Putin pia amesema kuwa Urusi iko tayari kwa mazungumzo na maridhiano kuhusu Ukraine, lakini inahitaji upande wa pili uwe tayari pia. Aidha, alionyesha utayari wa kukutana "wakati wowote" na Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, ambaye ameahidi kufanikisha mkataba wa amani wa Ukraine mara baada ya kuingia madarakani Januari.
Rais Putin pia, amekiri kasoro za vyombo vya usalama vya nchi yake kufuatia mauaji ya Jenerali Igor Kirillov jijini Moscow, yaliyodaiwa kufanywa na Ukraine.
Akizungumza katika mkutano wake wa mwisho wa mwaka, Putin amesisitiza haja ya kuboresha mfumo wa ulinzi ili kuepuka makosa makubwa kama hayo.
Putin amebainisha kuwa vikosi vya Urusi vinashikilia udhibiti mkubwa katika vita lakini hajui lini Urusi itarudisha eneo la Kursk lililovamiwa na Ukraine.
Kremlin hivi karibuni iliunga mkono ukosoaji wa Trump kwa Biden kuhusu kuiruhusu Kyiv kutumia makombora ya Marekani kushambulia Urusi, hatua inayoongeza mzozo wa karibu miaka mitatu.
Chanzo: DW Kiswahili