Q-Net na Forever Living zimenipotezea marafiki zangu wa karibu

Q-Net na Forever Living zimenipotezea marafiki zangu wa karibu

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Mara ya kwanza nasikia kuhusu Forever Living ilikuwa mwaka 2005 kipindi hicho imepamba moto sana. Kulikuwa na mtoto mmoja mkali sana chuo nlikuwa namfukuzia.

Naye akaona atumie nafasi hiyo kuniunganisha Forever Living nikamkubalia ili kwanza nimle halafu tutajuana mbele kwa mbele, kweli nikaenda kwenye semina elekezi moja wapo siku hiyo nikaonesha utayari sana wa kujiunga naye akafurahi maana ningekuwa mteja wake wa kwanza.

Tulipotoka kwenye semina jioni nikampitisha sehemu tukala ,tukanywa nikamla kwa mara ya kwanza. Chuo nikamrudisha kesho yake. Sikujiunga Forever Living nilijiunga kwake yeye kama yeye.

Miaka 8 baadaye dada mmoja mrembo sana alianza nitafuta akitaka tuonane ana maongezi mazito sana kila nlipomuuliza maongezi yanahusu nini hakutaka kunambia kwa dada mwenyewe mashallah nikawaza "pengine huyu dada anataka nyanjo" maana mara ya mwisho tulionana UDSM nikiwa namfukuzia akagundua namtumia rafiki yake tukaachana hapo.

Miaka nane baadaye ndo ananitafuta kwa udi na uvumba. Siku moja akanibembeleza sana kuwa Ijumaa nisikose kuonana naye sehemu ya kuonana naye ni pale Sinza kilipo Chuo cha Kilimanjaro.

Nikatoka mapema kazini Town nikisema mtu hakati wito anakataa aliloitiwa. Ingawa kila nikimuuliza huyu dada mada ya kutaniko letu ni nini anasema we njoo tu bwana, usiniangushe

Siku hiyo Ijumaa nikatoroka kazini nikiwa na shauku mrembo ananiitia nini week tatu zote anataka tuonane.

Kufika akanielekeza nipande juu kwenda ndani nikamkuta huyo dada na watu wengine kama wamemaliza issue flani sasa wanaconclude kwenye tuvikundi. Akanambia nikae sehemu pembeni, nikakaa nachezea chezea simu.

Baada ya muda akavuta kiti akawaita na wenzie wawili warembo waje kukaa ile meza, akanisalimia na kutambulisha wenzie na kutaka kuanza kunambia habari za Forever Living.

Kwa mwaka ule hamna siku ambayo nilikasirika kama ile nilianza kutetemeka kwa hasira na kumuuliza "ndo siku zote nakuuliza unaniitia nini kumbe unaniitia huu upuuzi? Kwa nini umenipotezea muda?" Nliamka na kuondoka.

Toka siku hiyo hatukuwasiliana tena. Nlikuwa namuona tu kwenye mitandao picha zake akionekana alivyochange toka kuwa mnene hadi kuwa mwembamba.

Mwaka huu mwanzo tena dada mmoja tumefahamiana kwa ajili ya mambo ya kazi tukawa marafiki wa penzi sana na huyu dada naye ni mashallah hasa kwa umbo, naye akaanza kunambia anahitaji tuonane, nikawa najiuliza ana nini analotaka tuonane "sehemu tulivu" maana hofu yangu ilikuwa nisije nikamtokea bure na wakati tunaheshimiana.

Jumatano moja nikamwambia nipo tayari kupata naye lunch. Tukatafuta hotel moja tulivu tule tuongee, baada ya maongezi ndo ananambia habari za Q-Net. Nikagundua yeye wameshampiga anatafuta pa kulipizia ana saa ya milions of money.

Nikamsikiliza akanisimulia jinsi watu wanavyotajirika n.k akasimulia kwa shauku na bashasha, akiniasa hayo anayombia ni siri sana hakupaswa niambia ila kuna sehemu itabidi anipeleke mikocheni kwa maelezo zaidi jumamosi.

