Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

ni wakati wa kushinikiza ili tupatiwe ufafanuzi wa kodi tunazolipa.isije ikawa tunalipa kodi mara mbili au zaidi katika suala moja yaani umeme!

Amini usiamini, kodi nyingi tulizipazo hazina tija kwetu kwani zinakuwa ni kwa ajili yao viongozi. Yaani ni vilivyopangwa tayari. Jaribu kujiuliza tunalipa kodi lakini bado hakuna maendeleo yeyote au hata kuonyesha tu kuwa kuna kinachofanyika katika kuleta hayo maendeleo.
 
kwa niaba ya wafanyakazi nchini napenda kuwasilisha maombi maalum ya kujua matumizi ya kodi ya PAYE kama ilivyokuwa kwa kodi mpya ya simcards.
Ni vyema tukaambiwa ni % ngapi ya PAYE inakwenda kwenye afya,elimu,miundombinu,maji,nishati n.k

Sidhani kama Serikali inajua kiasi cha pesa kinachopatikana kupitia makato haya. Nafikiri tungeanzia hapo kabla hatujajua matumizi yake!
 
Ni vema mapato ya Serikali, vyanzo vyake na matumizi yakawa wazi kwa wananchi kupitia gazeti la Serikali.
 
Hili nalo neno ... waweza kuta zinatumika kama sehemu ya budget ya viburudisho
 
Hawa Wabunge Ndio Chanzo Ilibidi Warudi Kwetu Wananchi Kabla Ya Kupitisha Hiyo Kodi Ya Simcard. Leo Nao Wanalalamika Kama Sisi.ni Bora Wakatwe Mishahara Kufidia Hiyo Kodi

ifanya fyongo wanakatwa mishahara, mrema alishadadia hili la DED, sasa ni zamu yako kushadadia wabunge mkatwe mishahara kwa kuborongo kiasi hicho.[/QUOTE
 
kwa niaba ya wafanyakazi nchini napenda kuwasilisha maombi maalum ya kujua matumizi ya kodi ya PAYE kama ilivyokuwa kwa kodi mpya ya simcards.
Ni vyema tukaambiwa ni % ngapi ya PAYE inakwenda kwenye afya,elimu,miundombinu,maji,nishati n.k

Mkuu naddhani unahitaji somo la utaratibu wa mapato na matumizi ya serikali. Pesa zote zinazokusanywa na serikali toka vyanzo mbalimbali kama vile kodi ya PAYE, ushuru wa forodha, nk. huwekwa kwenye fuko kuu la serikali (consolidated Fund) na toka humo basi matumizi hufanywa. Angalia mapato na matumizi ya serikali (Budget).
 
Kwa hiyo kodi hii ya simcard haitaingizwa kwenye hilo fuko?Na huo umeme vijijini tutachangia kwa miaka mingapi?
Naomba ufafanuzi au kama unavyoita 'somo'
 
mishahara,safari za raisi na msafara wake,kununulia V8 na mafuta yake,kununua fleet ya BMW,seminar,warsha,makongamano na mengineyo mengi tu,pitia budget ya serikali
 
Mkuu naddhani unahitaji somo la utaratibu wa mapato na matumizi ya serikali. Pesa zote zinazokusanywa na serikali toka vyanzo mbalimbali kama vile kodi ya PAYE, ushuru wa forodha, nk. huwekwa kwenye fuko kuu la serikali (consolidated Fund) na toka humo basi matumizi hufanywa. Angalia mapato na matumizi ya serikali (Budget).
kwa maana hii serikali haijui kuna wafanyakazi wangapi na kodi wanayotakiwa kukatwa,yaani ni kanyaga twende tu.hebu nipe ufafanuzi mkuu
 
Mkuu usijiumize kichwa, usitegemee Pinda atakuambia kitu kilichokwenda shule hata siku moja....naye yule ni janga lingine la taifa kwani hajuwi akifanyacho na haelewi nini anachokisema. Kwa kifupi, pole sana.

Naona unatafuta kupigwa. Liwalo na liwe.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Kwa hiyo kodi hii ya simcard haitaingizwa kwenye hilo fuko?Na huo umeme vijijini tutachangia kwa miaka mingapi?
Naomba ufafanuzi au kama unavyoita 'somo'

Mkuu haya mambo yanahitaji darsa! Mkuu kwa kujisomea kwangu najua fuko kuu huwa liko hazina. Pesa huingia huko na kugawanywa kulingana na budget. Lakini pia katika pita pita yangu na soma soma huku na huku nikakutana na kitu inaitwa ring fenced funds! Nikajijuza kwamba hizi ni pesa ambazo huwa zinatozwa kwa kazi maalumu na zikiingia huko fukoni hutolewa kama zilivyo na kwenda kufanya kazi husika. Mfano mzuri ni tozo mafuta kwa ajili ya barabara. Nasikia hizi huingia fukoni na kisha kutolewa kwenda Bodi ya Mfuko wa Barabara kwa ajili ya matengenezo ya barabara.
 
