Puuzeni taarifa ya Nipashe, hakuna uchotaji fedha BoT

ila we mzee naamini kabisa utaanza kuchomwa hapa hapa duniani yaani utaanza kuteseka hapa hapa duniani halafu kuzimu ni muendelezo tu
Hivi hizo hela mnazoiba hamuwaonei huruma watanzania?
Mamilioni ya watoto wa kitanzania wanasoma shule chakavu hapa nchini, huduma za afya ni ghali sana kwa mwananchi wa kawaida, mfumuko wa bei ni mkubwa sana kwa maisha ya Sasa, miradi lukuki inasuasua na kama inatekelezwa basi sio kwa wakati kwa sababu ya ufisadi, WIZI, uhujumu na ubadhirifu uliopitiliza uovu, lakini nyie mnaona sawa tu mateso ya watanzania kunufaisha matumbo yenu

MUNGU ninayemuamini ni mkuu sana hakika hataacha haya yapite katika JINA LA YESU KRISTU ALIYE HAI

kila kilichofichwa kitafunuliwa na hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe
Dr. Mwigulu Nchemba
 
Siku moja inakuja, nyie endeleeni kuchuma na kufaidi na watoto wenu
 
Jamanii jamanii waja mna nongwa mnataka mpaka ndugu waziri ajute kuja Jf kuanzisha Uzi.
Mkuu Nuzu, Nuzulati , kiukweli baadhi ya wana jf sio wastaarabu kabisa, badala ya appreciation ya uwepo wake, wanataka kumkera, hata mimi nina hoja zangu kumhusu, kila nikimuuliza, humuoni tena!, baada ya kulijua hilo, simuulizi tena!, I just appreciate uwepo wake.
Tujifunze kuwa appreciative!.
P
 
Raisi Samia ndio Muasisi wa matumizi ya anasa Serikalini
 
Yaani yeye kukanusha ufisadi wake tuna appreciate nini hapa
 
Ndio kama umekuja kututhibitishia tena hizi tuhuma nazo zinakaukweli fulani.

Unachanganya sana maelezo, umeeleweka mpaka hapo kwenye serikali inaweza kukopa short term loan, kufidia temporaryy budget short fall; kwa mujibu wa sheria.

Unapotuvuruga ni kusema short term loan (imegeuka kuwa ‘treasury bond), ambalo ni deni la muda mrefu mnalolipia riba. Na mkopo wenyewe mshaujumuisha kwenye deni la taifa.

Maana yake huo mkopo uliotakiwa kuwa wa (wa short term) kawaida muda wake ni maximum ya miezi 12 deni liwe limelipwa. Lengo likiwa kufidia temporary ‘budget shortfall’ mkipata makusanyo mrudishe hilo deni.

Mwaka umepita bado deni alijalipwa BoT mpaka leo. Sanasana mmeamishia kwenda kwenye long term debt; si ndio uchotaji wenyewe huo wa akiba kutoka BoT.
 
Lilikuwa Gazeti la Mfanyakazi ambalo Stan Katabalo alikuwa ni mwandishi wake.Aliuliwa kwa Kufuatilia sakata la Loliondo Gate (OBC) ambayo leo wanamiliki Nchi ndani ya Tanganyika yetu.
 
Pascal, kama kweli wamekopa kutoka BOT, una uhakika gani kuwa zimekopwa na kulekezwa kwenye matumizi yaliyokusudiwa?

Taarifa ya Nipashe ni vizuri pia tukaipata badala ya kusikia habari ya upande mmoja tu.
 
Yaani tunshukuru mtu kutimiza wajibu wake!
Hakika safari ni ndefu mno!
Tumshukuru kwa uwepo wake jf, Waziri kuingia jf na kujibu hoja sii miongoni mwa wajibu wake!, Waziri hawajibiki jf, hivyo uwepo wake humu ni ametuheshimu sana, turudishe heshima, Mawaziri zaidi waingie, juzi nimemuona Gerson Msigwa , hii ni heshima kubwa kwa jf, lets be appreciative.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…