Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!


Wabunge wanalipaje kodi kwenye mishahara yao
 

Hesabu za haraka haraka, kama ongezeko hilo la mshahara limesababisha ongezeko hilo la kodi basi mshahara wako wa mwanzo ulikuwa ama ni TZS 800,000 kamili au zaidi ya apo.

Kumbuka kiwango cha chini elekezi kutoka serikalini ni TZS 170,000.
Unapaswa kumshukuru Mungu kwa kipato hiki badala ya kuanza kulalamika, kuna watanzania mamilioni ambao hawapati hata shilingi kwa mwezi, si wafanyakazi, si wakulima, si wajasiriamali, si lolote, wako kama vile wanasindikiza wenzao (katika ulimwengu huu wa fedha na tamaa).

Nachokushauri, kwa ongezeko hili, na Mabenki outomatically yameongeza kiwango yaliyotayari kukukopesha, usiwasikilize, hao ni wabaya kuliko hata serikali.usiingie tamaa ya kufanya biashara kwa sababu unaweza kukopa pesa nyingi, wala usiwatenge wenzako uliowapita kipato na usijiunge na wale uliowafikia kipato katika matumizi.

Ongeza bidii kazini, inshalah, labda Mshahara utaongezeka tena muda si mrefu.
 

Kupambana nayo ni kuiondoa kwa box la kura,methods nyingine itashindikana kwani wanafiki na wachumia tumbo wale fisi kwenye ngozi ya kondoo ni wengi kati yetu.
 
Wabunge wanalipaje kodi kwenye mishahara yao

Hivi wabunge wanalipwa mshahara? wamehajiriwa na nani? wanafanya kazi gani? Kazi hiyo inakidhi viwango vya kazi ambazo kipato chake kinakatwa kodi?
 
Unakata kodi kwenye mshahala arafu ukinunua redio wanakata.TV wanakata ,sukari supermarket wanakata. huu unyonyaji

Decoder wanakata, umeme unaotumia kuangalia hiyo TV wanakata, kodi ya mjengo wanakata, hadi jeneza utalozikwa nalo wanakata.
 
Hivi wabunge wanalipwa mshahara? wamehajiriwa na nani? wanafanya kazi gani? Kazi hiyo inakidhi viwango vya kazi ambazo kipato chake kinakatwa kodi?

PAYE maana yake nini?
Mimi hata pesa yangu ya likizo nakatwa kodi.
 
Kitu ambacho wafanyakazi wangeshauri TRA ni kuwarejeshea kiasi kinachozidi kwa makati yao ya kodi kwa mwaka. Viwango vya kodi kwa mwaka, kwa hiyo mara nyingi wanapokata Kila mwezi mfanyakazi uchamgia zaidi ya kiwango alichotakiwa kulipa kwa mwaka. Bahati mbaya Tanzania hakuna utaratibu wa kufaili marejesho ya kodi Kila mwaka kwa walipa kodi wafanyakazi, hii ingeonekana.
 


Ndo maana watu woote waliochangia quote yako wanakudharau na kukuona you are just a junk, your brain has elapsed beyond scrap value.
-Yaani anayekusanya kodi hatakiwi kuitumia vzr kwa manufaa asubiri walionionywa/kuibiwa walie ndo atekeleze wajibu wa matumizi sahihi.Mi nilidhani huwa unaongea ujinga kwenye siasa za utoto kumbe haupo serious hata cku moja .ji.nga wewe.
-Kwanini liwe jukumu letu wafanyakazi kuwataka walipe kodi hao wanasiasa mbona wasiwe na internal push za kuwafanya walipe voluntarily.

-Uchumi utayumba kwa mlalahoi kama mimi kutolipa kodi lakini tycoon kama African Barick au AbduTembo KinaFaru asipolipa uchumi bado utakuwa stable!Shame upon your face subiri sikukuu yako 1st April utapata zawadi nyingi za midoli nyambaf.
 

kulipa kodi si tatizo hata kidogo.tatizo lililopo ni kiwango cha kodi tunachokatwa wafanyakazi.makato ya kodi hayana uwiano na kile mfanyakazi anachopata kwa mwezi.kwa mfano:wafanyabiashara wanalipa kodi kwa mwaka lakini hakuna uwiano na kile wanacholipa wafanyakazi kwa mwezi.achilia mbali wanasiasa wetu wasiokatwa kodi kwenye mamijishahara yao ya kifisadi!
 

