JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Zoezi la kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Mwenyekiti na Wajumbe wa serikali ya mtaa kwenye Mtaa wa Mailimoja B halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoa wa Pwani limelazimika kusimama kwa zaidi ya masaa matatu baada ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) kufika kwenye ofisi hiyo kwaajili ya kuchukua fomu na kuambiwa tayari kuna mgombea kutoka chama hicho ameshachukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti.
Katibu wa CHADEMA tawi la Tangini Leons Kaloli amesema wamefika Ofisi ya Mtaa Mailimoja B Oktoba 28 majira ya saa tano na kuonana na mtendaji Suzana Awiti kuchukua fomu na kuambiwa kuwa tayari Kuna mgombea wao ameshachukua fomu wakati hawamfahamu .
"Hiyo barua wanadai kuwa mimi ndiye nimeisaini lakini hiyo saini nilivyoingalia sio ya kwangu imefojiwa hivyo ni lazima nichukue hatua za kisheria" alisema.
Baada ya mvutano wa muda mrefu Afisa uchaguzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkhusin Saidi alipigiwa simu na kufika kwenye ofisi hiyo ili kulitolea ufafanuzi suala hilo ambapo Katika ufafanuzi wake afisa huyo alisema kuwa mtu anayegawa fomu hawezi kutambua chama kipi kina mhuri gani na badala yake kazi yake ni kugawa fomu.
Chanzo: Wasafi FM