Puuzeni taarifa za uteuzi wangu. Mimi ni Mwanachama wa kawaida na wala sina cheo ndani ya CCM

Biblia inasema asiyefanya kazi na Asile

Kuna shida gani iwapo umeajiriwa Serikalini/Chamani ama Private Sector?

Mbona kabla yako wewe Kuna watu walikwepo humu 24/7 wakafanya kazi kazi zao baada ya awamu kubadirika nao Kasi ikabadirika

Hii ni awamu yako, baada ya Kizimkazi festival huenda ikaja timu nyingine kusave the same purpose Kwa awamu nyingine pia.
 
Ndio maana nimesema ya kuwa kazi yangu ni kilimo na mimi ni mkulima mpaka muda huu na wala sina kazi au ajira ya aina yoyote ile ndani ya CCM au serikalini.
 
Mama akuangalie bwana lucas ..maaana tumekutukana sana humu jamvini ila bado uko ngangari hujakata tamaa kutetea chama chako.Ww ni mzalendo sana wa chama cha mapinduzi.Viongozi mpeni kijana hata u afisa mtendaji wa kata.😎
 
Huu ndio uzalendo wa kweli kwa taifa lako. Nakupongeza, nakuunga mkono, ubarikiwe sana.
P
 
We elewa nimeelewa.
Asante kama umeelewa. sasa nataka nikujibu swali lako kwa kusema kuwa nikipewa nafasi ya kutumikia sehemu yoyote nipo tayari kufanya kwa moyo wangu wote na kwa weledi wa hali ya juu sana kwa ajili ya kuleta matokeo chanya.Lakini sipo jukwaani au kuandika jukwaani kwa ajili ya kupewa uteuzi .maana lazima ufahamu ya kuwa Uongozi unatoka kwa Mungu Mwenyewe.
 
Asee mnajitekenya na kucheka wenyewe🤔
 
Swahiba unajipigia chapuo mwenyewe baada ya kuona wamekuchunia.

Ila ikitokea wakakuteua tu mimi nitakuwa nashusha uzi kwa niaba yako kila siku, nyuzi za kutoa watu machozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…