mazishi ni kitu cha private hakitakiwi kuonyeshwa kwenye internet. Huu ulimbukeni unaivamia jamii yetu kwa kasi kabisa.
Mkuu,

Watu wana uhuru wa kuzika wanavyotaka.

Mwaka jana kuna dada yetu mmoja alifariki viunga vya Washington DC, akazikwa huku kwa sababu aliagiza hivyo. Alikuwa kashaanzisha familia huku na watoto wake wako huku akasema anataka kuzikwa huku Marekani.

Kwenye mazishi walifanya livestreaming na rafiki zake walifuatilia dunia nzima.

Kuna mdogo wake mmoja alifuatilia kutoka Mwananyamala akasema alifarijika sana na kujiona kama amemzika dada yake.

Mimi kuna ndugu wamefariki kipindi cha pandemic sikuweza kuja nimeona mtandaoni.

Kuna videos mpaka Youtube msiba unasikia umeshapita, lakini unapata nafasi ya kuangalia ndugu yako alivyozikwa.

Hususan kwa watu tulio mbali na nyumbani ambao hatuwezi kuja kila msiba inatusaidia sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom