Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Rais wa Urusi anakabiliwa na tishio kubwa zaidi kuwahi kutokea kwa utawala wake katika miaka 23 yote aliyokuwa akiongoza taifa lenye nguvu ya nyuklia.
Ni jambo la kushangaza kuona jinsi alivyoweza kuendeleza udhibiti kamili kwa muda wote huo; sehemu muhimu ya kuonesha utawala wake wa kiimla, imeporomoka ghafla.
Lilikuwa jambo lisiloepukika na lisilowezekana. Lisiloepukika, kwani usimamizi mbaya wa vita ulimaanisha kuwa mfumo pekee wenye uzio imara na wenye kinga ya kukosolewa kama Kremlin ungeweza kuvuka hali hiyo mbaya.
Na lisilowezekana, baada ya wanaomkosoa Putin kupotea, au kuanguka kutoka madirishani, au kupewa sumu kikatili.
Lakini sasa jeshi la tano kwa ukubwa duniani ipo kwenye wikiendi inayohusisha wanajeshi kugeukana wenyewe na kuuana - ndiyo kitu pekee kinachoweza kuokoa Moscow ya wakubwa isiporomoke.
Ukraine inaweza kuwa inasherehekea muda huu mbaya wa uasi ndani ya safu za Urusi. Huenda ukabadilisha mwelekeo wa vita kwa faida ya Kyiv, lakini uasi mara chache unamalizika Urusi - au mahali pengine kwa matokeo waliyokusudia.
Prigozhin anaweza asishinde, na msingi wa udhibiti wa Kremlin huenda usiporomoke, lakini Putin dhaifu anaweza kufanya mambo kwa kukurupuka ili kuthibitisha nguvu yake.
Anaweza kukataa ukweli wa kushindwa kwenye vita hii na Ukraine katika miezi ijayo. Huenda asiwe na ufahamu wa kina wa kutokuridhika kati ya vikosi vyake vya kijeshi, na kukosa udhibiti sahihi wa vitendo vyao.
Nafasi ya Urusi kama nchi inayohusika na silaha za nyuklia inategemea utulivu katika ngazi za juu.
Kuna mengi yanayoweza kwenda vibaya kuliko yanavyoweza kwenda vizuri, akini ni vigumu kufikiria kuwa kamwe utawala wa Putin utarejea katika kiwango chake cha awali cha udhibiti kuanzia sasa.
Na ni jambo lisiloweza kuepukika kuwa kutakuwa na msukosuko na mabadiliko zaidi yanayokuja
Citizen Digital