Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

Kodi ni kwa ajili ya wanyonge tu? raisi, makamu wa raisi, waziri mkuu, mawaziri, wabunge na wakuu wa Mikoa na wilaya hawakatwi payee! Hii ni haki? kweli inauma sana sana jamani.:frusty:

Si kweli kwamba wafanyakazi ambao kwa kiasi kikubwa mna elimu kwamba mnaumia kwa kodi la sivyo mngechukua hatua kali inaonekana mmesoma ila tatizo upeo wa kiakili nyie wenyewe na viongozi wa TUCT.
 
Kama kwa mwaka wanapunguza 1% kwhyo mpaka bajeti ya 2018/2019 ndio itafikia single digit 9% endelea kufanya kazi tu kupata nafuu ya (1900 x 4=7600)

tanzania hapafai kuishi. Unaongozwa na mandondocha yani ni full kutabika!
 
kama kweli wamepunguza asilimia 1 wafanyakazi kwa pamoja kuna haja ya kuitoa serikali hii madarakani kwa kuinyima kura ccm

Wafanyakazi wa tz kama mazezeta ndio maana viongozi na wanasiasa huwafanya watakavyo
 
Wafanyakazi wa tz kama mazezeta ndio maana viongozi na wanasiasa huwafanya watakavyo



Umewahi kuona au kusikia kodi wanazokatwa wafanyakazi kwa nchi zilizoendelea?
 


Unataka waingie chadema wanufaishe kabila lao?
 
Umewahi kuona au kusikia kodi wanazokatwa wafanyakazi kwa nchi zilizoendelea?

Umewahi kuona au kusikia jinsi hizo kodi wanazokatwa wafanyakazi zinavyofanyiwa kazi kwa manufaa ya nchi zao?
 
hatari sana. kwa kifupi, mwenye mşhahara wa tshs 700,000 anamzidi kwa mbali sana mwenye mshahara wa tshs 750,000 kwa take home, kisa kodi!!!

Ndio maana yake mkuu, atakuwa group 4. Hivyo atalipa kodi ndogo.
 

mawazo ya kimasikini
 

Mkuu umesomeka vizuri tu.

Na mimi labda hujasoma post yangu ya mwanzo.

Hata mimi nimesema kuwa serikali haikumsaidia chochote mwananchi wa kawaida ktk hili.
Lkn kumbuka kwa serikali yenyewe hizi ni pesa nyingi mno.
Na hatuna budi kwenda hivo hivo tu!

Unless serikali iongeze kodi kwa hayo makampuni makubwa sisi wanyonge tutaendelea kuumia tu!

Hakuna njia nyingine.
 
Heshima mbele mkuu
Tupo pamoja

Mie nadhani serikali isingepunguza hii paye baadala yake ,hilo punguzo ambalo kwa upande wa serikali ni pesa nyingi kwa kuwa zinakuswanywa kutoka kwa wengi, hizi zingiweza kusaidia kupunguza vifo vya akina Mama na watoto wanopoteza maisha wakati wa kujifungua .Mbaya zaid hawa wakina mama wanapokufa wanaacha pengo kubwa sana nyuma yao

Hili punguzo alikufikiriwa vizuri ,limekaa kisiasa zaidi
 
tanzania hapafai kuishi. Unaongozwa na mandondocha yani ni full kutabika!

Kenyatta Sr aliwahi kumuambia Nyerere kwamba anaongoza MAITI! ni kweli kwamba watanzania wengi wana akili kama za maiti ndiyo maana kila mwaka huwachagua CCM ili wamalizie kazi ya kuwazika!
 
Umewahi kuona au kusikia kodi wanazokatwa wafanyakazi kwa nchi zilizoendelea?

hivi wewe pimbi kwanini unapenda kutuvurugia mijadala na kututafutia ban? kwani tanzania ni NCHI ILIYOENDELEA? na unajua wafanyakazi ktk nchi zilizoendelea wanalipwa mshahara sh ngapi? kwanini unafananisha vitu ambavyo havifanani?
 

sasa kwanini hawafanyi hivyo? wewe unataka tuendelee kuvumilia mpaka lini? kwanini humuambii haya katibu wako na kila siku unakutana naye hapo lumumba? ungependa watanzania waendelee kuteseka hadi Yesu atakaporudi?
 
Kenyatta Sr aliwahi kumuambia Nyerere kwamba anaongoza MAITI! ni kweli kwamba watanzania wengi wana akili kama za maiti ndiyo maana kila mwaka huwachagua CCM ili wamalizie kazi ya kuwazika!
Kwann hutumii kichwa kufikiri? Kwann umechangia ukurasa mzima peke yako?
 
Kwann hutumii kichwa kufikiri? Kwann umechangia ukurasa mzima peke yako?

usitishwe na kiasi cha michango yangu bali unapaswa kuzingatia theme ya yaliyomo...hilo ndilo suala la msingi. serikali yako imeonyesha udhaifu mkubwa sana wa kiuongozi.
 
Kweli hii ni dharau ina maana mkuu wa kaya alikuwa anatafuta umaarufu wa kupigiwa makofi ama wachumi wake hawakumshauri vizuri . Kama mshahara wa mfanyakazi ni 80000 na PAYE itakuawa 1200 kwa 15% na kama atakuwa amepunguza 1% hivyo atakuwa amepunguza tshs 12. Sasa swali linakuja kama angeogeza mshahara kweli angeongeza hicho kiasi cha pesa kwenye mshahara?
 

mkuu, uongozi wa nchi hii ni majanga makubwa sana. ubovu wa uongozi unaifanya safari ya kuelekea 2015 ionekane kama safari ngumu ya Musa kuwatoa watu wake utumwani kutoka Misri kuelekea Kaanani--ni safari ndefu na yenye misukosuko kibao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…