WanaJF hata kama jukwaa hili la siasa sio mahali pake, naomba tujadili hapa suala hili maana wizi wa serikali kwa wafanyakazi wa nchi hii umekithiri. Mi naumia sana maana nilipokea barua ya kuongezewa mshahara kwa sh 490,000/-, lakini kodi iliyoongezeka kwenye mshahara wangu mpya ni 132,300/-. Ukizidisha na hesabu kwa asilimia hii ni 27% ya kodi kwa nyongeza hiyo ya mshahara, ina maana nimeongezewa mshahara kwa sh 357,700/- na si 490,000/-. Hawa wenyewe wakubwa hawalipi kodi, hata wabunge, na wanazidi kutunyonya tu. Wafanyabiashara hawalipi kodi kwa asilimia hiyo ya faida zao, na wanaweza kukwepa. Naomba tujadili na tupate njia ya kupambana na serikali hii inayotuibia wananchi wake bila aibu.
 
Naunga mkono hoja huu wizi wa serikali. Mfano anayepokea zaidi ya laki saba analipa kodi asilimia 30 ya fedha inayozidi. Hatukatai kulipa kodi lakini basi kuwe na usawa. Wafanyabiashara na viongozi wa juu serikalini pia walipe kodi. Sio wananyonywa tu wanaofanya sekta binafsi.
 
Kuhusu kodi.

Kodi ni msingi wa maendeleo. Kulipa kodi ni jambo la kizalendo.

Wafanyakazi wasililie kufutiwa kodi. Wafanyakazi walilie kuona kodi yao ikitumiwa kwa manufaa yaliyodhamiriwa.

Wale wasiolipa kodi wasiigwe. Wafanyakazi wasitake kusamehewa kama wanasiasa. Wafanyakazi wasisitize kuwa wanasiasa nao walipe kodi.

Kila mtu akikimbia kodi, uchumi utazorota.
 
Mkuu serikali kandamiz ndivyo zilivyo , bado wameona kodi hizo bado hazitoshi wameamua kufuta increment ya mwaka katika mishahara ambayo ipo kisheria, mfano siku hizi watu wote wa tgs D wameachwa D1 hakuna kwenda D2 hatA kwa miaka zaidi ya 5. huu ni ukandamizaji wa waziwazi
 
Kuhusu kodi.

Kodi ni msingi wa maendeleo. Kulipa kodi ni jambo la kizalendo.

Wafanyakazi wasililie kufutiwa kodi. Wafanyakazi walilie kuona kodi yao ikitumiwa kwa manufaa yaliyodhamiriwa.

Wale wasiolipa kodi wasiigwe. Wafanyakazi wasitake kusamehewa kama wanasiasa. Wafanyakazi wasisitize kuwa wanasiasa nao walipe kodi.

Kila mtu akikimbia kodi, uchumi utazorota.

Unakata kodi kwenye mshahala arafu ukinunua redio wanakata.TV wanakata ,sukari supermarket wanakata. huu unyonyaji
 
Kuhusu kodi.

Kodi ni msingi wa maendeleo. Kulipa kodi ni jambo la kizalendo.

Wafanyakazi wasililie kufutiwa kodi. Wafanyakazi walilie kuona kodi yao ikitumiwa kwa manufaa yaliyodhamiriwa.

Wale wasiolipa kodi wasiigwe. Wafanyakazi wasitake kusamehewa kama wanasiasa. Wafanyakazi wasisitize kuwa wanasiasa nao walipe kodi.

Kila mtu akikimbia kodi, uchumi utazorota.

Upo sahihi Mkuu kwa kuwa wao wanamasoko yao ya bei nafuu, na pia wanapata faida kuliko wafanyabiashara, ni kweli Tanzania itajengwa na wanaonyonywa kwenye mishahara na sio makampuni ya madini na mengine mengi. Hongera mkuu
 
Kuhusu kodi.

Kodi ni msingi wa maendeleo. Kulipa kodi ni jambo la kizalendo.

Wafanyakazi wasililie kufutiwa kodi. Wafanyakazi walilie kuona kodi yao ikitumiwa kwa manufaa yaliyodhamiriwa.

Wale wasiolipa kodi wasiigwe. Wafanyakazi wasitake kusamehewa kama wanasiasa. Wafanyakazi wasisitize kuwa wanasiasa nao walipe kodi.

Kila mtu akikimbia kodi, uchumi utazorota.

Kwa nini wanasiasa wasilipe kodi voluntarily badala ya kusubiri wafanyakazi wasisitize?
 
Back
Top Bottom