Kalunya
JF-Expert Member
- Oct 5, 2021
- 13,322
- 18,609
Hakuna ubishi kuwa nchi za Magharibi zimejengwa kwa rasilimali kutoka mataifa mengine na watumwa. Mahitaji yaliyosababisha nchi za magharibi kutafuta makoloni na watumwa hayajakwisha hata kidogo, ile kiu ya kuzitawala nchi nyingine bado wanayo, na iko siku moja (sio mbali) watatumia NATO kutupora kwa nguvu rasilimali zetu ikiwemo ardhi ya kilimo na makazi.
Waafrika na nchi zote zilizowahi kutawaliwa na magharibi hatuwezi kubaki neutral kwenye hili kwa kisingizio cha aina yoyote ile. Kukaa kimya ni sawa na kumuunga mkono mtesi wetu ambae baada ya Urusi kuanguka atatuvamia tena.
Kila mtu mwenye akili anakumbuka namna misaada kutoka nchi za Magharibi kwenda nchi maskini na Afrika ilivyopungua ghafla baada ya USSR (Soviet) ilivyoanguka na kupelekea kwisha kwa vita baridi.
Leo hii baada ya kuimarika kwa Urusi na China kiuchumi na kijeshi magharibi wanarudi tena kwetu na misaada mbuzi ili tuwaunge mkono dhidi ya Urusi na China.
Hapa ndipo akina Nyerere, Nkrumah, Mugabe, Gaddafi, nk tunapo wamis.
Sikiliza wanaume waliobaki wanavyowaza kishujaa.
Walipora nusu ya robo tu yaani walipora asilimia 10 tu ya mali kwa maendeleo yote uyaonayo ulaya, but still 90 ya mali bado ipo nyingi tu afrika na haijatumika, ni wajibu wetu tu sisi waafrika tuzitumie tuwe na maendeleo kuwazidi wao.
Mfano mali zilizopo wilaya moja tu nchini unaweza ukalipa deni la taifa na kufanya maendeleo makubwa, tatizo utayari ndo haupo.