Putin kwa mara ya kwanza alia hali ilivyo ngumu kwenye uwanja wa mapambano huko Ukraine


Majenerali wa Urusi hawawezi kukubali hii vita ikuzwe mpaka kufikia matumizi ya nyuklia, maana ni dhahiri sasa hivi Putin amelewa hadi kilichobaki ni matumizi ya nyuklia, na ndio kitu akijaribu kitasababisha Urusi iangamizwe.
Kingine unapaswa ufahamu Ukraine bado haijapata full support ya West, kuna zana za aina nyingi hawajapewa, hata Magharibi pia wanajaribu mbinu za kumlemaza Mrusi bila kufanya provocation ya Urusi yote.

Wanachokifanya Magharibi ni kumtoa pumzi Mrusi akiwa ndani ya Ukraine na kuhakikisha amelemazwa kimya kimya bila kumfuata kule Urusi, na hicho Ukraine wamefanikisha pakubwa. Hao vijana 200,000 waliokusanywa kutoka mitaani acheni kuwategemea, hamna jipa wanachokifanya ila kuongeza mizoga Ukraine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…