Q-Net na Forever Living zimenipotezea marafiki zangu wa karibu

Q-Net na Forever Living zimenipotezea marafiki zangu wa karibu

Nowadays kuna aim global na eternal, yaani hawa jamaa wanachukulia njaa zetu kama fursa
 
mkuu hakuna biashara inalipa kwa haraka hivyo,Jirani yangu alikuja na kunihamasisha balaa nilikataa kwenda hadi tukawa hatuonani nikamwambia mimi nafuga tu bwana haya mambo yenu siyawezi .Juzi karudi kaniambia dogo uliona mbali nikamwambia brother nikupatie mayai mangapi mkuu.Hizi biashara nyingi za mtandao ni utapeli tu
 
Kuna dem amenitafuta sana wiki ya pili hii simjui ila anapiga simu anasema tuonane kuna ishu ya maana tukajadili lakini hasemi ni nini.sasa namvutia upepo tu amesema weekend hii tukutane makumbusho.ila nazani ni hizi mambo
makumbusho wapo wale wanajiita alliance in motion global (aim global). ile siku jamaa aliniita wala hakuniambia kama ni hao, alisema uje makumbusho kuna seminar nzuri sana itakusaidia alaf nikakutana na hao, nilikaa kwa vile ni rafiki yangu ila nilichukia mnoo.
 
kuna wengine wanajiita helpinghands ebwana eehh wakianza hesabu zao utajikuta imekula kwako
 
Hakuna pesa ya kirahis namna hiyo. Binafsi nimeshakuwa approached na wadada wa aina hiyo lakin napiga chini.

All wanachoongwa ni fantasy tu
 
Kuna mwalimu wangu wa A level nlikua namuheshimu kweli...mwezi uliopita akanipigia simu anasema tuonane . Me nikajua anataka nikafundishe kwenye tution center yake. Kufika pale wana mbwembwe balaaaaaaa yaan kama sio mtoto wa mjini unapigwa hivihivi
Ofisi yenyewe imechoka balaaa haina hata meza halafu ananishawishi nijiunge nao niwe nalipwa millioni 9 kwa wiki. Ila to my amazement nimekuta hadi vijana wa chuo wamezama kwenye huo upuuzii......NETWORK MARKETING NI PYRAMIDAL SCHEME KAMA ZILIVYO NYINGINE USIIBIWE KIJINGA

Kwenye RED unauhakika gani kuwa hao noi vijana wa CHUO, maana mtu yeyote aweza kujitambulisha kuwa ni kijana wa CHUO wakati SIYO!
 
Binafsi sitak na sipend kufanya kazi yoyote ambayo inaonekana ni rahis kunipatia pesa.utapeli huanzia hapo.sijawah tapeliwa na sitak kuanza sasa. Hakuna maisha rahisi. Kuna mtu anakuja anakwambia nliacha kazi bank,chuo,udaktar,sijui kampuni gan ili nifanye hii Forever,Qnet and the like.
Mimi binafsi mwaka jana walinipiga kwenye D9, Sitaki tena kusikia hizi longolongo za Qnet.Shemeji yangu yeye ndio kwanza ameingizwa huko na kaingiza hela zake, akanialika nikaenda kuwasikiliza na kuwasilikiza nikasema hawa wapuuzi kabisa yaani kwa tumaneno twao uto ndio niiingize mkwanja wangu!!!??? Hapa hata machungu ya D9 Hayajaisha. Hawanipati kabsaaaa.
 
Woii, Weekend ilopita tu m/city nimejichokea ile mbaya akaja mdada kavaa vizurii ananukia,ananiambia habari zake za semina kuanngalia tshirt imeandikwa FL afu ansema mm baba angu aliumwa cancer akapona,Yani jinsi nimechoka nilimuangalia tu.
 
Nimevumilia kutukana ofisi nzima ya qnet baada ya kuniita kilaghai kuniambia upuuzi huo. Kilichosaidia miongoni mwao kuna mtu tunaheshimiana. reception wanedanganyishia mapicha ya maghorofa ukutani unadhani ni ofisi ya waandisi majengo.
Halafu wanaongea habari ya kampuni yetu, wakati hata wenye kampuni hawawajui.
Walivyoniambia habari za kufunguliwa akaunti kwenye mtandao nikajua tu hawa kama jamii ile ile ya D9.
 
Kuna kidem changu cha chuo kwasasa yupo likizo ila yupo bze sana namaswala ya pesa yn kama yupo ofis flan ivi zamichongo yapesa sasa leo ndo nimepata jibu mana juz kati alinitext "Habari Majan Samahani kesho kama hutojali naomba Uje ofcn Kwetu saa nane kuna program muhimu kwa wageni nakuomba nimekununulia ticket" ila kila nikimuuliza ofis zao zinahusika na nini hajawai kuniambia
 
Naulizia kuhusu bitclub advantage faida kila siku bila network, na AWS Mining "utajiri nje nje", kuna watu wananibembeleza mtumishi nijiunge, naomba mchango wa mawazo.

Kuna mmoja nimemuomba anipe kianzio, faida itakayopatikana tugawane nusu kwa nusu, amenitukana kimoyo moyo!!
 
Back
Top Bottom