EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,711
- 35,644
Rais Vladimir Putin ametoa hotuba kali kwa wabunge la Urusi, akithubutu nchi za Magharibi kujaribu kupambana na Moscow kwenye uwanja wa vita nchini Ukraine .
"Unaweza kusema nini, waache wajaribu," alisema kwa sauti.
Kiongozi huyo wa Urusi pia alidai kuwa upande wake ulikuwa umeanza mashambulizi yake kwa dhati.
Hoja yake ilitoa taswira ya kile kinachoweza kuwa mkakati mpana zaidi wa Moscow: kadiri vita vinavyoendelea, alidai, ndivyo itakavyokuwa vigumu kwa upande mwingine kufanya mazungumzo.
Nchini Ukraine vikosi vyake vimeendelea na msukumo wao wa polepole katika eneo la mashariki la Donetsk, ambapo shambulio la kombora lilisababisha vifo vya raia mmoja siku ya Alhamisi.
Urusi imeelekeza umakini wake kwa Donetsk baada ya kuuteka mji wa mwisho katika eneo jirani la Luhansk - ambayo, pamoja na Donetsk, inaunda Donbas.
Lakini kusini, kulikuwa na maendeleo fulani kwa Ukraine.
Bendera ya nchi hiyo ilipandishwa tena kwenye Kisiwa cha Snake, ambacho kilichukuliwa na Warusi mwanzoni mwa vita. kilipata umaarufu baada ya walinzi wa mpaka wa Kiukreni walioko kwenye kisiwa hicho kuiambia meli ya kivita ya Urusi "ipotee" - ingawa kwa lugha isiyo ya tafsida.
Vikosi vya Urusi viliondoka kisiwani hapo mwezi uliopita.