Putin: Hatutaki vita Ulaya, tuko tayari kwa mazungumzo

Putin: Hatutaki vita Ulaya, tuko tayari kwa mazungumzo

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amemueleza Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz kuwa nchi yake haitaki vita barani Ulaya. Viongozi hao wawili walikutana jana mjini Moscow ikiwa ni juhudi za hivi karibuni za kuepusha vita.

Putin ameelezea utayari wa Moscow wa kufanya mazungumzo na Marekani pamoja na Jumuiya ya Kujihami NATO juu ya masuala ya usalama.

Kauli ya Putin imezidisha matumaini ya kupungua kwa mvutano na jirani yake Ukraine na uwezekano wa uvamizi, lakini Rais wa Marekani, Joe Biden amesema hawajathibitisha madai ya Urusi na kwamba bado kuna uwezekano wa uvamizi.

Kwa upande wake Kansela Olaf Scholz amesifu hatua za Urusi za kuondoa baadhi ya wanajeshi wake akisema ni ishara inayotoa matumaini. Kabla ya mkutano wake na Putin, Scholz alikutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky siku ya Jumatatu mjini Kiev.

FLsrfMmX0AEPWOr.jpg
 
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amemueleza Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz kuwa nchi yake haitaki vita barani Ulaya. Viongozi hao wawili walikutana jana mjini Moscow ikiwa ni juhudi za hivi karibuni za kuepusha vita...
Putin wants Soviet back Anasema hivyo ili watu wa relax Halafu wavamie .Putin Si mtu wa kumchezea.KGB director alikuwa he writes dossier ,he can destroy you completely
 
Russia akiigusa Ukraine anajua kabisa biashara ya bomba la gesi Europe inakufa ....kwahyo hawezi kabisa kujiharibia

20220216_131114.jpg
 
Urusi haina nia ya kuivamia Ukraine suala hilo linakazaniwa na Marekani kila kutwa ,hongera Sana kansela wa ujerumani mazungumzo yako na Putin matunda yameanza kuonekana
 
Putin wants Soviet back Anasema hivyo ili watu wa relax Halafu wavamie .Putin Si mtu wa kumchezea.KGB director alikuwa he writes dossier ,he can destroy you completely
Putin hataki kuirudisha soviet kama awali, anachopigania ni usalama wa taifa lake. Sintofahamu baina ya NATO na URUSI inafahamika na ina historia yake na athari yake inafahamika kwani historia yake ipo wazi. Uhasama huu bado upo pande mbili.

Ukraine ni nchi huru. Lakini kwa nini ujiwekeze kwenye tension kubwa ya kivita ilihali mnaweza mkashirikiana na kujikita kuimarisha uchumi zaidi? Hungary ni nchi iliyopakana na nchi zote mbili, yaani Ukraine na Urusi. Ni mwanachama wa NATO.

Walipoulizwa iwapo majeshi ya NATO yakitakiwa yawepo nchini mwao kukabiliana na pressure ya Mrusi nchini Ukraine walikataa. Walikataa! Kwa sababu nchi nyengine zipo mbali na tension hiyo! Hivyo athari ya aina yoyote ikitokea iwapo watajiingiza kwa namna yoyote nayo itawakumba.

Hivyo hapa watu wanaofanya mchezo mbaya dhidi ya haya yote ni wawili, NATO na UKRAINE. Kwa nini wasijikite kwenye kuimarisha na kuujenga uchumi imara baina yao? Kwa nini wanaanzisha vuguvugu ambalo uwezo wa kuepukika upo?
 
Urusi haina nia ya kuivamia Ukraine suala hilo linakazaniwa na Marekani kila kutwa ,hongera Sana kansela wa ujerumani mazungumzo yako na Putin matunda yameanza kuonekana
Juzi kati kuna interview ilifanyika kituo cha kurushia matangazo ya habari cha Australia. Mhojiwa alikuwa ni kamanda mstaafu wa jeshi la US. Alizungumza wazi kwa sasa US haina uwezo na wala haitotuma na wala haitoingilia kwa namna yoyote ikiwa kwa bahati mbaya Urusi ikitumia nguvu za kijeshi kuikabili Ukraine.

Kwa bahati mbaya hiyo Channel wameifuta interview hiyo.
 
Russia akiigusa Ukraine anajua kabisa biashara ya bomba la gesi Europe inakufa ....kwahyo hawezi kabisa kujiharibia

View attachment 2120937
Mjerumani si mjinga!

Kwa sasa ndiyo nchi yenye uchumi mzuri bara la Ulaya. Ndiye anayetumia gesi kwa wingi. Gesi wenzetu wanatumia kwa matumizi mengi. Urusi ndiye anayesambaza gesi nchini mwao. Kabla ya kuingia makubaliano ya kimkataba US aliweka pressure ili Ujerumani isisaini mkataba. Lakini Ujerumani si dhaifu, haipangiwi na ina maamuzi yake binafsi haswa ikiwa ni maslahi ya nchi yake. Gesi ya Urusi ni nafuu, gesi ya US ni ghali zaidi.

Kwa mtazamo wangu juu ya Ujerumani kwa jinsi inavyokuwa na msimamo wake kwa maslahi ya Uchumi wa Taifa lake amekuwa akitofautiana na US. Hivyo, sioni Mjerumani akivunja huu mkataba ikiwa kwa bahati mbaya vita itatokea baina ya Urusi na Ukraine. Bali atatafuta namna nyengine ya kutatua hiyo changamoto kama walivyofanya sasa kuzungumza na Putin.
 
Putin wants Soviet back Anasema hivyo ili watu wa relax Halafu wavamie .Putin Si mtu wa kumchezea.KGB director alikuwa he writes dossier ,he can destroy you completely
Hakuna kitu kama hicho imeisha hiyo watayamaliza
 
Back
Top Bottom