Hakuna aliyepinga kulipa kodi kila raia au Mfanyakazi mwenye nia njema na nchi yake hawezi kutaka kuondolewa kodi katika Mshahara au biashara yake, hapa tunachojadili ni kwa nini Wafanyakazi wanalipa kodi kubwa kuliko mtu yeyote katika nchi hii kwani kulipa 27% au 30% huu ni uonevu. Tukiangalia kwa makini Mfanyakazi analipa kodi za ziada katika maeneo yafuatayo:-
1. Mshahara wake unakatwa kodi
2. Akinunua bidhaa madukani analipia na kodi ya muuza duka anayotakiwa kuwalipa TRA
3. Akisafiri analipa kodi ambayo ipo ndani ya nauli anayolipa
4. Akinunua LUKU analipa kodi ikiwemo na ile ya REA
Kwa hiyo mtu anayenyonywa na asiyethaminiwa katika nchi hii ni Mtumishi wa Umma ambae Serikali haitaki kumuongezea mshahara ila kumnyonya kodi ndio wa kwanza kufanyiwa hivyo.
 
PAYE maana yake nini?
Mimi hata pesa yangu ya likizo nakatwa kodi.

PAYE ni kodi wanayokatwa wafanyakazi na Muajiriwa wao kutoka kwenye kipato walichokubariana katika Mkataba wa Kazi, sasa wabunge wanamkataba na nani? Bunge?Serikali? Mkataba wa kufanya nini?
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote. Vip kuhusu hao wanaolipwa mamikioni ya kodi zetu halafu hawakatwi kodi!? Mimi nadhani kuwa kiongozi ni kuongoza kwa mfano, sasa jnawezaje kuwa na uthubuti wa kukemea wakwepa kodi wakati wewe mwenyewe hulipi? Viongozi wetu waache usanii, walipe kodi kama wanania njema na watanzania hata kama sheria zetu ni za kikoloni.
 

Hiki kilichokutokea inawezekana kabisa katika hii Serikali haina viwango vya % vya ukataji wa kodi, ebu angalia na huu mfano

Mtumishi analipwa - 1,133,200/= lakini Kodi(Income Tax) ni 221,361.20 ambacho ukitafuta asilimia inakuwa 19.53% sasa inakuwaje mwingine akatwe 27, 30 na mwingine 19(20) kwa nini hakuna uwiano sawa?
 
Kwa lugha rahisi, mtu asiyelipa kodi hawezi kujua uchungu wa kuilipa na hata kuitumia...!! Government officials should pay tax.. Pia matumizi ya kodi yawe transparent huku vipaumbele vikiwekwa mbele. Tuna matatizo mengi ambayo walipa kodi tungependa kuona yakipewa msisitizo... Na sio kodi kuelekezwa kwenye starehe za watu ambao baadhi yao hawana impact hata kwenye maendeleo ya nchi zaidi ya kuirudisha tu nyuma...

Hv wale waliokuwa wanapinga wananchi kujua salary za viongozi...are you there..?? Are you paying taxes..??
 

ZeMarcopolo usizungumze kinafiki kwa sababu unajua matuumizi mabaya ya kodi za Walalahoi zinavyotafunwa na wao ambao hata chembe ya pato lao halilipiwi kodi!.

ZeMarcopolo ningekuona wa maana kama ungeweka chembe za aibu pembeni na kuishinikiza viongozi wote wasiokatwa kodi kwenye mishahara yao waaanze kukatwa kodi ili pato la kodi liongezeke.
 
Last edited by a moderator:

Jitahidi kusoma vizuri post yangu na kuielewa. Unarudia kilekile nilichoandika...
 

ni kweli njia iliyopo kila mwajiliwa alipe kodi kwa kutumia tin number yake kusudi viwango vinavyozidi watu warudishiwe pesa yao kwani hilo ni jasho lao.
 
Sawa nikatwe kodi...lakini basi nikiugua nikienda hospital nipate vipimo vya kunipima japo kwa kulipia, dawa ziwepo hata km ni za kununua, mwanangu pale st kayumba asilipe kitu manake kodi ninayo katwa kwa mwezi nalipa mishahara ya waalimu km 3 with average salary ya Tshs 350, 000/, wale vibaka wakinitembelea ninapoenda kutoa taarifa polis wale polis wasinidai karatas ya kuandikia maelezo....n the like
 

Kuwa Mfanyabiashara nikufundishe jinsi yakukwepa suala hilo ama soma Vitabu vya Mwandishi Robert Kiyosaki upate maarifa zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…