Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

Haya majamaa akina muongo,mugimwa,kiwete,savimbi,kinana lager,mzee wa gombe na wengineo ni janga la kitaifa!
 
Wana JF,

Kuna mambo ya Kushangaza sana, eti kodi imepungua kwenye Mshahara kwa TSH. 2000/= kwa Mfanyakati. Eti kuna watu wanakaa asubuhi hadi jioni ohh Serikali imepunguza kodi kwenye Mishahara ya wafanyakazi hivi kweli? Waziri anasimama kabisa bungeni kutangaza punguzo la shilingi elfu mbili? Rais anakwenda kwenye sherehe ya wafanyakazi na kutangaza kwa mbwembwe zote eti kapunguza kodi kumbe ni SH elfu mbila hana hata aibu.

Just imagine wamepandinsha kodi kwenye mafuta na sasa kila kitu kimepanda kwa kati ya TSH 100/= na 200/= huku ukipunguza kodi kwa Tsh BK 2.

Hii inatia aibu kwa CCM. Wafanyakazi amkeni CCM haitujali kabisa.
mimi pia nashindwa kuelewa.hv tanzania kuna wafanyakaz wangapi 2naolipwa poorly? 2jifunge mkanda,hakuna kupofuka,2naona saizi.changes are innevitable.2015,ccm,hawanawchao.
 
maudhi ya ujamaa na kujitegemea bado yanatawala nchi, . Chama chashika hatamu bado kina sera za tamba uone. Watanzania tutalia kama watu wa korea kaskazini waliavyo kila kukicha. yaani kila kukicha ni kupata maudhi tuu na maudhi yasiyokwisha! wahitimu wa kivukoni toka lini wakajua maswala ya kutumia kodi ya wananchi?
 
Binafsi sioni tatizo hapa, kwani kama ilivyoada ya wafanyakazi pamoja na vyama vya wafanyakazi huwa wanajipendekeza kwa serikali. Sasa kama mtu unajipendekeza kwake acha akupe za uso kavu kavu. Binafsi ningependa wafanyakazi wazidi kunyonywa na kupandishia kodi kubwa ili wajitambue na waamke kupigania haki zao.

Eti kila sherehe za mei mosi wanamualika rais akapige politiksi. Hata ningekuwa mimi kama mijitu inajipendekeza yenyewe na mimi na ichinjia baharini tu kwani si ni waoga hawawezi nifanya kitu. Tena hakuna watu majuha na majununi kama wafanyakazi na vyama vyao. Ni heri hata kungekuwa hakuna mambo ya vyama vya wafanyakazi kwani hivi vyama vipo tu kama miamvuli ya kufichia maovu ya serikali.

Chukueni hatua la sivyo mtabaki tu kama vifaranga vya kuku mkisubiri kunyonya hadi mtakapo gundua kumbe mwafanyiwa usanii kweupe mchana. Kuna haja gani ya kujipendekeza kumualika rais wa jamuhuri ya muungano awe mgeni rasmi? Hivi mnafikiri atasema nini zaidi ya kuwadanganya tu na kupiga siasa na fiksi nyingi? Hebu jaribuni ikifika siku ya wafanyakazi basi mkusanyike na kujadili dhuluma mnazofanyiwa. Fanyeni makongamano kila mwaka katika kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi. Alikeni wanaharakati, wanasiasa, na wadau wengine wengi katika hilo kongamano. Ikosoeni serikali mchana kweupe na pia muipe mapendekezo yenu mnayoona yataboresha maslahi yenu. Na kama hamuwezi basi ni bora mkanyamaza kulalamika kwani tumechoka kuwasikia kila mwaka na malalamiko haya haya.

Mwisho kabisa napenda kuchukua fursa hii kuwatakia pole kwa maumivu mnayopata kwa kodi zitozwao katika mishahara yenu. Lakini niwaache na usemi usemao kuwa wajinga ndio waliwao.

Unakosea sana kuwajumuisha wafanyakazi wote ili hali unajua wanaoandaa taratibu zote ni viongozi wa vyama vya wafanyakazi wadau wakiwa hawajui A wala B.
 
Kasungura ni kadogo itabidi tushirikiane hivyo hivyo. Tufanye kazi kwa bidii zaidi ili pato la taifa liongezeke.

Si tumeona waziri wa hela alivyofanya kwa bidii, Kaosha na sasa hivi kila kona anasifiwa.
 
Wala usijisumbue, walaumu Watz kwa kutojua kwao na kuendelea kuvumilia ujinga huo!
 
Mkuu STEIN, hawa jamaa siku zote ni watu wa kufanya mzaha na maisha yetu. Nakumbuka mwaka jana walipunguza shilingi elfu nne na mamia kadhaa tu! Sasa unapunguza elfu mbili halafu unaleta kodi ya laini ya simu ya shilingi 1,000 na mimi uliyenipunguzia hiyo 2,000 nina laini tatu za simu na kwa maana hiyo bado inabidi nitafute 1,000 nyingine ya ziada. Kazi tunayo hapa manake unafuu wa maisha haupo kabisa na badala yake ndo wanayafanya yanazidi kuwa magumu zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Mbona humalizii hiyo 2,000 kutoka kodi ya shillingi ngapi?

Mkuu FaizaFoxy,

Nachojaribu kusema ni kwamba serikali ilisema makato ya kodi yamepungua kutoka 14% hadi 13%, tulitegema tungeona effect kwenye mishahara lakini chakushangaza ndiyo hiyo bk 2 imeongezeka.
 
