MzeeKipusa
JF-Expert Member
- Feb 10, 2023
- 2,705
- 4,967
Yani unakua tajiri halafu unaacha vitoto viwili tu na mjane mmoja? HII NI MAAJABU! Huenda Marehemu alikua muoga sana wa maisha!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
RIP Bilionea Makilagi
Mazishi ya msiba wa Said Kate Makilagi wa Musoma Food, vilio mjini Shinyanga
Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza kuaga mwili wa Mfanyabiashara wa nafaka mkoa wa Shinyanga Said Makilagi maarufu Musoma Food aliyefariki dunia ghafla jijini Mwanza Jumatatu Aprili 3,2023 akiwa Hotelini.
Mazishi ya marehemu Said Kate Makilagi yamefanyika leo Alhamisi Aprili 6,2023 nyumbani kwake Kambarage Mjini Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya familia tarehe 27.5.2021 Said Makilagi alipata ajali ya gari huko Mpanda Rukwa akapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu na kutokana na afya yake kutetereka alikuwa akipatwa matibabu Bugando, Kenya na India.
Hata hivyo kutokana na matibabu hayo alipata nafuu na kwa nyakati tofauti alikuwa anapata maumivu ya kichwa na mnamo tarehe 3.4.2023 akiwa jijini Mwanza aliugua ghafla jijini akafariki dunia.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Musoma Food, Said Kate Makilagi alizaliwa 01.06.1967 alifariki dunia 03.04.2023, ameacha mjane na watoto wawili
Salaam za rambirambi zamiminika toka kila kona ya nchi zimetolewa, Bwana Alitoa na Bwana Ametwa jina lake lihimidiwe
View attachment 2580954
Pia ni supplier unga kwa kampuni ya bia serengetiNi mfanyabiashara mkubwa wa nafaka na bilionea ambaye alipata tenda za kusambaza mchele, unga, maharagwe kwenye kambi za wakimbizi kuanzia Tanzania, Sudani, Congo kwa miaka mingi amekua akifanya kazi na WFP, kwa mtu wa mazao yeyote Tanzania lazima umfahamu huyu mwamba, wa Musoma Food aliejikita Shinyanga kulipo na viwanda vyake
Nani huyo kafa hapo ngaramtoniTunaenda wa ngaramtoni tulioko arusha,,,ni pombe tuu
Bila kusahau pilipili ya kung'atia nyamaApumzike kwa Amani Maskini naona wanajiandaa kwenda kula ubwabwa na chai