Putin: Hatutaki vita Ulaya, tuko tayari kwa mazungumzo

Putin: Hatutaki vita Ulaya, tuko tayari kwa mazungumzo

Mbona Rais Putin analindwa na wanajeshi waliozeeka hivyo, kwani uko kwa wenzetu awazingatii umri wa kustaafu nini?
 
Kashauriwa na intelligence yake kuwa amepaniwa sana
 
Putin hataki kuirudisha soviet kama awali, anachopigania ni usalama wa taifa lake. Sintofahamu baina ya NATO na URUSI inafahamika na ina historia yake na athari yake inafahamika kwani historia yake ipo wazi. Uhasama huu bado upo pande mbili.

Ukraine ni nchi huru. Lakini kwa nini ujiwekeze kwenye tension kubwa ya kivita ilihali mnaweza mkashirikiana na kujikita kuimarisha uchumi zaidi? Hungary ni nchi iliyopakana na nchi zote mbili, yaani Ukraine na Urusi. Ni mwanachama wa NATO.

Walipoulizwa iwapo majeshi ya NATO yakitakiwa yawepo nchini mwao kukabiliana na pressure ya Mrusi nchini Ukraine walikataa. Walikataa! Kwa sababu nchi nyengine zipo mbali na tension hiyo! Hivyo athari ya aina yoyote ikitokea iwapo watajiingiza kwa namna yoyote nayo itawakumba.

Hivyo hapa watu wanaofanya mchezo mbaya dhidi ya haya yote ni wawili, NATO na UKRAINE. Kwa nini wasijikite kwenye kuimarisha na kuujenga uchumi imara baina yao? Kwa nini wanaanzisha vuguvugu ambalo uwezo wa kuepukika upo?
Ulipotea sana Hammaz
 
Putin kwa heri na urusi yake tatizo nikwamba putin Yuko pekeake wezake wanaungana dhidi yake huo uchumi atakuja lini kuufanya utengemae ,bado soko la gesi anawategea watu wa ulaya magharibi
 
Mbona Rais Putin analindwa na wanajeshi waliozeeka hivyo, kwani uko kwa wenzetu awazingatii umri wa kustaafu nini?
Hao ndo best friend zake waliishi woote ujeruman mashariki nakufanya opareaheni mbalimbali wajamaa kwakweli na wanufaikaji wakubwa wautawala wa Putin. .........
 
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amemueleza Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz kuwa nchi yake haitaki vita barani Ulaya. Viongozi hao wawili walikutana jana mjini Moscow ikiwa ni juhudi za hivi karibuni za kuepusha vita.

Putin ameelezea utayari wa Moscow wa kufanya mazungumzo na Marekani pamoja na Jumuiya ya Kujihami NATO juu ya masuala ya usalama.

Kauli ya Putin imezidisha matumaini ya kupungua kwa mvutano na jirani yake Ukraine na uwezekano wa uvamizi, lakini Rais wa Marekani, Joe Biden amesema hawajathibitisha madai ya Urusi na kwamba bado kuna uwezekano wa uvamizi.

Kwa upande wake Kansela Olaf Scholz amesifu hatua za Urusi za kuondoa baadhi ya wanajeshi wake akisema ni ishara inayotoa matumaini. Kabla ya mkutano wake na Putin, Scholz alikutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky siku ya Jumatatu mjini Kiev.

Putini choka mbaya kila akiona mazungumzo ya kuzima vita ndo anayotaka, hakutegemea alichokikuta Ukrean mbaya zaidi hata huko Donbas atafurushwa anytime soon.,
 
Putini choka mbaya kila akiona mazungumzo ya kuzima vita ndo anayotaka, hakutegemea alichokikuta Ukrean mbaya zaidi hata huko Donbas atafurushwa anytime soon.,
Unadhani ni rahisi kama unavyobinuliwa kichuguu
 
Back
Top Bottom