Wana JF,

Kuna mambo ya Kushangaza sana, eti kodi imepungua kwenye Mshahara kwa TSH. 2000/= kwa Mfanyakati. Eti kuna watu wanakaa asubuhi hadi jioni ohh Serikali imepunguza kodi kwenye Mishahara ya wafanyakazi hivi kweli? Waziri anasimama kabisa bungeni kutangaza punguzo la shilingi elfu mbili? Rais anakwenda kwenye sherehe ya wafanyakazi na kutangaza kwa mbwembwe zote eti kapunguza kodi kumbe ni SH elfu mbila hana hata aibu.

Just imagine wamepandinsha kodi kwenye mafuta na sasa kila kitu kimepanda kwa kati ya TSH 100/= na 200/= huku ukipunguza kodi kwa Tsh BK 2.

Hii inatia aibu kwa CCM. Wafanyakazi amkeni CCM haitujali kabisa.

Hayo ndiyo maisha bora kwa kila Mfanyakazi wa Kitanzania!
Walaaniwe wote walioichagua CCM mwaka 2010 na wanaotaka CCM iendelee kutawala nchi hii! Ni pumbaf tu kama Mizengo Pinda ndiye anayeweza kuwa na imani na Chama Twawala-CCM na serikali yake.Inasikit

Inasikitiisha kwamba mpaka sasa kuna Watanzania bado hawajajitambua katika nchi hii kwamba kuichagua CCM ni kujitakia misiba isiyokuwa na mwenzie. Badilikeni kifikra enyi watu ili muweze kuruhusu mabadiliko katika nji hii hatimaye ukombozi na uhuru wa kweli uweze kuwaangazia Watanzania wote.

Chagua mabadiliko. Chagua CHADEMA. Changes we can beilieve in.
 
Wana JF,

Kuna mambo ya Kushangaza sana, eti kodi imepungua kwenye Mshahara kwa TSH. 2000/= kwa Mfanyakati. Eti kuna watu wanakaa asubuhi hadi jioni ohh Serikali imepunguza kodi kwenye Mishahara ya wafanyakazi hivi kweli? Waziri anasimama kabisa bungeni kutangaza punguzo la shilingi elfu mbili? Rais anakwenda kwenye sherehe ya wafanyakazi na kutangaza kwa mbwembwe zote eti kapunguza kodi kumbe ni SH elfu mbila hana hata aibu.

Just imagine wamepandinsha kodi kwenye mafuta na sasa kila kitu kimepanda kwa kati ya TSH 100/= na 200/= huku ukipunguza kodi kwa Tsh BK 2.

Hii inatia aibu kwa CCM. Wafanyakazi amkeni CCM haitujali kabisa.

Huo ndio upeo wao wa kufikiri! Baadae wakibanwa mbavu, oooh TUNAWAJALI wapiga kura wetu! Nepi imelegea hapo!
 
Mkuu FaizaFoxy,

Nachojaribu kusema ni kwamba serikali ilisema makato ya kodi yamepungua kutoka 14% hadi 13%, tulitegema tungeona effect kwenye mishahara lakini chakushangaza ndiyo hiyo bk 2 imeongezeka.

Stein....naungana na wewe kabisa kuwa hii serikali ya CCM ni ya wahuni. Lakini unaposema kuwa imepunguwa 2000 hii ni kutokana na Mshahara wako X, kwa mtu mwingine mwenye mshahara Y inaweza kuwa imepungua 20,000. Au unaonaje?
 
Nilsena madaraja hayata hamishwa na mishahara haitapanda kama kiwete alivyoporoja mei mosi mbeya.kaka yangu alinikalipia bila hata kujenga hoja juzi alinifuta nyumbani kwangu na kuniomba msamaha kasema serikali hi ya kihuni na akadai kuwa mdogo wangu nikweli inaongozwa na wahuni.upo usanii wa hali ya juu serikalini chini ya msanii na mfalme wa wasanii jm kikwete na mavuvuzela wake mwigulu,lukuvi,wahasira na nyumambele nape
 
Na sisi wafanyakazi ni mapunguani, wakati wa uchaguzi huwa tunafanya kila mbinu kuhakikisha kuwa ccm inashinda! Acha tukome kabisa. Wameshatutumia kama ndomu sasa hatuna maana tena!
 
Tunataka kujua kodi kwenye mishahara imepungua kwa asilimia ngapi?
Kusema buku bee haieleweki vizuri

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Mkuu kamanda Mungi hiki anachokisema hapa STEIN ni kitu serious lakini naona watu wanakichukulia poa.
Ukweli ni kwamba hili punguzo la PAYE ni usanii wa hali ya juu. Kuna jamaa yangu yeye amepata nyongeza ya sh.1,900 kufuatia punguzo hili la PAYE lililotangazwa na waziri Mgimwa.

Kwakweli serikali ya ccm inazidi kuwadhihirishia watanzania jinsi ilivyo majanga. Kama wafanyakazi wa TTanzania hawataamka na kupigania haki zao ni dhahiri kuwa watendelea kukaangwa na ccm hadi wafe wzikwe. Mgaya wa TUCTA peke yake hawezi kupambana na serikali hii ya kisanii ni lazima wafanyakazi kwa unoja wao wasimame pamoja kuitaka serikali iache usanii.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom