TANZIA Pumzika kwa amani Said Makilagi, mfanyabiashara mkubwa wa nafaka na mmiliki wa Musoma Food

TANZIA Pumzika kwa amani Said Makilagi, mfanyabiashara mkubwa wa nafaka na mmiliki wa Musoma Food

Yani unakua tajiri halafu unaacha vitoto viwili tu na mjane mmoja? HII NI MAAJABU! Huenda Marehemu alikua muoga sana wa maisha!
 
RIP Bilionea Makilagi

Mazishi ya msiba wa Said Kate Makilagi wa Musoma Food, vilio mjini Shinyanga


Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza kuaga mwili wa Mfanyabiashara wa nafaka mkoa wa Shinyanga Said Makilagi maarufu Musoma Food aliyefariki dunia ghafla jijini Mwanza Jumatatu Aprili 3,2023 akiwa Hotelini.

Mazishi ya marehemu Said Kate Makilagi yamefanyika leo Alhamisi Aprili 6,2023 nyumbani kwake Kambarage Mjini Shinyanga.

Kwa mujibu wa taarifa ya familia tarehe 27.5.2021 Said Makilagi alipata ajali ya gari huko Mpanda Rukwa akapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu na kutokana na afya yake kutetereka alikuwa akipatwa matibabu Bugando, Kenya na India.


Hata hivyo kutokana na matibabu hayo alipata nafuu na kwa nyakati tofauti alikuwa anapata maumivu ya kichwa na mnamo tarehe 3.4.2023 akiwa jijini Mwanza aliugua ghafla jijini akafariki dunia.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Musoma Food, Said Kate Makilagi alizaliwa 01.06.1967 alifariki dunia 03.04.2023, ameacha mjane na watoto wawili

Salaam za rambirambi zamiminika toka kila kona ya nchi zimetolewa, Bwana Alitoa na Bwana Ametwa jina lake lihimidiwe

View attachment 2580954


Ni ipi tarehe sahihi ya kuzaliwa kwake kati ya 1.6.1967 uliyoandika na 1.6.1970 iliyoandikwa kwenye hilo bango hapo msibani?
 
Ni ipi tarehe sahihi ya kuzaliwa kwake kati ya 1.6.1967 uliyoandika na 1.6.1970 iliyoandikwa kwenye hilo bango hapo msibani?
Arovera yuko sahihi sababu Msalaba wameandika KUZALIWA 01.06.1967
Screenshot_20230408-175628_Edge.jpg
 
Ni mfanyabiashara mkubwa wa nafaka na bilionea ambaye alipata tenda za kusambaza mchele, unga, maharagwe kwenye kambi za wakimbizi kuanzia Tanzania, Sudani, Congo kwa miaka mingi amekua akifanya kazi na WFP, kwa mtu wa mazao yeyote Tanzania lazima umfahamu huyu mwamba, wa Musoma Food aliejikita Shinyanga kulipo na viwanda vyake
Pia ni supplier unga kwa kampuni ya bia serengeti
 
Back
Top Bottom