Sikutaka muumiza. Nilimsikiliza na mwishowe nikamwambia ntamtaarifu, alipoona sina uelekeo kwa sasa hata nikipiga simu hapokei ni kama ameshanichukia. Nawaza why anichukie kwa pesa zangu mwenyewe?

Binafsi sitaki na sipendi kufanya kazi yoyote ambayo inaonekana ni rahisi kunipatia pesa. Utapeli huanzia hapo, sijawahi tapeliwa na sitaki kuanza sasa. Hakuna maisha rahisi. Kuna mtu anakuja anakwambia niliacha kazi bank, chuo, udaktari, sijui kampuni gani ili nifanye hii Forever, Q-Net and the like.

Ukimtizama anavyokubembeleza mpaka anataka kulia ili ujiunge unagundua alishapigwa naye anataka akupige. Mmoja alikuja ofisini akanambia aliacha upolisi ili afanye Forever Living, nilimtizama alivyochoka viatu vina vumbi, vimeisha upande, ameloana na jasho, midomo imemkauka.

Nikamwambia alifanya kitendo cha kipumbavu sana maana sasa anapata taaabu yoote hiyo kwa kuwa hana kazi ya maana. Jamaa aliondoka mnyonge sana. Ashakum si matusi dont let yourself fucked by these people and their fascinating stories. Maisha si rahisi hivyo.
 
Nimevumilia kutukana ofisi nzima ya qnet baada ya kuniita kilaghai kuniambia upuuzi huo. Kilichosaidia miongoni mwao kuna mtu tunaheshimiana. reception wanedanganyishia mapicha ya maghorofa ukutani unadhani ni ofisi ya waandisi majengo.

Kama mimi mkuu! We acha tu
 
Kuna dem amenitafuta sana wiki ya pili hii simjui ila anapiga simu anasema tuonane kuna ishu ya maana tukajadili lakini hasemi ni nini.sasa namvutia upepo tu amesema weekend hii tukutane makumbusho.ila nazani ni hizi mambo
 
Kuna dem amenitafuta sana wiki ya pili hii simjui ila anapiga simu anasema tuonane kuna ishu ya maana tukajadili lakini hasemi ni nini.sasa namvutia upepo tu amesema weekend hii tukutane makumbusho.ila nazani ni hizi mambo
Kama ni makumbusho hapo anataka kukupeleka kwa wale Aim Global ndo huwa nawaona vijana wanashinda pale wamevaa suti zao na simu kibao mkononi
 
Mie kuna jamaa yangu aliingia kwa mikwala licha ya kumsihi maana mie nayajua Hayo lakini wapi, jamaa likajitosa Q-net siku za kwanza kanisumbua sana na mapicha ya seminars mpaka akaenda mbali kusema ameagiza BMW X3 , ukabidi niogope hata kuonana nae nikiwa na kijicrown changu,.....tukapotezana kama mwezi na nusu sijui ndio alikua busy, majuzi kanikumbuka cha kwanza anasema nimuazime 20,000/= kanikomalia siku nzima mpaka nikamtumia....

Nkajiuliza inamaana Q-net mapene yameisha au
 
Kuna mwalimu wangu wa A level nlikua namuheshimu kweli...mwezi uliopita akanipigia simu anasema tuonane . Me nikajua anataka nikafundishe kwenye tution center yake. Kufika pale wana mbwembwe balaaaaaaa yaan kama sio mtoto wa mjini unapigwa hivihivi
Ofisi yenyewe imechoka balaaa haina hata meza halafu ananishawishi nijiunge nao niwe nalipwa millioni 9 kwa wiki. Ila to my amazement nimekuta hadi vijana wa chuo wamezama kwenye huo upuuzii......NETWORK MARKETING NI PYRAMIDAL SCHEME KAMA ZILIVYO NYINGINE USIIBIWE KIJINGA
 
.....uliwashawishi wakijiunga watapata mahelaaaa....wakajiungaaaa...biashara ikadodo....na awamu hiii hamna hela za KIUJANJA JANJAAaaaaa
 
Back
Top Bottom